Tafuta

Eneo la Huduma za Raia na Uhamiaji za Marekani,huko New York. Eneo la Huduma za Raia na Uhamiaji za Marekani,huko New York. 

Marekani:Idara ya Usalama wa Nchi yapunguza muda wa kusubiri visa kwa waamini

Idara ya Usalama wa Nchi ya Marekani(DHS)imetangaza mabadiliko makubwa ya kisheria yanayolenga kupunguza usumbufu unaohusiana na Visa kwa watawa wa kike na kiume na Mapadre waliozaliwa nje ya nchi wanaohudumia Jumuiya na jamii nchini kote,Marekani.Kwa upande wa Maaskofu Katoliki nchini Marekani(USCCB walieleza kuridhika,hasa walionesha uungaji mkono mkubwa kwa mabadiliko hayo.

Na Sr. Christine Masivo CPS – Vatican.

Katika kifungu cha sheria ya mwisho ya muda iliyotolewa mnamotarehe 14 Januari 2026, na Idara ya Usalama wa Nchiya Marekani(DHS)iliondoa masharti ya muda mrefu yaliyowalazimisha wahudumu wa  kidini kubaki nje ya Marekani kwa mwaka mzima baada ya kufikia kikomo cha juu cha miaka mitano kwa visa ya Watawa wa kike na kiume na mapadre ya( R-1.) Kwa njia hiyo kifungu cha  sheria mpya, wamiliki wa visa ya (R-1) kama vile Mapadre, Watawa, wachungaji wa madhedhebu mengine, na wakuu wa Kiyahudi, bado watahitajika hata baada ya kuondoka Marekani baada ya kukamilisha kipindi cha miaka mitano kilichowekwa kisheria. Kutokana na sababu hiyo hawatalazimika tena kupewa kipindi cha chini cha lazima cha kuishi nje ya nchi kabla ya kuomba tena visa mpya ya(R-1.)

Maafisa wa Idara ya Usalama wa Nchi ya Marekani(DHS), walisema mabadiliko haya yatapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kusubiri na kuzuia usumbufu usio wa lazima kwa huduma za kidini. Katika taarifa, msemaji wa Maafisa wa Idara ya Usalama wa Nchi ya Marekani(DHS) alisisitiza kujitolea kwa utawala kulinda uhuru wa kidini na kuhakikisha kwamba mashirika ya kidini yanaweza kuendelea kutoa huduma muhimu. "Wachungaji, mapadre, watawa, na wakuu wa Kiyahudi ni muhimu kwa muundo wa kijamii na kimaadili wa nchi hii," msemaji huyo alisema, akiongeza kuwa idara hiyo inaendelea kuzingatia kusaidia mashirika haya ya imani katika kazi yao muhimu.

Maaskofu wa Marekani wanashukuru

Kwa upande wa Maaskofu Katoliki nchini Marekani walieleza kuridhika, hasa walionesha uungaji mkono mkubwa kwa mabadiliko hayo. Askofu Mkuu Paul S. Coakley wa Jiji la Oklahoma, na rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani(USCCB), na Askofu Brendan J. Cahill wa Victoria, Texas, mwenyekiti wa Kamati ya Uhamiaji ya Baraza la Maaskofu Marekani(USCCB,) walitoa taarifa ya pamoja wakikaribisha uamuzi huo. Walielezea hatua hiyo kama "hatua muhimu sana" ambayo itasaidia kupunguza usumbufu kwa huduma muhimu za kidini nchini kote Marekani.

Tangazo hilo linafuatia utetezi endelevu kutoka Mashirika ya Wakatoliki na mengine yanayotegemea imani, yanayohusika na kuongezeka kwa mrundiko wa visa vya EB-4 vinavyotegemea ajira, ambavyo wahudumu wa kidini,  mara nyingi huomba ili kubaki Marekani daima. Kulingana na utafiti wa kitaifa wa 2022, karibu robo  ya Mapadre Wakatoliki wanaohudumu nchini Marekani ni wazawa wa kigeni, ambao wengi wao hutegemea visa ya muda na mpya ili kuendelea na huduma yao ya kichungaji.

Ujumbe maalum wa Kichungaji wa Maaskofu 

Katika mkutano wao wa mwezi Novemba 2025, Maaskofu wa Marekani waliidhinisha “ujumbe maalum wa kichungaji” uliokuwa wa kwanza tangu mwaka 2013, uliopinga agizo la utawala wa Obama kuhusu Uzazi wa Mpango huku wakielezea “wasiwasi wetu hapa kwa wahamiaji.” Ujumbe maalum wa Maaskofu ulipinga “kuhamishwa kwa watu kwa wingi bila ubaguzi” na pia uliomba “kukomeshwa kwa maneno na vurugu zinazodhalilisha utu, ziwe zinaelekezwa kwa wahamiaji au vyombo vya sheria.” Taarifa hiyo, ambayo haikumtaja Trump, ilikuja huku idadi inaongezeka ya Maaskofu wabainisha  kwamba baadhi ya sera za uhamiaji za utawala huo zinahatarisha kuliletea Kanisa changamoto katika vitendo hasa katika kusimamia usaidizi wa kichungaji na juhudi za Upendo, pamoja na changamoto za uhuru wa kidini, kama vile sera ya kupunguza vikwazo vya Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha katika kile kinachoonekana kama maeneo nyeti, ikiwa ni pamoja na nyumba za ibada.

Miguel Naranjo: "Mabadiliko hato ni hatua chanya"

Miguel Naranjo, mkurugenzi wa huduma za uhamiaji wa kidini na Uhamiaji Kisheria wa Kikatoliki (CLINIC), aliita mabadiliko hayo "hatua chanya na ya vitendo," akibainisha kuwa yanashughulikia moja ya vipengele vinavyosumbua zaidi vya mfumo wa visa ya R-1. Hata hivyo, alionya kwamba changamoto bado zipo, kwani wafanyakazi wa kidini bado wanatakiwa kuondoka nchini baada ya miaka mitano na wanakabiliwa na vikwazo vikubwa vya uhamiaji, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya usafiri na mrundikano wa visa. Na Watetezi wa Wakatoliki wanaendelea kuhimiza Bunge kupitisha Sheria ya Ulinzi wa Nguvu Kazi ya Kidini ya pande mbili, ambayo itawaruhusu wafanyakazi wa kidini walio na maombi ya kudumu ya ukaazi kubaki Marekani huku wakisubiri idhini. Wanaonga mkono swala hili walisema kwamba sheria kama hiyo ni muhimu ili kulinda kikamilifu uhuru wa kidini na kuhakikisha mwendelezo wa huduma ya kichungaji.

Huku wakikaribisha uamuzi wa Idara ya Usalama wa Nchi ya Marekani(DHS, viongozi wa Kanisa pia wameelezea wasiwasi kuhusu sera zingine za uhamiaji, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kwa watu wengi na hatua za utekelezaji karibu na nyumba za ibada. Hata hivyo, wengi wanaona sheria mpya kama maendeleo ya kutia moyo. Kama J. Kevin Appleby wa Kituo cha Mafunzo ya Uhamiaji alivyosema, kuwa mabadiliko hayo yatasaidia Maaskofu na viongozi wengine wa madhehebu mengine ya kidini kukidhi mahitaji ya kichungaji ya Jumuiya zao kwa kujiamini na utulivu zaidi.

Kuhusu Visa Marekani

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

16 Januari 2026, 18:00