Siku ya Radio Duniani:Mwanadamu aongoze Akili Unde!
Andrea De Angelis - Milano
"Ningependa kuingia kwenye nyaya za radio. Na kuruka juu ya paa za jiji. Kukutana na maneno ya kilugha. Kuchanganyika na harufu ya kahawa," aliimba Lucio Dalla, bila kuficha nguvu ya mawasiliano isiyozuilika ya radio, ambayo ilisherehekewa , Jumatatu tarehe 9 Machi 2026 katika toleo la VI la Siku ya Radio Duniani. Tukio la Italia lililojikita kwa Siku ya Radio Duniani, lililoanzishwa na UNESCO mwaka 2011 na kurudiwa kila ifikapo Februari 13 ya kila mwaka.
Radio na Akili Unde
"Akili Unde ni chombo. Sio sauti." Mada iliyochaguliwa na shirika la Umoja wa Mataifa kwa Siku ya Radio Duniani ya mwaka huu 2026 ilikuwa kiongozi wa kawaida wa majadiliano na mawasilisho jukwaani katika 'Bustani ya Vipaji' huko Milano. Radio ya Vatican pia ilikuwepo kwa mara ya kwanza, ikikusanya maoni ya wageni kadhaa, wakiwemo waandishi wa habari, wasemaji wa radio, waandishi, na watangazaji wa podikasti kutoka mashirika ya kibiashara na ya umma, katika matangazo ya moja kwa moja ya saa manne, masaa mawili asubuhi na masaa mawili alasiri. Dhana ni kwamba akili unde ni chombo, msaada wa kueleweka na kudhibitiwa, na hitaji la kulinda sauti na nyuso liliibuka kwa nguvu. Upekee wa mwanadamu na hatari za matumizi yasiyodhibitiwa ya mifumo hii zilithibitishwa tena.
Upendo wa Vizazi Mbalimbali
Huko Milan,nchini Italia kama kauli mbiu ya tukio hilo ilivyosema, pia kulikuwa na "wapenzi wengi wa radio" kwa siku hiyo wasikilizaji wa rika zote, wakiwemo vijana wengi, ambao walisisitiza jinsi njia hii ya radio inavyopendwa sana hata miongoni mwa wadogo zaidi. Upendo ambao haujui mipaka ya umbali wa kijiografia au ya muda na kwamba, leo hii kama ilivyokuwa zamani, unalishwa na kusikiliza na maswali. Kuanzia na uhusiano huo unaozalishwa "tunapoandaa pamoja," walisimulia Mary Cacciola na Flavia Cercato wa Radio Capital, ambao walihitimisha matangazo ya moja kwa moja ya Radio ya Vatican ya saa nne, ambayo yalifunguliwa na mkurugenzi wa Rai Radio Marco Caputo, ambaye alisisitiza jinsi redio inavyo jukumu la kumweka mtu binafsi, mwanadamu, katikati.
"Radio hujenga madaraja," alisema Elena Carbonari, mwandishi wa habari wa Rai Isoradio, akirudia "uhusiano wa haraka kati ya redio na huduma ya umma." Radio kama "nguzo kamili ya habari," aliongeza Federico Silvestri, Mkurugenzi Mtendaji wa Gruppo 24 Ore. Na mwandishi wa habari Francesco Repice, mchambuzi wa redio wa RAI, anatumia etimolojia kuonyesha uzuri wa njia hii ya mawasiliano: "Maoni ya redio hutuongoza kuzungumza kuhusu miale, ya mwanga kwa wakati.
"Kila mtu anaweza kuchangia kupitia mzaungumzo na kujenga madaraja"
Mwale huo ndio neno." Akizungumza jukwaani katika Siku ya Radio Duniani, Massimiliano Menichetti, Mhusika Mkuu wa Radio Vatican - Vatican News na Naibu mkurugenzi wa uhariri wa vyombo vya habari vya Vatican, alikumbuka kwamba si tu "waandishi wa habari, bali kila msikilizaji, kila mpenda radio anaweza kuchangia kupitia mazungumzo, kukutana, na maneno ili kujenga madaraja, kwa ajili ya ulimwengu wa udugu, mshikamano, ujumuishaji, na amani."
![]()
Mwanzilishi wa tukio, hilo Giorgio D'Ecclesia, akiwa juu ya jukwaa na Massimiliano Menichetti
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here