Tafuta

Kifaru cha jeshi la Pakistani huko Chaman,kwenye mpaka na Afghanistan, katika Wilaya ya Balochistan. Kifaru cha jeshi la Pakistani huko Chaman,kwenye mpaka na Afghanistan, katika Wilaya ya Balochistan.  (AFP or licensors)

Afghanistan-Pakistan:Zaidi ya Wataliban 400 na raia 100 wauawa

Kinachofanya hali kuwa mbaya zaidi ni hali ya kibinadamu nchini Afghanistan,ambayo tayari ni miongoni mwa nchi dhaifu zaidi duniani.Kulingana na Shirika la Mpango na chakula Duniani(WFP,)mtu mmoja kati ya watatu,takriban milioni 17.4,anahitaji msaada wa haraka wa chakula,huku watoto milioni 3.7 walio chini ya umri wa miaka mitano wakiteseka kutokana na utapiamlo mkali.

Na Guglielmo Gallone – Vatican.

Vikosi vya Pakistan vimeripotiwa kuwaua zaidi ya Taliban 400 wa Afghanistan, katika Operesheni Ghazb lil Haq (Ghadhabu ya Haki) dhidi ya Afghanistan, iliyoanza mnamo Februari 27. Hii ilitangazwa na Waziri wa Habari wa Pakistan Attaullah Tarar. Wakati huo huo, idadi ya watu waliofariki kutokana ukosefu wa msaada wa kibinadamu bado ni kubwa. Inasemakana kuwa raia 42 wa Afghanistan waliuawa na 104 kujeruhiwa katika mapigano kati ya Februari 26 na Machi 2. Kulingana na Umoja wa Mataifa, waathiriwa, wakiwemo wanawake na watoto walisababishwa na “mashambulizi ya moja kwa moja” na mashambulizi ya anga yaliyopiga maeneo ya makazi katika majimbo ya Afghanistan ya Paktia, Paktika, Nangarhar, Kunar, na Khost.

Hapo ardhini, hali bado ni tete na ya kuyumba. Mapigano kando ya mpaka yanaendelea, huku Kabul ikidai kuteka kambi ya Pakistan katika eneo la kusini ya Kandahar, ambayo si mbali na mpaka. Mapigano hayo ni sehemu ya ongezeko lililoanza baada ya mabomu ya Pakistan, ambayo Islamabad inadai yalilenga makundi yenye silaha yanayofanya kazi katika mpaka. Hata hivyo, mamlaka ya Taliban yanakataa shutuma hizi na yanazungumzia mashambulizi yasiyo na mpangilio. Milipuko na mapigano yameripotiwa katika majimbo kadhaa ya mashariki, huku mapigano yakiendelea kuwa wazi katika wilaya zaidi ya thelathini.

Suala la kikanda

Ghasia hizo tayari zimesababisha watu wengi kuhama makazi yao. Shirika la Mpango na Chakula Duniani(WFP) linaripoti kwamba takriban familia 20,000 zimelazimika kukimbia makazi yao katika maeneo ya mashariki na kusini mashariki mwa nchi. Mpaka mrefu kati ya Afghanistan na Pakistan, takriban kilomita 2,400, unavuka karibu theluthi moja ya majimbo ya Afghanistan, na  kufanya kuwa magumu sana kuyadhibiti. Kufuatia shambulio la Marekani na Israel dhidi ya Iran, mzozo huo pia ni wasiwasi wa kikanda. Afghanistan na Pakistan zote zinapakana na Iran, na vipengele hivyo viwili linatokea wakati mvutano na harakati za kuwarudisha nyumbani tayari zinaongezeka upande wa magharibi wa nchi. Hatari ni Kusini-magharibi mwa Asia itakuwa kitovu cha mahitaji ya msaada, huku kuingiliana ikichochea mtiririko mpya wa waliokimbia makazi yao na wahamiaji.

Kinachofanya hali kuwa mbaya zaidi ni hali ya kutumika nchini Afghanistan, ambayo tayari ni miongoni mwa dhaifu zaidi duniani. kwa mujibu wa WFP, mtu mmoja kati ya watatu, takriban Waafghanistan million 17.4, anahitaji msaada wa haraka wa chakula, huku watoto million 3.7 walio chini ya umri wa miaka 5 kwa utapiamlo wa kukithiri. Mapigano hayo yamesababisha baadhi ya shughuli za dharura, na kuwaacha takriban watu 160,000 bila chakula. Wakati huo huo, UNICEF imeongeza tahadhari kuhusu watoto na imetuma vifaa vya ziada vya lishe kwa watoto wenye utapiamlo.

Amani pekee zawadi kutoka kwa Mungu

Mfuko wa Pangea pia unaripoti kwamba mabomu hayo yanapiga maeneo ambayo tayari yameharibiwa na tetemeko la ardhi la mwaka jana, ambapo maelfu ya familia walikuwa bado wanaishi katika mahema na kambi za muda. "Wanawapiga mabomu wale ambao tayari wamepoteza kila kitu," shirika hilo lilionya. Hali hii iliyoonyeshwa na vurugu na mgogoro wa kibinadamu pia inazidishwa na kuzorota kwa hali ya haki za binadamu nchini.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani matumizi yanayoongezeka ya adhabu ya viboko ya umma, ambayo wanaona ni kinyume cha sheria ya kimataifa na utu wa binadamu. Katika sala ya Jumapili iliyopita, Papa Leo XIV alizungumzia hali inayoendelea kwa kutoa wito wa amani: "Zaidi ya hayo, katika siku za hivi karibuni, tumepokea habari za kutisha za mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan. Ninatoa ombi langu la kurejea kwa haraka kwa mazungumzo. Tuombe pamoja kwamba maelewano yaweze kutawala katika migogoro yote duniani kote. Amani pekee, zawadi kutoka kwa Mungu, ndiyo inayoweza kuponya majeraha kati ya watu."

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

04 Machi 2026, 14:04