Padre Mattia Ferrari:Nchini Libya,hali ya kinyama kwa wahamiaji wanaopita
Na Beatrice Guarrera na Angella Rwezaula – Vatican.
Wanaume na wanawake waliopatikana katika siku za hivi karibuni katika makaburi mawili ya halaiki nchini Libya bado walikuwa wakipiga mayowe chini ya vumbi. Sio tena kwa sauti zao, lakini kwa miili yao isiyo na uhai tena, iliyoteswa, ikionesha majeraha ya risasi. Miili 19 iligunduliwa huko Jakharrah, kama kilomita 400 kusini mwa Benghazi na mingine 30 (lakini inaweza kuwa zaidi hadi 70) ilipatikana katika jangwa la al-Kufra kusini-mashariki mwa nchi. Hayo yaliripotiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), ambalo lilionesha mshtuko na wasiwasi katika ugunduzi wa makaburi mawili ya pamoja nchini Libya. Sio mara ya kwanza kwa miili ya wahamiaji kuibuka tena nchini humo, kwa watu ambao watabaki bila majina, bila mama au mtoto anayeweza kuomboleza kwa ajili yao kwa heshima. Ni wanaume na wanawake ambao huenda waliangukia katika mikono ya wafanya biashara haramu ya binadamu na huku wakitafuta maisha bora baada ya kulazimika kukimbia umaskini na dhuluma.
Kukataliwa kwa utaratibu
Kugunduliwa kwa makaburi ya halaiki ni uthibitisho mwingine wa hali ya kinyama nchini Libya, kwa hasara ya kaka na dada wengi wahamiaj, alisema Padre Mattia Ferrari, wa Shirika moja lisilo la Kiserikali (NGO), la kutoa huduma ya kusaidia Binadamu katika bahari ya Mediterranea akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican kwamba: "Nchini Libya kuna kile ambacho Papa anakiita: "kambi za mateso" na kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita cha: "kutisha" kinachofanyika na hii ni historia nyingine ya ukatili usiokubalika kabisa, ambao unaumiza dhamiri zetu za kibinadamu na za Kikristo.” Libya, kiukweli, Padre huyo alikumbushaa kuwa “siyo nchi ya kupitia tu lakini pia ni nchi ambayo wahamiaji wanalazimishwa kupitia, kwa sababu ya kufungwa kwa njia za kisheria za ufikiaji na ambamo wanarudishwa, kwa sababu ya kukatalia kwa utaratibu kwamba Italia na Umoja wa Ulaya zinawafadhili.
Ukiukwaji mwingi wa haki za binadamu
Hadi sasa, idadi ya watu wanaoweza kuingia katika eneo la Ulaya kupitia njia za kawaida ni ndogo sana. Tangu Desemba 2023, baada ya kusainiwa kwa itifaki kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Italia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, UNHCR, Arci na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, watu 592 wamewasili nchini Italia. Wa hivi karibuni waliwasili, Jumanne tarehe 11 Februari 2025, kwa ndege kutoka Tripoli. Kuna wakimbizi 139, wakiwemo watoto 69, baadhi yao walizaliwa nchini Libya, ambako wameishi kwa muda mrefu na familia zao katika mazingira magumu mno. Zaidi ya hayo, kwa miaka mingi sasa, mashirika kadhaa ya kimataifa yamekuwa yakiripoti ukiukwaji mwingi wa haki za binadamu unaofanywia wahamiaji nchini Libya: kazi za kulazimishwa, utekaji nyara, unyang'anyi, kulazimishwa kuajiriwa katika makundi ya wanamgambo, hadi kuvuka kwa hatari ya Mediterania, kujaribu kupitia kwenye boti za muda na zisizo salama. Na kinachowangoja wale wanaokataliwa na kurudishwa Libya kinatisha vile vile: vizuizini ambako mateso, ubakaji, ukosefu wa chakula na huduma ya matibabu, kufungwa katika gereza zenye msongamano mkubwa na katika hali ya usafi wa kuogofya ni mambo ya kila siku.
Matumaini yalipungua
Padre Mattia Ferrari anayajua maisha ya wahamiaji hao vyema, ambao anakutana nao baada ya kuepukana na kifo anapofanya kazi kwenye Meri ya Bahari ya Jonio, ambayo ni meli ya uokoaji katika Bahari ya Mediterranea inayohudumiwa na Shirika hilo, lisilo la Kiserikali. Hata kwenye ardhi, Padre Mattia anaendelea kujitolea kwake kwa waathirika, kama vile wale kutoka shirika la Wakimbizi nchini Libya. "Watu hawa wanaripoti unyanyasaji wa ajabu na mateso zaidi ya mipaka yote, zaidi ya mawazo yote. Kila mtu hubeba ndani yake historia, nyuso, matumaini, ambayo yanasalitiwa na mfumo huu wa vurugu isiyoelezeka ambayo hutokea kwa ushirikiano wetu au wakati mwingine hata kwa ushirikiano wa kutojali kwetu."
Haja ya upatanisho
Kiukweli, sauti zinazotolewa na ulimwengu wa kisiasa kuchukua hatua ambazo zinaweza kubadilisha hali ambazo bado zinaonekana kuwa dhaifu. Kesi kwa mfano ya jenerali wa Libya, Nijeem Osama Almasri, anayeshtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, mahakama hiyo hiyo ilithibitisha Jumatatu tarehe 10 Februari 2025, kwamba ilikuwa imefungua faili juu ya "Italia ya kutofuata ombi la ushirikiano kwa kukamatwa na kujisalimisha kwa jenerali wa Libya, ambaye alisimamishwa katika ardhi ya Italia, lakini akarudishwa nyumbani Januari 21, 2025. "Kilichofanyika kimezidisha jeraha kubwa na kwa hivyo kuna haja ya upatanisho, yaani upatanisho na wahamiaji na wale ambao ni waathiriwa wa Almasri,” alisema Padre Mattia. Kwa hiyo mwaliko wa Padre ni kuacha tuhojiwe na uchungu wote huu na kisha: “tufungue mioyo yetu, kwa sababu watu hawa wanainua kwetu kile ambacho ni kilio cha udugu na wanatuomba tutambuliwe katika hadhi yao kama kaka na dada.” Na Bado kuna matumaini, kwa kweli, kugeuza mwelekeo kwamba: "Ikiwa tutashikamana mikono na mashirika ya kiraia, na wahamiaji wenyewe, basi tunaweza kujenga ulimwengu mpya, mfumo mwingine wa hatimaye kutoa mwili kwa udugu.” Kwa sababu ya kile kinachotokea huko Libya na Tunisia na sehemu nyingi za ulimwengu, udugu wa kibinadamu unaharibiwa, na ikiwa hatutaujenga tena, hatutakuwa na njia mbadala dhidi ya unyama, kwa maendeleo ya vita, vurugu na janga la mazingira. Hakuna njia mbadala, isipokuwa kujitambua tena kuwa kama kaka na dada."
Mfumo wa Mtandao wa kihalifu wa Mafia wa Libya
Bidii ya Padre huyo katika kuishi kwa uthabiti kile anachohubiri imempelekea kupokea vitisho na hata kuwekwa chini ya ulinzi, zaidi ya yote, kwa kushutumu mfumo wa kihalifu wa mafia wa Libya, ambapo wakuu wa mtandao wa kihalifu wa mafia wa Libya wanafaidika na biashara haramu ya binadamu, kutokana na kukataliwa kwa wahamiaji, kama Umoja wa Mataifa pia umelaani.” Padre huyo aliomba taasisi, siasa na jamii kuwashika wahamiaji kwa mkono wa ukaribu, kuwasikiliza, kukutana nao na kisha kutembea pamoja nao pamoja na kila mtu. Yeye anatoa huduma ambayo anaifanya kwa shauku kama mwanadamu na kama kuhani, akisindikizana na wanaharakati wengi, watu mara nyingi tofauti naye: “Ndani yao naona upendo wa Yesu, shauku ya Yesu.” Na kwa njia hiyo wengine hawamwamini, wengine hawamwamini, lakini kwa wote ni Msamaria wa mfano huo, ambaye anaishi upendo huo wa macho unaoonesha moyo wa Yesu.