Tafuta

Maisha magumu ya wanawake nchini Msumbiji,yamepelekea kukataa zawadi ya mke wa Rais. Maisha magumu ya wanawake nchini Msumbiji,yamepelekea kukataa zawadi ya mke wa Rais.  (AFP or licensors)

Msumbiji:Wanawake wakataa Makapulana,wadai hatua halisi kutoka kwa Mke wa Rais

Kikundi cha wanawake wa Msumbiji kimeandika barua ya wazi kwa Mke wa Rais,kikipinga mipango ya kusambaza nguo za kiutamaduni(Capulana),katika kuelekea siku ya Wanawake na badala yake kinatoa wito wa marekebisho ya haraka kwa huduma ya afya inayozorota na ukosefu wa usawa.

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Wanawake nchini  Msumbiji wamepaza sauti zao dhidi ya kile wanachokiona kama ishara tupu, huku kukiwa na migogoro mikubwa katika huduma ya afya na maisha ya kila siku. Katika barua ya wazi kwa mke wa Rais Daniel Francisco Chapo, Bi. Gueta Selemane Chapo, Umoja wa wanawake ulionesha hasira yao kuhusu ripoti kwamba nguo za kiutamaduni zenye rangi nyingi zitatolewa nchini kote katika  kuadhimisha Siku ya Wanawake wa Msumbiji mnamo tarehe 7 Aprili ijayo. Kwa mujibu wa Habari kutoka Shirika la Kipapa la habari za kimisionari Fides, ilibainisha kwamba  barua hiyo ilisainiwa na wanawake wakizungumza kwa niaba ya: "mama zetu, binti zetu, dada zetu, na bibi zetu, kuwa suala hilo  halileti maana.  "Hatutaki makapulana, tunahitaji utu na heshima kwa haki za wote," wanaandika huku, wakisisitiza kwamba ishara hizo hazieleweki wakati watu wanateseka.

Hasira kufuatia huduma hafifu za afya

Kiini cha ujumbe wao ni hali mbaya ya hospitali za umma. Watoto wanakufa katika vituo visivyo na vifaa, wanawake wajawazito wanakabiliwa na uchungu wa kujifungua kwenye vitanda vitupu bila magodoro au dawa muhimu, na familia zinakosa huduma za msingi. "Kuna nini cha kusherehekea?" wanawake waliuliza. "Kusherehekea kutokuwepo kwa hospitali nzuri? Kusherehekea upotevu wa rasilimali za umma? Kusherehekea ukosefu wa usawa na vurugu ambazo bado zinaendelea?" Wanatoa picha dhahiri ya mikasa  ya kila siku, wakiwasihi viongozi kukabiliana na hali halisi badala ya kuificha kwa sherehe.

Wito wa kuelekeza fedha ili kuokoa maisha

Kikundi hicho kinadai kwamba pesa za serikali zilizotengwa kwa ajili ya capulana zielekezwe kwa mahitaji halisi. "Hatutaki capulana; tayari tuna za kutosha na hatuhitaji zaidi," walisema waziwazi. Badala yake, fedha zinapaswa kununua dawa, kutoa vitanda vinavyofaa, kuhakikisha upatikanaji wa chakula, na kudumisha heshima kwa wanawake, watoto, na familia. "Mpango huu hautatui matatizo halisi tunayokabiliana nayo," wanaongeza, wakishtumu usambazaji kama matumizi mabaya ya rasilimali wakati maisha yanapokwama.

Ombi la hadhi na haki

Barua hiyo inahitimisha kwa msimamo mkali dhidi ya kutochukua hatua. "Tunadai heshima kwa haki ya utu, afya, na haki ya kijamii," wanawake hao wanatangaza. Wakiwa wamechoka na "ukimya na kutochukua hatua" na "propaganda huku hospitali, shule, na familia zikiteseka," wanatoa wito wa usikivu na suluhisho zinazolingana na hali halisi ya dharura ya Msumbiji.  Ujumbe wao unasisitiza kuchanganyikiwa kunakoongezeka: sherehe ya kweli hutokana na maendeleo, si kitambaa.

 

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

 

24 Februari 2026, 11:04