Israel yasitisha Msaada kwa Gaza hadi Hamas ikubali mpango
Na Angela Rwezaula – Vatican.
Ni Uamuzi, wa Israeli wa kusimamisha uingiaji wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza ambapo Israel itajiondoa ikiwa Hamas haitakubali kile kinachoitwa "mpango wa Witkoff", ulioandaliwa na mjumbe wa Marekani katika Mashariki ya Kati, ambao unatoa muda wa kurefushwa kwa awamu ya kwanza ya makubaliano ya mapatano katika Gaza ya takriban siku 50, ikijumuisha kipindi chote cha Ramadhani - mwezi mtukufu kwa Kiislamu ulioanza Machi 1 - na Pasaka ya Kiyahudi. Wakati wa awamu hii, kundi la Kiislamu linatarajiwa kuwaachilia mateka ambao bado wako hai, karibu 24 na kukabidhi miili ya marehemu.
Nafasi za kimataifa
Lawama hizo zilikuwa kali kutoka katika nchi za Kiarabu, ikiwa ni pamoja na Misri - mmoja wa wapatanishi wakuu wa usitishaji mapigano - na pia kutoka Umoja wa Mataifa, ambao kupitia msemaji wake Tom Fletcher aliuita uamuzi wa Israeli "wa kutisha," ukizingatia kwamba sheria ya kimataifa ya kibinadamu inaweka wazi kwamba ufikiaji wa misaada lazima uruhusiwe. Kusitishwa kwa msaada huo, kunaungwa mkono na urais wa Marekani wa Trump, ambaye, kupitia kwa msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa Ikulu (White House,) Brian Hughes, alisema kuwa "Israel imejadiliana kwa nia njema tangu mwanzo wa utawala huu ili kupata kuachiliwa kwa mateka". Katika shutuma za Hamas kwamba Israel inawasababishia njaa wakazi wa Gaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Sa'ar alisema kwamba wakati wa mapatano ya majuma sita, vifaa vya kutosha kwa takriban miezi minne viliingia Ukanda huo.