Mazungumzo ya Marekani na Urusi yaanza mjini Riyadh.Kiev haitambui meza
Vatican News
Wajumbe wa Marekani na Urusi wamekuwa katika mji mkuu wa Saudia Arabia tangu Jumatatu jioni tarehe 17 Februari 2025 ambapo wanafanya Mkutano Jumanne tarehe 18 Februari. Waziri Lavrov anaongoza ujumbe wa Moscow, ambao pia unajumuisha Yuri Ushakov na oligarch Kirill Dmitriev washauri wa kidiplomasia wa Kremlin(Urusi). Wawakilishi wa utawala wa Marekani ni Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, Mshauri wa Usalama wa Taifa Mike Waltz na Mjumbe wa Mashariki ya Kati Steve Witkoff.
Lavrov: Hapana kuwa na makubaliano ya eneo kwa Ukraine
Maneno yaliyotolewa na Rubio usiku wa kuamkia Jumanne 18 Februari 2025 yanaonekana kutaka kuwahakikishia washirika wa Ulaya na Kyiv: "Mkutano sio meza ya mazungumzo ya kuamua amani ya Ukraine, lakini ni mwanzo tu wa kutoa ubaridi kati ya nchi hizo mbili, anasisitiza Katibu wa Nchi kuwa, Ulaya hakika itahusika katika mazungumzo." Maneno ya Lavrov yalikuwa ya asili tofauti kabla ya kuwasili Riyadh, alisema kwamba hakuna makubaliano ya eneo yangefanywa kwa Ukraine na kwamba hakukuwa na nafasi mezani kwa "wa Ulaya wanaotaka kurefusha vita." Wakati huo huo Rais wa Ukraine Zelensky kwa upande wake alimsuta Trump akisema anataka kumfurahisha Putin. "Kwa sasa, meza hii haipo kwa ajili yetu," aliongeza Mychailo Podolyak, mshauri wa kwanza wa rais wa Ukraine.
Ulaya iligawanyika
Viongozi wa Ulaya waliokutana mjini Paris tarehe 17 Februari 2025, walisalia kuwa na mgawanyiko kuhusu iwapo watatuma wanajeshi wa kulinda amani nchini Ukraine. Ufaransa, Italia, Ujerumani, Hispania, Uingereza, Denmark, Poland na Uholanzi zilijikuta kwenye safu tu ya jumla ya msaada kwa Kiev. Baada ya mkutano huo katika mji mkuu wa Ufaransa, Rais Macron alifanya mazungumzo ya simu na Trump na Zelensky, ambapo mwisho wake aliandika ujumbe katika X kwamba amani ya kudumu lazima Urusi ikomeshe uchokozi wake na hii lazima iambatane na dhamana kali na za kuaminika za usalama kwa Waukraine: “Tutashughulikia hili na wa Ulaya wote, Wamarekani na Waukraine."