M23 inaendelea kusonga mbele na hatari ya kuingia Uvira
Na Angella Rwezaula – Vatican.
M23 inaendelea kusonga mbele katika Kivu Kusini baada ya kutekwa kwa Bukavu, mji mkuu wa Wilaya hiyo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwa ushindi wa hivi karibuni wa miji ya Kamanyola na Luvungi, wanamgambo wa M23 sasa wana njia wazi kuchukua Uvira, jiji la pili katika Kivu Kusini. Uvira inatazamana na Ziwa Tanganyika, ambapo barabara inaelekea Bujumbura, mji mkuu wa Burundi. Kujiondoa kwa wanajeshi wa Burundi siku chache baada ya kuanguka kwa mji wa Bukavu kungepelekea kusonga mbele kwa waasi kuelekea Uvira, ambapo hali ya wasiwasi inaongezeka; Mamlaka za serikali hata ziliamua kuwaachilia wafungwa kabla ya waasi kuwasili.
Mapigano tarehe 17 Februari 2025
Katika jiji hilo, takriban watu 12 waliuawa mnamo tarehe 17 Februari 2025 katika mapigano kati ya wanajeshi wa kawaida wa jeshi (FARDC) na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Wazalendo. Kwa mujibu wa Radio Okapi, ikimnukuu rais wa Jumuiya ya Kiraia ya Wazalendo wa Congo, Serge Kigwati, mapigano yalianza wakati Wazalendo walipojaribu kuwapokonya silaha wanajeshi waliokuwa wakirejea kutoka upande wa kaskazini kuelekea kusini mwa wilaya hiyo. Kukataa kwa FARDC kukabidhi silaha zao kulisababisha mapigano ya moto kati ya pande hizo mbili. Wakati huo huo, vikosi maalum vya Uganda viliingia Bunia, mji mkuu wa mkoa wa karibu wa Ituri.
Mgogoro wa kikanda sasa unaikumba DRC
Wanajeshi wa Uganda wamekuwepo kwa muda mrefu katika eneo hilo kufanya, pamoja na FARDC, operesheni ya pamoja iitwayo Shujaa dhidi ya wanajihadi wa ADF/NALU wanaoshirikiana na Serikali ya Kiislamu.Kuimarika kwa jeshi la Uganda huko Ituri, kunatukumbusha hatua za pamoja za jeshi la Rwanda na Uganda wakati wa vita viwili vya awali, vile vya 1996-97 dhidi ya Zaire ya wakati huo ya Mobutu na ile ya 1998 dhidi ya Rais wa wakati huo Laurent-Désiré Kabila. Mgogoro wa migogoro ya kikanda kwa mara nyingine tena unaikumba DRC.