Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
PROGRAMU YA KISWAHILI
Ratiba Podcast
Bi Mia Amor Mottley, Waziri Mkuu wa Barbados alihutubia  Baraza la Umoja wa Afrika huko Addis Ababa , Ethiopia. Bi Mia Amor Mottley, Waziri Mkuu wa Barbados alihutubia Baraza la Umoja wa Afrika huko Addis Ababa , Ethiopia. 

Hotuba ya Bi Mia Amor Mottley kwa AU:Umuhimu wa kuungana kati ya AU na Caribbean!

Waziri Mkuu wa Barbados alitoa wito wa nguvu wa kuwa na uhusiano wa karibu kati ya Afrika na Visiwa vya Caribbean katika Mkutano wa XXXVIII wa Umoja wa Afrika.Aliwataka viongozi kuweka kipaumbele katika hatua zinazoonekana kuunda madaraja ya anga na bahari kuunganisha kanda hizo mbili.Suala la Akili Mnemba Afrika na utajiri wa madini.Kama Mwenyekiti wa V20,muungano wa nchi 70 zinazoathiriwa na tabianchi,40% miongoni ni kutoka bara la Afrika!

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika  Mkutano wa XXXVIII  wa Umoja wa Afrika(AU) uliofanyika huko Addis Ababa, Nchi  Ethiopita tarehe 15 Februari 2025, Waziri Mkuu wa Barbados, Bi Mia Amor Mottley alitoa hotuba ya nguvu katika Mkutano huo hasa kwa kusisitizia uhusiano wa karibu kati ya Afrika na Visiwa vya Carribean, kwa namna nyingine kwa utambuzi kuwa wote ni ndugu kutokana na watu wa Afrika waliopelekwa katika visiwa hivyo kama watumwa. Aliwataka viongozi kuvuka matamshi na kuweka kipaumbele kwa hatua zinazoonekana hasa kuunda madaraja ya anga na bahari kuunganisha kanda hizo mbili. Maswali yaliyochangamotishwa: Je, bara ambalo lina 40% ya madini yote duniani linawezaje kuwa mstari wa mbele katika kupata utulivu wa sayari hii? Je, ni kwa jinsi gani eneo linalowakilisha theluthi moja ya mataifa ya ulimwengu lisifanye kazi kwa madhumuni ya umoja kufafanua upya utawala wa kimataifa? Hata hivyo hapa unaweza kusoma kwa kirefu hotuba kamili ya Waziri Mkuu wa Barbados Bi Mia Amor Mottley:

Barbados, Bi Mia Amor Mottley, Waziri Mkuu wa Barbados

Waheshimiwa, ninaomba nianze kwa kumtambua Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais wa Angola; Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia na mwenyeji wetu, Dk. Amin Abed; Mheshimiwa Mwenyekiti, anayemaliza muda wake wa Umoja wa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania; Wakuu; Waheshimiwa, Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika na Marais wa Kwanza mliopo; Mheshimiwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina; Mheshimiwa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa; Mheshimiwa, Moussa Fakih Mohamed, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika; Waheshimiwa,wajumbe mashuhuri, mabalozi na wageni wote. Ninasimama hapa nikiwa nimevikwa roho ya vita vya Adwa, nikitambua kwamba ni vita hivyo, vilivyopiganwa ndani ya saa 24, vilivyotikisa imani ya mamlaka ya Ulaya lakini viliwatia moyo watu wa Afrika na watoto wa ughaibuni wa Afrika. Ilitufundisha kwamba wema utashinda uovu na mwanga juu ya giza, lakini katika mazingira ya umoja wetu tu.

Nasimama hapa, nikifahamu kwamba ni vita hivyo vilivyozua mwanzo wa Umoja wa Afrika (Pan-Africanism) na hatimaye kusababisha harakati  la kudai uhuru, na kusambaratisha nguvu za kikoloni. Hii haikutupa maendeleo kamili na nguvu, lakini ilitupa hatua za kwanza kuelekea uhuru wa kisiasa. Ninasimama hapa, nikiongozwa na ndoto na kazi za waanzilishi wakuu wa Umoja wa Afrika (Pan-African), na nikifahamu kwamba kama watoto wa Karibia, tumetamani kwa muda mrefu umoja na kaka na dada zetu wa Afrika. Mgawanyiko ambao ulitekelezwa na wale ambao mafanikio na maisha yao yalitegemea kujitenga kwetu, badala ya uwezo wetu wa kutenda kama watu wa kawaida. Uhusiano wetu, tunaweza kusema, ulikuwa wa kiinitete, lakini cha kusikitisha, kwa kuwa ni wa muda mrefu na uliounganishwa sana kama ulivyokuwa, umebaki mara kwa mara. Ni juu yetu, kama watoto wa mataifa huru, kuamua ikiwa historia ya kutengana itakuwa wakati wetu ujao au kama roho ya Adwa inaweza kututia moyo kukabiliana na changamoto za ulimwengu mpya.

Ndiyo, ninasimama hapa kama binti wa Afrika. Pia nasimama hapa kama Waziri Mkuu mwenye fahari ya Barbados, nchi ambayo ni nchi ya kwanza kufikia baada ya kuondoka katika bara hili kubwa la Afrika. Nchi ambayo hapo awali, ilikuwa kitovu kwa sababu zisizo sahihi lakini, leo hii, ninakuja Ethiopia na Umoja wa Afrika kushiriki nanyi kwamba, sasa tunaweza kuwa kitovu kwa sababu zinazofaa—kuwaleta watu wetu wawili pamoja. Ninasimama hapa kama Mwenyekiti wa fahari wa CARICOM, Jumuiya ya Karibea, nikitambua kwamba kama wanachama wa Kanda ya Sita ya Afrika, tumekuja kurejesha hatima yetu ya Atlantiki. Tumekuja kuhakikisha kwamba wakati ujao wa watu wetu ni tofauti, na hautaamuliwa tena na waamuzi ambao walitumia Njia ya Kati kuona watu wetu chini ya kilindi cha  bahari ya Atlantiki au kufanya kazi kwa bidii katika mashamba ya Karibea. Badala yake, ni lazima tuunde siku zijazo ambapo watu wetu wanaonekana, kusikika, na kuhisiwa, tukihakikisha kwamba tunaamua jinsi tunavyoshirikiana, kuunganisha, na kuwekeza, badala ya kubaki wahanga wa historia ya zamani.

Ninasimama hapa pia kama Mwenyekiti wa V20, muungano wa nchi 70 zinazoathiriwa na hali ya tabianchi, 40% kati hizo wanatoka bara hili kubwa la Afrika. Ninatambua kuwa ni kwa umoja tu ndipo tunaweza kukabiliana na mzozo uliopo wa kizazi chetu- shida ya hali ya tabianchi. Ni mkuu Haile Selassie aliyetukumbusha kwamba hakutakuwa na raia wa daraja la kwanza au daraja la pili, maneno ambayo baadaye yalipendwa na Bob Marley. Maneno haya, tuliyojifunza na watu wetu, yanapaswa kueleweka ndani ya muktadha ambayo yalisemwa na utume waliotuwekea. Mfalme huyo(ndivyo anaitwa kwa sababu ya muziki wake) alituonya kwamba kutakuwa na vita ikiwa watu watachukuliwa kama raia wa daraja la kwanza na la pili, na ikiwa rangi ya ngozi yetu inachukuliwa kuwa muhimu zaidi kuliko rangi ya macho yetu.

Leo, tunaona mizozo barani humo iliyotokana na migawanyiko ya kikabila, kutokana na kunyakua rasilimali—mara nyingi si kwa manufaa yetu wenyewe, bali kwa ajili ya wengine wanaotaka kuwatumia watu wetu kama vibaraka katika kupata maisha yao ya baadaye. Hata hivyo, tunasimama hapa tukiwa watu wenye fahari, wenye uwezo kamili wa kutofautisha mema na mabaya na kutengeneza wakati ujao unaonufaisha wengi, na si wachache tu. Wakati dunia inakabiliwa na mzozo wa tabianchi, ni maskini zaidi kati ya watu maskini ambao wanabaki katika hatari kubwa ya mafuriko, ukame na vimbunga.

Hivi karibuni, hata watu wa tabaka la kati hawataweza tena kupata bima, jambo linalozuia uwezo wao wa kujenga upya na kuendeleza isipokuwa tufanye mabadiliko ya haraka. Tumeona ushirikiano ukifanya kazi kwa ajili yetu, sio tu kupitia moyo wa Adwa na kuongezeka kwa harakati ya Umoja wa Afrika ( Pan-Africanist), lakini pia katika siku za hivi karibuni, wakati wa janga la UVIKO-19, ilikuwa ni Umoja wa Afrika, chini ya uongozi wa Rais Ramaphosa na kwa msaada wa Dk. Tedros wa WHO, ambao walihakikisha kwamba Karibea  haijatengwa. Kupitia Jukwaa la Ugavi wa Matibabu la Afrika, tulipata ufikiaji wa matibabu muhimu, vifaa vya matibabu, na chanjo. Vile vile, kupitia mshikamano wa wengi wenu katika Umoja wa Afrika, Mpango wa Bridgetown ulichukua msingi, ukitetea mfumo wa kifedha wa haki zaidi na wa kisasa ambao unatuwezesha kusitisha ulipaji wa madeni wakati wa migogoro, kuhakikisha uwezo wetu wa kujenga upya baada ya majanga ya hali ya tabianchi.

Hatuhitaji ushahidi zaidi kwamba ushirikiano unafanya kazi. Kinachotakiwa kwetu sasa ni uongozi, kuelekea amani, ufanisi, na haki. Na tunapotoa wito wa kulipwa fidia kutoka katika jumuiya ya kimataifa, kwanza tunaomba kitu rahisi: msamaha. Lazima kukiri kwa dhati kwa makosa. Lakini zaidi ya hayo, fidia lazima pia zihakikishe ufikiaji wa haki wa maendeleo na fidia, kwa sababu safari yetu ya uhuru ilianza na upungufu wa kudumu-upungufu wa rasilimali, haki na fursa. Ni juu yetu sisi, kizazi cha pili na cha tatu cha uhuru, kupanga jinsi ambavyo malipo yanapaswa kuonekana katika mazungumzo yaliyokomaa na yenye kujenga, kuhakikisha haki kwa watu wetu na kuwahamasisha vijana kuamini kwamba wema lazima kushinda uovu daima. Hata hivyo, si jumuiya ya kimataifa pekee ambayo inapaswa kuchukua hatua.

Sisi pia, lazima turekebishe uharibifu uliowekwa juu yetu. Ukweli kwamba watu wetu lazima waombe visa vya usafiri kuzunguka ulimwengu ambao  haukubaliki. Ili kusafiri mashariki au magharibi, tunalazimika kwenda kaskazini. Hii si sawa. Ni ndani ya uwezo wa viongozi wa Kiafrika na Karibea kubadili hili, kujenga madaraja ya anga na baharini ambayo yanahakikisha kwamba tunadhibiti hatima yetu wenyewe. Wacha tufanye mabadiliko haya, sio tu kwa wakuu wa nchi, lakini kwa watu wa kawaida ambao wanataka kufanya biashara, kusafiri na kuunda mustakabali wa pamoja.

Suala la Akili Mnemba  unapotishia kuunda upya ubinadamu, hatupaswi kuachwa tena kama waathiriwa wa teknolojia, kama tulivyokuwa na baruti na ukuaji wa viwanda. Ni lazima tutengeneze siku zijazo, kwa kuwa Afrika siku zote imekuwa nguvu ya hadhi katika ustaarabu. Je, bara ambalo lina 40% ya madini yote duniani linawezaje kuwa mstari wa mbele katika kupata utulivu wa sayari hii? Je, ni kwa jinsi gani eneo linalowakilisha theluthi moja ya mataifa ya ulimwengu lisifanye kazi kwa madhumuni ya umoja kufafanua upya utawala wa kimataifa?

Rafiki zangu, tunapaswa kuulinda ushindi huu. Kufikia 2050, mtu mmoja kati ya kila watu wanne kwenye sayari atakuwa anatoka bara hili au diaspora yake. Viongozi wetu wana umuhimu wa kimaadili kuhakikisha umoja.  Roho ya Adwa inadai kwamba tutambue uwezo wetu, kwamba tutende kwa umoja licha ya nguvu zinazotaka kutugawa. Ikiwa tunashindwa kufikia umoja huu, kosa haliko nje, bali ndani. Wengine wanaweza kuiita hii ndoto ya binti asiye na akili na wa kimapendo wa Kiafrika. Lakini ikiwa hivyo ndivyo, ningependelea kuwa mjinga na mwenye matumaini kuliko kuwa mzaha na kupooza na nguvu za wengine. Historia yetu inathibitisha kuwa umoja unawezekana. Tulipambania ubaguzi wa rangi pamoja. Tulikomboa Afrika Kusini pamoja. Na leo, lazima tutengeneze njia mpya pamoja.

Tunapojitayarisha kwa ajili ya Mkutano wa kwanza wa Umoja wa CARICOM na Afrika, mjini Addis Ababa Septemba hii, tuchukue wakati huu ili kuimarisha ushirikiano wetu. Nchini Barbados, tutaandaa Tamasha la XV la Sanaa la Karibea (CARIFESTA) mwezi Agosti, tukialika familia yetu ya Kiafrika kusherehekea utamaduni wetu wa pamoja, chakula, muziki na falsafa. Hii ni fursa yetu ya kuonesha ulimwengu kwamba sisi siyo  maelezo ya chini tu katika historia, lakini ni wa muhimu katika kuunda siku zijazo. Tuondoe makovu ya historia na tujenge mustakabali unaostahili watu wetu. Ni lazima tujikomboe wenyewe kutoka katika utumwa wa kiakili na kutimiza ahadi ya Adwa. Asante.

Ilifuatiwa makofi mengi ya kumpongeza kwa hotuba yake.

Hotuba ya waziri Mkuu wa Barabados kwa AU
17 Februari 2025, 14:30
Prev
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930   
Next
May 2025
SuMoTuWeThFrSa
    123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031