Tafuta

2019.06.08 scuola in Sud Sudan, Loreto School, lasalliani

UN:Zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili

WHO ilizindua mwongozo mpya wa kupanua wigo wa huduma za afya ya akili.Shirika hili linaamini kuwa mwongozo huu utachangia juhudi za kimataifa za kupanua wigo wa huduma za afya ya akili zinazopatikana kwa urahisi,kwa gharama nafuu na kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.

Umoja wa Mataifa

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO) limezindua mwongozo mpya wa kusaidia nchi na mashirika kuongeza upatikanaji wa huduma za afya ya akili kupitia mbinu za msaada wa kisaikolojia zinazotegemea ushahidi wa kisayansi. WHO ilisema zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili, huku wengi wakikosa huduma stahiki. Mwongozo huo unatoa maelekezo ya jinsi ya kuanzisha na kutekeleza huduma za msaada,zikiwemo zinazotolewa kwa njia za kidijitali au kwa msaada wa wahudumu wasio wataalamu lakini waliopata mafunzo.

Mbinu za huduma za afya ya akili

Shirika hilo linaeleza kuwa mbinu hizo zimeonesha mafanikio katika kupunguza dalili za msongo wa mawazo na wasiwasi, hasa katika maeneo yenye rasilimali chache na yaliyoathiriwa na migogoro. Mwongozo huo pia unaelekeza utekelezaji wa hatua mbili za matibabu za WHO,  wa "Step-by-Step" yaani  “Hatua kwa Hatua” na "Doing What Matters in Times of Stress"  yaani "Kufanya Yaliyo Muhimu Wakati wa Msongo wa Mawazo", ambazo tayari zinatumika katika huduma za kitaifa nchini Lebanon na Thailand. WHO inaamini kuwa mwongozo huu utachangia juhudi za kimataifa za kupanua wigo wa huduma za afya ya akili zinazopatikana kwa urahisi, kwa gharama nafuu na kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.

Imesasishwa tarehe 3 Juni 2026 saa 7.10 mchana na Angella Rwezaula.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

03 Juni 2026, 13:08