Viongozi wa EU na Zelensky mjini Brussels kuendeleza mpango wa ulinzi wa Ulaya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Afisa mkuu wa Umoja wa Ulaya alisema saa chache kabla ya mkutano kuanza ambao pia uliudhuriwa na Rais wa Ukraine Zelensky: “ Katika Baraza la Ulaya la leo tarehe 6 Machi 2025 suala la muungano wa walio tayari kutoa dhamana ya usalama wa Kyiv litashughulikiwa, na jukumu la kifedha na kisiasa la Umoja wa Ula ( EU) pia litajadiliwa, ikiwa suluhisho na misheni na askari walioko chini itafikiwa.”
Mpango wa euro bilioni 800
Rasimu ya hivi karibuni ya hitimisho inasema kwamba dhamana ya usalama inapaswa kufanywa kwa kushauriana na Ukraine na NATO. Kulingana na CNN, Uingereza, Ufaransa na Türkiye zitatoa idadi kubwa ya vikosi vya kulinda amani. Siku ya Jumanne, Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen alitangaza mpango wa Euro bilioni 800 wa kurejesha tena Ulaya na kuongeza matumizi ya kijeshi ya nchi wanachama.
Kupanua mwavuli wa kijeshi wa Ufaransa
Wakati huo huo, pendekezo lililozinduliwa jana jioni tarehe 5 Machi 2025 na Rais wa Ufaransa Macron, wakati wa hotuba kwa taifa, kurefusha uzuiaji wa nyuklia wa Ufaransa kwa nchi zingine za Ulaya, linazua utata. Kiongozi huyo kisha alizungumza juu ya uwepo wa "mpango thabiti na wa kudumu wa amani, ambao tumetayarisha na Waukraine na washirika wengine kadhaa wa Ulaya.Wakati huo huo, Trump pia amesitisha ubadilishanaji wa habari za kijasusi na Kyiv, lakini mazungumzo na Zelensky yameanza tena. Rais wa Ukraine alisema kuwa kazi inaendelea ya kupanga mkutano mpya kati ya viongozi wa Marekani na Ukraine. Zelensky pia aliandika kwenye Telegram kwamba "hakuwezi kuwa na utulivu katika shinikizo kwa Urusi kukomesha vita hivi na ugaidi huu dhidi ya maisha," akirejea shambulio la kombora lililotokea jana usiku kwenye hoteli huko Kryvyi Rih, mji alikozaliwa, na kusababisha vifo vya watu wanne na angalau 30 kujeruhiwa.