Tafuta

2019.04.16 Spighe di grano, alimentazione, nutrizione, Fao, grano, fame nel mondo, agricoltura

FAO:Kuwekeza mapema kuna faida ya kulinda mifumo ya chakula Kusini mwa Afrika

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumatatu tarehe 22 Juni mjini Roma Italia na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO,)limetaka uwekezaji wa hatua za mapema wa kulinda mifumo ya chakula Kusini mwa Afrika.Shirika hilo limebainisha kuwa kuwekeza kuna manufaa makubwa kiuchumi,ambapo kila dola moja inayowekezwa katika hatua za kujiandaa na majanga inaweza kuokoa hadi dola saba ambazo zingetumika baadaye kukabiliana na hasara na athari za dharura.

Umoja wa Mataifa

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limezitaka nchi za Kusini mwa Afrika kuongeza uwekezaji wa mapema katika kilimo, usimamizi wa maji na mifumo ya chakula ili kupunguza athari za majanga ya hali ya hewa yanayochochewa na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa  Jumatatu tarehe 22 Juni  2026 mjini Roma Italia na FAO, uwekezaji wa hatua za mapema una manufaa makubwa kiuchumi, ambapo kila dola moja inayowekezwa katika hatua za kujiandaa na majanga inaweza kuokoa hadi dola saba ambazo zingetumika baadaye kukabiliana na hasara na athari za dharura. Haya yamejiri siku ambayo Baba Mtakatifu Leo XIV alitembelea Makao makuu ya  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango na Chakula (WFP) ambalo ni moja ya washirika wa FAO.

Shirika hilo linaeleza kuwa hatua kama usambazaji wa mbegu zinazohimili ukame, ulinzi wa mifugo na utoaji wa tahadhari za mapema zimeonesha uwezo mkubwa wa kulinda mavuno, mali za wakulima na usalama wa chakula katika jamii zilizo hatarini. FAO inaonya kuwa kuchelewa kuchukua hatua husababisha gharama kubwa zaidi za kiuchumi na kijamii. Kupotea kwa mazao na mifugo huongeza umaskini, huathiri lishe ya kaya nyingi na kudhoofisha uzalishaji pamoja na uthabiti wa uchumi wa nchi husika. Licha ya sekta ya kilimo kuchangia sehemu kubwa ya uchumi katika nchi nyingi za Kusini mwa Afrika, FAO inabainisha kuwa matumizi ya miundombinu muhimu kama mabwawa, mifumo ya umwagiliaji na rasilimali watu bado hayajafikia uwezo wake kamili. Wakulima wengi pia wanaendelea kukumbwa na changamoto za upatikanaji wa masoko, fedha na mifumo ya kupunguza hatari za uzalishaji.

Miradi ya uwekezaji kwa wakulima

Kupitia mpango wa Mkono-kwa-Mkono na ushirikiano na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) FAO imesaidia kuandaliwa kwa miradi ya uwekezaji katika umwagiliaji, kilimo chenye mnepo dhidi ya  tabianchi, uchakataji wa mazao na biashara kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kuimarisha ustahimilivu wa mifumo ya chakula. FAO pia imehimiza mabadiliko kutoka mfumo wa ufadhili wa dharura unaotolewa baada ya majanga kutokea kwenda mfumo wa ufadhili wa mapema unaounganishwa na mifumo ya tahadhari za mapema, ili fedha ziweze kutolewa mara tu viashiria vya hatari vinapobainika.

Changamoto za tabianchi:ukame mafuriko ongezeko la bei katika masoko

Shirika hilo linasisitiza kuwa changamoto za tabianchi kama ukame, mafuriko na mishtuko ya masoko huvuka mipaka ya nchi, hivyo ushirikiano kati ya serikali, taasisi za fedha, washirika wa maendeleo na sekta binafsi ni muhimu katika kujenga mifumo imara ya chakula. FAO imehitimisha kuwa ushahidi wa kisayansi, teknolojia na fursa za uwekezaji tayari zipo, na kwamba hatua za haraka pamoja na dhamira ya kisiasa zinahitajika sasa ili kulinda maisha ya mamilioni ya watu na kuhakikisha usalama wa chakula wa siku zijazo katika Kusini mwa Afrika.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

23 Juni 2026, 10:09