Israel yajiondoa kwenye Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa
Na Angella Rwezaula - vatican
Israel itafuata mfano wa Marekani na kujiondoa katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa. Uamuzi huo uliotangazwa kupitia mitandao ya kijamii na Waziri wa Mambo ya Nje Gideon Saar haukukosi utata: "Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kiutamaduni limewalinda wanaokiuka haki za binadamu huku likitilia shaka demokrasia pekee ya Mashariki ya Kati: Israel," alisema Saar.
Ufafanuzi kuhusu mpango wa Trump kwa Gaza
Wakati huo huo, upinzani wa kimataifa unazidi kukua kwa mpango wa Rais Trump kwa mustakabali wa Ukanda wa Gaza. Ndani ya masaa 24 baada ya tangazo hilo, mkuu wa Ikulu ya Marekani alitoa ufafanuzi: kwanza kabisa, kwamba hakuwa na ahadi yoyote ya kutuma wanajeshi wa Kiamerika huko Gaza na akataja kwamba uhamisho wa Wapalestina kwenda nchi zingine utakuwa wa muda mfupi ili kutekeleza urejeshaji wa eneo hilo.
Ulimwenguni wachachamaa na tamko la Trump
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran naye pia alilaani pendekezo la Mkuu wa Ikulu ya White House, na kulitaja pendekezo la kuwaondoa kwa nguvu Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza "ni la kushtua." Kwa upande wa Jordan na Misri, nchini ambazo ni tajiri alizitaja kuwa ndizo zinazofaa zaidi kuwakaribisha Wapalestina katika Ukanda huo, tayari zilikuwa zimekataa kwa nguvu dhana yoyote katika mwelekeo huu. Urusi, China na Ulaya pia hazikukubaliana, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres akikumbuka kwamba "harakati zozote za kulazimishwa za watu ni sawa na mauaji ya kikabila". Maoni yote ambayo ni pamoja na yale ya pande zinazohusika: rais wa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina, Mahmoud Abbas, alikuwa amepinga kukataa kwa wazi, akisisitiza kwamba "haki halali za Wapalestina haziwezi kujadiliwa" wakati Hamas ilizungumza hata "msimamo wa kibaguzi".