Tafuta

Lebanon inageuzwa vifusi. Lebanon inageuzwa vifusi.  (AFP or licensors)

UNICEF yaomba kusitisha mapigano nchini Lebanon

Katika siku 46 zilizopita,takribani watoto 172 wameripotiwa kuuawa,661 wamejeruhiwa na zaidi ya 415,000 wamelazimika kuhama makazi yao.Ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kusaidia watoto(UNICEF) sehemu ya Lebanon.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kupitia mtandao wake wa X wa UNICEF huko Lebanon,  wa Shirika la Umoja wa Matafia la  Kuhudumia watoto(UNICEF) linakaribisha tangazo la kusitisha mapigano la usiku wa 20 Aprili usiku nchini Lebanon. Hatua hii inawakilisha fursa muhimu ya kuwalinda watoto na familia ambazo zimepitia mateso makubwa. Katika siku ya 46 zilizopita, watoto wamelipa gharama kubwa. Kulingana na ripoti, karibu  watoto 172 wameuawa na 661 wamejeruhiwa. Zaidi ya watoto 415,000 wamehamishwa makazi yao.

Kusitisha mapigano lazima kuheshimiwa

Kusitisha mapigano huku lazima kuheshimiwe. Tunarudia wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa pande zote kuheshimu kikamilifu kusitisha mapigano na sheria ya kimataifa wakati wote. Watoto wanahitaji zaidi ya utulivu wa uhasama: wanahitaji nafasi halisi ya kupona. Urejeshaji utachukua muda, kwani uharibifu mkubwa wa nyumba, hospitali, shule, na miundombinu utapunguza upatikanaji wa watoto kwa huduma muhimu.

Kurejesha huduma muhimu

Kurejesha elimu, huduma za afya, mifumo ya maji, na huduma zingine za msingi ni kipaumbele. UNICEF inaendelea kufanya kazi na Serikali ya Lebanon na washirika kushughulikia mahitaji ya dharura na kuunga mkono mchakato wa urejeshaji. UNICEF inatoa wito kwa nchi zote na wafadhili kujiunga haraka na juhudi hizi ili kuhakikisha watoto wanapata ulinzi, utunzaji, na fursa wanazohitaji ili kupona, kujenga upya maisha yao, na kufikia uwezo wao kamili.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

21 Aprili 2026, 15:00