Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Allegro vivace
Ratiba Podcast
Wenyeji  wakitazama uharibifu kutokana na mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Congo huko Goma ambapo hawana mahali pa kukaa. Wenyeji wakitazama uharibifu kutokana na mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Congo huko Goma ambapo hawana mahali pa kukaa.  (Arlette BASHIZI for Reuters)

Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa upatanisho kuhusu mzozo DRC!

Mashariki mwa DRC,ni eneo tajiri kwa madini na rasilimali nyingine za asili na limekuwa na vita kwa miongo mingi.Inaripotiwa kuwa zaidi ya makundi 100 yenye silaha yanafanya shughuli zao katika eneo hilo.Ni katika muktadha huo wa ghasi zinazoendelea ambapo Katibu Mkuu wa UN ametoa wito wa kumaliza mzozo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Bwana António Guterres tarehe 6 Februari 2025 katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York, Marekani alitoa ombi  maalum kuhusu  amani kabla ya mikutano miwili muhimu ya kushughulikia mashambulizi makali ya kundi la waasi la M23 lililosaidiwa na Rwanda katika kanda hiyo.   Katibu Mkuu alisema kuwa: “Tupo katika wakati muhimu na ni wakati wa kushirikiana kwa ajili ya amani.” Akiwa katika Baraza Kuu linalofuatia mgogoro huo alisema: “tunahitaji jukumu lenye ushirikiano na la kujenga kutoka kwa wadau wote hasa nchi zinazozunguka eneo hilo, mashirika ya kikanda, Muungano  wa Afrika na Umoja wa Mataifa.”

Ikumbukwe  Mashariki mwa DRC ni eneo tajiri sana kwa madini na rasilimali nyingine za asili na limekuwa na vita kwa miongo kadhaa. Inaripotiwa kuwa zaidi ya makundi 100 yenye silaha yanafanya shughuli zao katika eneo hilo. Mapigano kati ya M23 na vikosi vya serikali ya Congo yalikithiri mwezi Januari 2025  ambapo waasi waliteka mji mkuu wa kanda, huko Goma, kabla ya kuelekea kusini kwenye mji muhimu wa Bukavu, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini. Maelfu ya watu wameuawa, wakiwemo wanawake na watoto na mamia ya maelfu ya wengine wamefukuzwa  kutoka majumbani mwao.  Bwana Gutteres alisema: “Tunaona pia tishio endelevu kutoka kwa makundi mengine yenye silaha, ama ya Congo au ya kigeni. Hii yote ina athari kubwa kwa binadamu.” Katibu Mkuu wa UN aidha alieleza kuhusu ripoti zisizo na mwisho za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwemo ukatili wa kijinsia na kingono, kushurutishwa kujiunga vitani na vikundi vyenye silaha, na kuvurugika kwa misaada ya kuokoa maisha. Alisisitiza kuwa hali ya kibinadamu ndani na katika viunga vya Goma ni ya hatari. Mamia ya maelfu ya watu sasa wako katika harakati, na maeneo mengi ya awali yaliyokuwa na wakimbizi kaskazini mwa mji sasa yamevamiwa, kuharibiwa au kutelekezwa.

Zaidi ya hayo, Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) alisema vituo vya huduma za afya vimefurika, na huduma zingine za msingi ikiwa ni pamoja na shule, maji, umeme, mawasiliano ya simu na intaneti zimepunguzwa kwa kiwango kikubwa. “Wakati huo, vita vinaendelea kushamiri katika jimbo la Kivu Kusini na vitahatarisha janga kubwa zaidi.” Katibu Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaenzi watu wote waliopoteza maisha yao, ikiwa ni pamoja na walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO na vikosi vya kikanda. Alionesha pia mshikamano na watu wa Congo ambao wanajikuta tena kuwa waathirika wa mzunguko wa vurugu unaoonekana kuwa hauna mwisho.”

Tarehe 7 Februari 2025 viongozi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC walitarajiwa kuhudhuria mkutano wa viongozi huko Dar es Saaam Tanzania ili kushughulikia mzozo huu. Kwa njia hiyo Bwana Guterres alisema hali hii pia itakuwa kitovu cha mkutano wa ngazi ya Viongozi wa Baraza la Amani na Usalama la Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa juma lijalo, ambapo atahudhuria pia: “Kadri mkutano huko Tanzania utakavyoanza, na kadri ninavyojiandaa kuondoka kwenda Addis Ababa, ujumbe wangu ni wazi,”. Kwa kuongezea alisema: Nyamazisheni mtutu wa bunduki, zuieni kuendelea kwa machafuko. Heshimuni uhuru na utu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Tekelezeni sheria za haki za binadamu za kimataifa na sheria za kibinadamu za kimataifa.” Kiongozi wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo huu Ni wakati wa kuhakikisha amani. Kiongozi huyo alisema kuwa ni wakati kwa wote waliotia saini mkataba wa amani, usalama na ushirikiano kwa ajili ya DRC na kanda kutekeleza ahadi zao. Hati ya mwaka 2013, iliyotiwa saini na nchi 11, ilikuwa na lengo la kumaliza mzunguko wa vita na vurugu inayojirudia katika eneo la mashariki mwa DRC. BKatibu Mkuu wa UN  alisisitiza kuwa: “Ni wakati wa upatanisho. Ni wakati wa kumaliza mzozo huu. Ni wakati wa amani. Jukumu kwa hiyo  ni kubwa mno.”

07 Februari 2025, 16:15
Prev
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930   
Next
May 2025
SuMoTuWeThFrSa
    123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031