Tafuta

Rais Macron wa Ufaransa alikuwa mwenyeji wa Mkutano wa G7 huku Evian. Rais Macron wa Ufaransa alikuwa mwenyeji wa Mkutano wa G7 huku Evian.  (AFP or licensors)

Katika mkutano wa G7 huko Evian,viongozi wanakutana kuhusu Iran,Ukraine na AI

Makubaliano kati ya Marekani na Iran yalikaribishwa katika mkutano huo katika hoteli ya Ufaransa.Viongozi wa mataifa saba yenye nguvu pia walionesha nia yao ya kuhakikisha usalama wa Mlango-Bahari wa Hormuz. Mkutano huo pia ulilenga utawala wa akili unde na usaidizi kwa Ukraine.

Marco Guerra na Angella Rwezaula – Vatican.

Muunganiko wa Mkataba wa Marekani na Iran, usaidizi kwa ajili ya Ukraine na Hati kuhusu Akili Unde( AI) zilikuwa mada moto moto katika mkutano ambao kwa hakika uliakisiwa na utafutaji wa umoja kati ya Ulaya na Marekani, huku viongozi wa Bara la Kale(Ulaya) wakijaribu kuirudisha Washington katika mfumo wa pande nyingi kuhusu masuala muhimu ya kimataifa. Ni katika Mkutano mkuu wa viongozi wa kundi la nchi saba zinazoongoza kiviwanda duniani kote ziitwazo kwa jina(G7). Kupitia Mkutano wa Viongozi hao wa G7  kwa 2026 uliofanyika huko  Evian, nchini Ufaransa, viongozi hao vile vile walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa yakiwemo amani na usalama duniani, utulivu wa uchumi wa dunia, ukuaji wa uchumi pamoja na maendeleo ya teknolojia zinazoibukia.

Muunganiko wa Mkataba wa Marekani na Iran

G7 ilikaribisha makubaliano ya Marekani na Iran, ikiyaita "fursa ya kihistoria"ya kuzuia Tehran kupata silaha za nyuklia na kushughulikia vitisho vya kikanda na makombora. Katika taarifa hiyo, viongozi hao walionesha utayari wao wa kuchangia katika utekelezaji wa makubaliano hayo na kuunga mkono makubaliano ya kidiplomasia "madhubuti na ya kina" yaliyofuata. Rais Macron wa Ufaransa  aliyaita "makubaliano bora." Viongozi mbalimbali pia walionesha nia yao ya kujitolea kwa usalama katika  Mlango-Bahari wa Hormuz.

Usaidizi kwa Ukraine

Katika tamko la mwisho la pamoja, viongozi hao saba pia walithibitisha tena "uungaji mkono wao usioyumba" kwa Ukraine, wakijitolea kuongeza usambazaji wa ulinzi wa anga, vizuizi, na uwezo wa masafa marefu. Maandishi hayo pia yanatoa wito wa kuongezeka kwa shinikizo kwa uchumi wa vita wa Urusi, "ikiwa ni pamoja na" sekta za mafuta na gesi. Mwenyeji Rais Macron aliita makubaliano hayo "maendeleo halisi" na "sharti la ufanisi wetu wa pamoja katika kuhakikisha mafanikio ya watu wa Ukraine katika vita hivi vya upinzani."

Hati ya AI

Haikuwa ulinzi tu uliojadiliwa. G7 iliweka msingi wa ushirikiano imara kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya kwa ajili ya utawala wa akili unde (AI). Hati ya mfumo inalenga kuanzisha sheria za maadili, viwango vya usalama, na miongozo ya pamoja kwa ajili ya maendeleo ya teknolojia.

Mkutano wa G7

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

 

18 Juni 2026, 15:27