Tafuta

Mashambulizi ya anga huko Nigeria. Mashambulizi ya anga huko Nigeria.  (AFP or licensors)

Noeli ya umwagaji damu nchini Nigeria:Marekani yafanya mashambulizi ya anga dhidi ya kambi za IS

Vifo vingi katika mashambulizi ya mabomu dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika.Rais wa Marekani Trump aonya:hatua lazima zichukuliwe ili kuwalinda Wakristo.Lakini serikali ya Nigeria,huku ikiunga mkono mashambulizi hayo,inajitenga na utawala wa Marekani:"Hakuna mauaji yanayoendelea.Mambo haya hayaakisi ukweli uliopo."Kardinali Lojudice:"Mashambulizi ya mabomu hayawasaidii Wakristo.Kiukweli,yanaishia kuwaweka hatarini."

Na Federico Piana – Vatican.

Mashambulizi ya anga ya Marekani nchini Nigeria siku ya Noeli Desemba 25, na mapema sana ya Siku ya Noeli  yalizipiga kambi mbili za kijeshi zilizohusishwa na makundi ya kigaidi ya kile kinachoitwa Islamic State (IS), ambazo zilikuwa zimefichwa katika mimea minene ya msitu wa Baunei, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ya Afrika.

Mashambulizi yaliyolengwa

Uthibitisho umetolewa asubuhi Desemba 27 kutoka  serikali ya Nigeria, saa chache tu baada ya mabomu yaliyowalenga wapiganaji wa kigeni kutoka eneo la Sahel. "Katika kambi hizo, maandalizi yalifanywa kupanga mashambulizi makubwa ya kigaidi katika eneo letu la kitaifa," Wizara ya Habari ilisema katika taarifa iliyotolewa 26 Desemba jioni.

Maamuzi ya pamoja

Uingiliaji kati wa serikali ya Nigeria kuelezea matukio hayo pia unalenga kufafanua kwamba mashambulizi hayo hayakuwa uamuzi wa upande mmoja na utawala wa Marekani bali yalipokea idhini ya moja kwa moja ya Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu. Pia inaripotiwa alikubali kuzindua mashambulizi hayo kutoka kwa majukwaa ya baharini yaliyoko katika Ghuba ya Guinea. Operesheni hiyo, Wizara ya Habari ya Nigeria pia ilijifunza, ilitumia makombora 16 ya usahihi yaliyozinduliwa na ndege zisizo na rubani zinazodhibitiwa kwa mbali.

Majeruhi wengi

Vyanzo vya Pentagon vinaonesha kiwango cha vifo cha shambulio la anga, ikisisitiza kwamba kulikuwa na vifo vingi, ingawa idadi kamili ya waathiriwa bado haijafunuliwa. "Hapo awali niliwaonya magaidi hawa kwamba ikiwa hawatazuia mauaji ya Wakristo, kuzimu kungetokea. Na usiku wa leo ilitokea," Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye Twitter kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth,  dakika chache tu baada ya mashambulizi hayo kuanza.

Kujitenga mbali

Lakini serikali ya Nigeria yenyewe imejitenga na msimamo wa Marekani kwamba mauaji ya Wakristo yanaendelea nchini Nigeria, hadi kufikia hatua ya kuiainisha kama "taifa la wasiwasi," kundi lililotengwa kwa ajili ya nchi zinazopitia ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa kidini: "Sio hivyo. Mambo haya hayaakisi ukweli halisi." Kardinali Augusto Paolo Lojudice, Askofu Mkuu wa Siena-Colle di Val d'Elsa-Montalcino na Askofu wa Montepulciano-Chiusi-Pienza, katika mahojiano na gazeti la Italia, alibainisha kuwa  mashambulizi ya Marekani hayana maana katika kuwalinda Wakristo: "Mabomu hayawasaidii bali yanaishia kuwaweka hatarini. Vurugu huzaa vurugu zaidi. Lazima tujiepushe na vita."

Hali Ngumu

Tukiangalia data rasmi, hali inaonekana kuwa ngumu zaidi na yenye utata kuliko ile ambayo utawala wa Marekani unafikiria kwa sasa. Mashambulizi na vurugu, zilizofanywa tangu 2009 na kundi la kijihadi la Boko Haram na baadaye, tangu 2016, na kundi lililojitenga linalojulikana kama Serikali ya  Kiislamu ya Mkoa wa Afrika Magharibi (ISWAP), hadi sasa zimesababisha vifo vya watu wasiopungua 35,000, wengi wao wakiwa Waislamu, na kuhama makazi yao zaidi ya milioni 2.5. Hapa pia, Waislamu wanakadiriwa kuwa wengi. Zaidi ya hayo, kuna magenge ya wahalifu ambao, kwa sababu za kifedha, hupora, huteka nyara, na kuua bila kubagua.

Mwanzo Tu

Mashambulizi ya Marekani, ambayo yalianza kwa mfano usiku wa Noeli, kulingana na baadhi ya wachambuzi wa ndani, yanawakilisha mwanzo tu wa kampeni inayolenga kulenga makundi ya Kiislamu yenye msimamo mkali Nigeria yote. Mapigano haya pia yanaongeza mauzo ya silaha: leo desemba 27, Rais Timubu wa Nigeria  alitangaza ununuzi wa helikopta nne za mashambulizi. Ile itakayoziuza kwa moja ya mataifa maskini zaidi duniani itakuwa Marekani.

27 Desemba 2025, 15:24