Ethiopia:Ukame,Uhamiaji na Uwepo wa Utume huko Bale Mashariki
Na Christine Masivo CPS, - Vatican.
Katikati ya mgogoro huo, wamisionari Wakatoliki wanaendelea na kazi yao,wakitoa programu za uhamasishaji dhidi ya mila na desturi hatari za kiutamaduni na kusimama katika mshikamano na walio hatarini zaidi. Katika eneo la kusini mashariki mwa Oromia, hasa huko Bale Mashariki na Laga Hidha nchini Ethiopia idadi ya watu inakabiliwa na dharura kubwa ya kibinadamu. Miaka mingi ya ukame mbaya imesababisha ukosefu wa usalama wa chakula, uhaba mkubwa wa maji, na upotevu wa mazao na mifugo. Familia zimelazimika kuacha nyumba zao kutafuta njia ya kijikimu na kupata chakula.
Mafunzo dhidi ya ukeketeaji wa mwanawake na ndoa za utotoni
"Tuko hasa Bale Mashariki, Laga Hidha, ambapo tunatoa mafunzo dhidi ya ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni." Hii ni sauti ya wamisionari katika huduma nyumba ya kitume ya Robe katika miaka ya uwepo wao nchini Ethiopia, kwenye hali ngumu, vikwazo, na matatizo, ya kutoa huduma kwa ajili ya idadi ya watu katika eneo hilo, ambalo umaskinii umekithiri kwenye eneo hili nchini na lina Waislamu wengi. "Kwa zaidi ya miaka mitatu, kwa makubaliano na Mwakilishi wa Kitume wa huduma ya kimisionari, Padre Angelo Antolini, OFM Cap., alisema “tumekuwa tukifanya kazi katika eneo hili, katika mji ulio umbali wa saa tatu kutoka Robe, mji mkuu wa mkoa wa Mashariki ya Bale, ili kuongeza uelewa wa mila na tamaduni zinazowadhuru wanawake," alisema Padre Emanuele Ciccia.
Hali ya utata
Wamisionari hawa wanaelezea matukio wanayoyaona ya kutatanisha. Katika sehemu yenye ukame, wanawake kadhaa waliohamishwa walianza kujenga makazi ya muda kwa kutumia matawi na makasha ya plastiki. Walikuwa wamekimbia maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame na njaa. Walipoulizwa kwa nini walichagua mahali hapo, majibu yao yalikuwa makali: walitaka kuonekana. "Tulikuja kuiambia serikali kwamba tunakufa. Hatuna maji," walisema. Siku iliyofuata, zaidi ya wanawake na watoto 150 walikuwa wamekusanyika hapo. Wamisionari waliweza kutoa mifuko michache tu ya mchele. Lakini hata kwa uhaba, walipata nafasi ya kuungana na watu. Walicheza na watoto, na kwa muda mfupi, furaha ilirudi na sio kwa vijana tu, bali pia kwa watu wazima waliojiunga.
Utume wa uelewa na uwepo
Kwa zaidi ya miaka mitatu, wamisionari wamefanya kazi katika eneo hilo. Kulingana na Padre Emanuele Ciccia, juhudi zao katika mji ulio umbali wa saa tatu kutoka Robe, mji mkuu wa mkoa wa Mashariki mwa Bale, zinalenga kuongeza uelewa kuhusu desturi za kiutamaduni zinazowadhuru wanawake, hasa ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni.
Licha ya vikwazo na rasilimali chache, wanaona mgogoro unaozidi kuwa mkubwa huko Bale Mashariki
Eneo hilo ni miongoni mwa maskini zaidi nchini Ethiopia na lina Waislamu wengi. Wamisionari sasa wanajiandaa kupanua uwepo wao katika jiji ambalo hakuna Kanisa Katoliki la kuwakaribisha. Hii ni changamoto kubwa wanapoanza awamu hii mpya ya huduma. Licha ya hali hatarishi, vikwazo, na rasilimali chache, wanaona mgogoro unaozidi kuwa mkubwa huko Bale Mashariki kama wito mpya wa kubaki karibu na watu. Dhamira yao si tu ya usaidizi wa kimwili bali pia ya kuwasindikiza, kusimama na jamii ambazo mateso yao mara nyingi hayaonekani
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here