Tafuta

Kiev,:Watu wamekufa kufuatia shambulio huko Lviv. Kiev,:Watu wamekufa kufuatia shambulio huko Lviv.  (ANSA)

Ulimwenguni,matukio ya kila siku:Dunia inahitaji amani!

Ukraine watu kadhaa wanasadikika wamefariki na wengine 19 wamejeruhiwa,kufuatia mashambulizi makubwa ya Urusi dhidi ya Kiev.Serikali mpya ya Venezuela yatangaza kuachiliwa huru kwa wafungwa kadhaa wa kigeni.Maandamano mapya yanaenea Marekani yote kufuatia mauaji ya Renee Good mwenye umri wa miaka 37 na vikosi maalum vya ICE katika kituo cha ukaguzi dhidi ya wahamiaji huko Minneapolis.Januari 9 ni Siku ya kitaifa ya maombolezo ya vijana 40 huko Crans-Montana.

 Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kuanzia kaskazi, kusini, mashariki, magharibi, na Mashariki ya Kati, kila eneo linasikika vurugu na vita, hii inathibitisha kile ambacho Papa Francisko na ambacho kimerudiwa na Mfuasi wake Papa Leo XIV hivi karibuni, kwamba vita vya Dunia vya tatu vilivyogawanyika vipande vipande. Kwa mfano kuanzia Ukraine  taarifa zinabainisha kuwa watu wanne wanasadikika wamefariki, na wengine 19 wamejeruhiwa, kufuatia mashambulizi makubwa ya Urusi dhidi ya Kiev. Meya wa mji mkuu aliripotiwa. Vitali Klitschko, "mhudumu wa afya alifariki na wengine wanne walijeruhiwa wakati wa kutoa msaada kwa watu katika wilaya ya Darnytskyi." Jeshi la Anga baadaye lilieleza kwamba mashambulizi kadhaa yalirekodiwa juu ya jiji la Lviv, ambapo makombora ya masafa marefu yanayosafiri kwa kasi ya juu, takriban kilomita 13,000 kwa saa, yalizuiliwa.

Venezuela: Serikali mpya ya Venezuela yatangaza kuachiliwa huru kwa wafungwa kadhaa wa kigeni. Luigi Gasperin wa Italia, aliyekamatwa Agosti iliyopita kwa kumiliki vilipuzi, na Biagio Pilieri wa Italia-Venezuela wameachiliwa huru. Kuna matumaini kwa Alberto Trentini, mfanyakazi wa misaada aliyekamatwa Novemba 2024 na kwa sasa yuko katika gereza lenye ulinzi mkali nje kidogo ya Caracas. Rais wa Marekani Bwana Trump alitangaza kwamba atakutana na kiongozi wa upinzani wa Venezuela na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Maria Corina Machado huko Washington wiki ijayo.

Marekani - Maandamano mapya yanaenea Marekani yote kufuatia mauaji ya Renee Good mwenye umri wa miaka 37 na vikosi maalum vya ICE wakati wakiwa katika kituo cha ukaguzi dhidi ya wahamiaji huko Minneapolis. Umati mkubwa zaidi uko Minneapolis, ambapo mazingira ni ya wasiwasi sana. Lakini maandamano mbalimbali pia yameonekana New York, Boston, Baltimore, Birmingham, na miji mingine ya Marekani. Wakati huo huo, vyombo vya habari vimetoa jina linalodaiwa la wakala aliyefungua moto.

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kwamba Marekani itaanza mashambulizi ya ardhini dhidi ya magenge ya dawa za kulevya, baada ya kufanya mapigano na meli katika Karibea na Pasifiki katika siku za hivi karibuni."Tutaanzisha mashambulizi ya ardhini dhidi ya magenge hayo. Magenge hayo yanadhibiti Mexico," alisema katika mahojiano na Fox News. Akizungumza na New York Times, tajiri huyo alisema alikuwa tayari kuilinda Kiev, lakini akiwa na jukumu la pili. Rais Trump atakutana na watendaji kutoka makampuni kadhaa makubwa ya mafuta ya Marekani kuhusu uwekezaji katika sekta ya mafuta ya Venezuela. Na wakati huo huo alisaini amri ya utendaji inayoamuru Marekani kujiondoa katika mashirika 66 ya kimataifa, mengi yakiwa yameunganishwa na Umoja wa Mataifa(UN). Hizi ni pamoja na Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, msingi wa mikataba ya kimataifa ya hali ya hewa.

Uswiss. Siku ya kitaifa ya maombolezo kufuatia moto wa mkesha wa Mwaka Mpya huko Crans-Montana, ambao uliwaacha watu 40 wakiwa wamekufa na zaidi ya mia moja kujeruhiwa. Kengele zote za Kanisa la Uswisi zitalia saa 8:00 mchana ili kuendana na haflfa iliyoandaliwa kwa heshima kwa waathiriwa.

Nigeria 

"Watoto walioachiliwa hivi karibuni kutoka shule ya Papiri wamepata kiwewe kipya kufuatia uvamizi wa majambazi wa hivi karibuni uliosababisha vifo vya watu 49." Hii ilitokea kati ya tarehe 28 Desemba 2025 na Januari 3, 2026 ambapo takriban majambazi sitini walifanya bila kuadhibiwa, na kuwaua watu wasiopungua 49 walipokuwa wakizurura kwa uhuru kati ya Eneo la Serikali ya Mtaa ya Borgu katika Jimbo la Niger na sehemu ya kusini ya Eneo la Serikali ya Mtaa ya Shanga katika Jimbo la Kebbi. Hili ndilo Askofu Bulus Dauwa Yohanna wa Kontagora, Jimbo  ambalo tayari imeathiriwa vibaya mnamo Novemba 21 na utekaji nyara wa wanafunzi 265 kutoka shule ya msingi na sekondari ya Katoliki ya Mtakatifu Maria katika Jumuiya ya Papiri, aliripoti kwa Shirika la Kipapa la Habari za Kimsionari Fides.

Ni watoto na vijana walioachiliwa huru katika hatua kadhaa ambao wameathiriwa zaidi na uvamizi mpya wa majambazi ambao, kulingana na Askofu Yohanna, walifanya "bila kupingwa na vikosi vya usalama." "Watoto wa shule ya Papiri ambao waliachiliwa hivi karibuni kutoka kifungoni wameathiriwa zaidi," alisema Askofu wa Kontagora, "kwa sababu kutokana na uvamizi mpya, wamelazimika kujificha msituni na familia zao mchana na usiku." Kulingana na kile ambacho kilisimuliwa kwa Fides na Askofu huyo alisema uvamizi wa kwanza ulianza Desemba 28 wakati "majambazi wenye silaha nzito wakiendesha pikipiki 30, kila mmoja akiwa amebeba watu wawili, walipoacha maficho yao katika msitu wa hifadhi ya Borgu" na kisha kushambulia kijiji cha Kaiwa, ambapo waliwaua watu watano na kupora na kuchoma nyumba na ghala. Kisha komandoo huyo alielekea kijiji cha Gebe, ambapo watu wengine wawili waliuawa.

Uvamizi uliendelea Januari 1, ukipitia kijiji cha Shafaci, ambapo walishambulia kituo cha polisi cha eneo hilo na kuharibu hati zake. Majambazi kisha wakajificha kwenye kichaka kilicho karibu ambapo walilala usiku. Mnamo Januari 2, walishambulia kanisa Katoliki la Sokonbora, wakiharibu msalaba, michoro ya Vituo vya Msalaba, na ala za muziki. Pia walichukua pikipiki mbili, simu kadhaa za mkononi, na pesa taslimu kutoka parokiani.  Wahalifu kisha walikaa katika eneo la makazi katika kijiji cha karibu cha Kambari, ambapo walitumia siku nzima kula kuku na mbuzi wa wakazi. Kutoka hapo, Januari 3, walielekea kijiji cha Kusuwan Daji, kilomita 8 kutoka Sokonbora, ambapo walishambulia soko. Majambazi hao walichoma moto biashara hizo na kuwaua wanaume 42 baada ya kuwafunga mikono yao nyuma ya migongo yao.

"Waathiriwa walikuwa Wakristo na Waislamu," aliripoti Askofu Yohanna, akiongeza kuwa majambazi hao waliteka nyara idadi isiyojulikana ya wanawake na watoto. "Moto uliowashwa na majambazi ulikuwa mkali sana kiasi kwamba ungeweza kuonekana kutoka Papari kilomita 15," anasema Askofu. Katika kutoa rambirambi zake kwa waathiriwa wa shambulio kwenye soko la Kusuwan Daji, Askofu Yohanna aliwasihi wakazi wa eneo hilo wa asili mbalimbali za kikabila (Kamabari, Bussawa, Fulani, na Hausa) "wasiwaone wengine kama maadui, bali waendelee kuwa pamoja katika kukataa vurugu katika aina zake zote na kusimama pamoja katika kukabiliana na ujambazi." Hatimaye, Askofu anatoa wito kwa mamlaka ya Nigeria kuwafikisha wahusika wa "uhalifu huu mbaya" mbele ya sheria na kuhakikisha usalama wa wote.

09 Januari 2026, 09:46