Tafuta

Tanzania,Shule kwa ajili ya wote

Shukrani kwa juhudi za IBO Italia,Shirika moja la kijamii(Focsiv),lilitimiza aina ya ushirikiano jumuishi katika uwanja wa elimu kwa watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu.Kwa zaidi ya miaka saba, mradi huo umehusisha zaidi ya shule 80,lakini suala la rasilimali fedha bado ni tatizo.

Na Vincenzo Giardina – Vatican.

Kwa lugha ya kiitaliano "Naso” ni  pua, na ”ginocchio" ni "goti. Ni lugha ya Kiswahili, kwa kutumia maneno ya viungo vya mwili: ikiwa na sehemu zinazopatikana kwa haraka na kuoneshwa moja baada ya nyingine kwenye kinyago, kuanzia kichwani hadi chini: ili kuelewana, kukua kwa kujiamini na furaha zaidi. Tuko Kipera, nchini Tanzania, katika shule jumuishi ambapo watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu hujifunza kwa pamoja.

Strumenti di apprendimento inclusivi

Zana za kujifunzia jumuishi (© Elena Galeotti)

Elimu inayopatikana kwa Wote

"Leo darasani tunafanya mazoezi ya kutambua sehemu za mwili," alielezea Stanley Mtweve, mmoja wa walimu wanaoshirikiana na Shirika hilo la IBO Italia, Shirika moja la  kijami ambalo ni   Shirikisho la Mashirika ya Kimataifa ya Kujitolea,  yenye Msukumo wa Kikristo(Focsiv). "Kila siku tunafanya shughuli za kujifunza hapa ili kuwasaidia watoto." Kipera iko karibu na jiji la Iringa, kusini mwa Tanzania. Na ni kutoka hapa ndipo picha na video, zilizoshirikishwa na Mtweve na walimu wengine shuleni, zinatokea.

Watoto hugusa kinyago na kisha huweka alama ukutani, wakitumia stika zenye rangi nyingi juu ya michoro ya nyuso za wanafunzi wenzao wakicheka pamoja. Nchini Tanzania, kwa mujibu wa sheria, shule ya msingi ni ya lazima na bure kwa wote; hata hivyo, katika vitendo, watoto wengi wenye ulemavu bado hutengwa kutokana na ukosefu wa mazingira yanayoweza kufikiwa, wafanyakazi maalum, na vifaa vya kufundishia vinavyofaa. "Katika jamii," Mtweve alilalamika, "mara nyingi kuna tatizo la unyanyapaa dhidi ya watoto hawa."

I bambini impegnati con un'insegnante

Watoto wakijifunza wakiwa na mwalimu (© Elena Galeotti).

Ushirikiano kwa ajili ya Elimu

Jibu katika eneo la Iringa limetokana na muungano mpya. kwa hiyo IBO Italia, ikifanya kazi pamoja na Idara ya Elimu ya eneo hilo tangu 2018, imejitolea katika elimu bora: inawafunza wafanyakazi wa shule katika mbinu za mawasiliano na ufundishaji mahsusi kwa watoto wenye ulemavu, ikitoa misaada kwa ushirikiano wa karibu na walimu. Michango ya awali pia imejumuisha fedha za 8xmille kwa ajili ya Kanisa Katoliki. Wafadhili wakuu katika miaka ya hivi karibuni wamejumuisha Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Italia (AICS), Mfuko wa Upendo wa Uswiss kupitia Mfuko wa Angela na Guido Magni na Harambee Onlus.

L'esterno di una scuola in Tanziania

Nje ya shule mojawapi ya Tanzania(© Elena Galeotti)

Zaidi ya Shule 80 zinazohusika

Rasilimali kwa sasa ni suala muhimu. Na kwa kuzingatia matokeo yaliyopatikana, suluhisho zinahitajika haraka iwezekanavyo, Mtweve alisisitiza: "Tangu ushirikiano na shule uanze, kumekuwa na maboresho makubwa kwa watoto; tunafurahi na tunajivunia hili." Kwa upande wa Paola Ghezzi, mwakilishi wa nchi wa Ibo Italia, alielezea "maboresho makubwa" kwa wanafunzi na walimu. "Katika miaka saba," alikadiria, "tumeweza kufikia zaidi ya shule 80 na maelfu ya watoto, kuhakikisha kwamba elimu ni haki ya wote."

Iringa iko kama umbali wa saa kumi kwa gari kutoka Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi  na biashara wa Tanzania kwenye Bahari ya Hindi. Katika eneo hilo, watu wanne kati ya watano wanaishi katika vijiji au maeneo ya vijijini nje ya maeneo ya makazi. Kwa kiasi fulani kutokana na changamoto za mfumo wa huduma ya afya, kiwango cha ulemavu ni cha juu kuliko katika sehemu zingine za nchi, kikikaribia asilimia 8. Hata hivyo, katika shule ya Kipera, watu hujifunza mengi. Kwenye mlango,  kuna maneno  yaliyoandikiwa: "karibuni."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

19 Januari 2026, 14:13