Tafuta

Bi Sima Bahouse na Bi Amina J. Muhammed wakisalimiana. Bi Sima Bahouse na Bi Amina J. Muhammed wakisalimiana. 

CSW70:Serikali zakubaliana kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wanawake na wasichana

Katika Mkutano huo wa CSW70 ulifunguliwa kuanzia tarehe 9 hadi 19 Machi 2026 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa(UN),ukiwaleta pamoja wawakilishi wa serikali,mashirika ya kiraia na wadau wengine kujadili sera,rasilimali na uwajibikaji ili kuharakisha usawa wa kijinsia duniani.Bi Bahous,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake,UN Women,alikaribisha hatua hiyo kuwa makubaliano yanaonesha dhamira za serikali za kumaliza kutokuchukuliwa hatua kwa hilo

Umoja wa Mataifa(UN)

Wawakilishi wa serikali kutoka nchi mbalimbali duniani wanaoshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni  ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani walipitisha makubaliano muhimu ya kimataifa ya kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wanawake na wasichana wote. Kwa kutambuliwa kama “Agreed Conclusions” yaaniHitimisho Lililokubaliwa,”  nyaraka hiyo ilipitishwa kwa makubaliano mapana wakati wa ufunguzi wa CSW70,  ambao ni mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa unaojikita katika usawa wa kijinsia na haki za wanawake. 

Kujadili sera, rasilimali na uwajibikaji ili kuharakisha usawa wa kijinsia duniani

Mkutano  huo wa  CSW70 ulifunguliwa  kuanzia tarehe 9 hadi 19 Machi 2026 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa(UN),ukileta pamoja wawakilishi wa serikali, mashirika ya kiraia na wadau wengine kujadili sera, rasilimali na uwajibikaji ili kuharakisha usawa wa kijinsia duniani.

Nyaraka inaweka mwongozo wa hatua za kuimarisha mifumo ya sheria

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumanne tarehe 10 Machi 2026  na UN Women,  jijini New York, Marekani, nyaraka inaweka mwongozo wa hatua za kuimarisha mifumo ya sheria na kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata haki kwa usawa duniani.

Nyaraka ni kiashiria cha dhamira za serikali kuwahudumia watu wote kwa usawa”

Bi Sima Bahous,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women, alikaribisha hatua hiyo akisema kuwa makubaliano hayo yanaonesha dhamira za serikali za kumaliza kutokuchukuliwa hatua dhidi ya wahalifu na kujenga mifumo ya haki inayowahudumia watu wote kwa usawa.

Nyuma ya takwimu zote za ukosefu wa usawa kuna maisha halisi ya wanawake na wasichana”

Kwa upande wa Bi Maritza Chan wa Costa Rica,  Mwenyekiti wa CSW70,  alisema kuwa “jukumu kubwa sasa ni kuhakikisha ahadi hizo zinatekelezwa,” akisisitiza kuwa “nyuma ya takwimu zote za ukosefu wa usawa kuna maisha halisi ya wanawake na wasichana wanaosubiri kuona kama viongozi watatekeleza wanachokiahidi.”

Matarajio: Serikali zimehimizwa kuchunguza na kurekebisha sheria zinazobagua wanawake

Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa hadi sasa hakuna nchi iliyofikia usawa kamili wa kisheria kati ya wanawake na wanaume:

Kupitia makubaliano hayo, serikali zimehimizwa kuchunguza na kurekebisha sheria zinazobagua wanawake, ikiwemo zile zinazohusu ndoa za utotoni, sheria za familia na haki za kumiliki mali.

Pia zinatakiwa kuchukua hatua kali zaidi kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, mtandaoni na nje ya mtandao, pamoja na kuhakikisha wahusika wanawajibishwa na manusura wanapata msaada na haki kwa wakati.

Mapendekezo mengine muhimu ni pamoja na kupanua upatikanaji wa msaada wa kisheria, kuimarisha uratibu kati ya taasisi za haki, kutumia teknolojia kwa uwajibikaji katika mifumo ya sheria, na kutambua rasmi wafanyakazi wa haki za jamii na wasaidizi wa kisheria katika mifumo ya kitaifa.

Unaweza kusoma hitimisho:https://www.unwomen.org/sites/default/files/2026-02/csw70-agreed-conclusions-zero-draft-en.pdf

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

11 Machi 2026, 17:19