Gaza,wito wa wakuu ya wayahudi 350:kusema hapana ubaguzi wa kikabila wa Wapalestina
Na Roberto Paglialonga – Vatican.
Habari hiyo hisingekosa kuleta mtafaruku. Ukurasa mzima wa Gazeti la The New York Times, ukiwa mweupe na kisanduku kikubwa cheusi katikati, ambapo maneno machache muhimu yalijitokeza: "Trump ametoa wito wa kufukuzwa kwa Wapalestina wote kutoka Gaza.” Wayahudi wanasema hapana kuwasafisha kikabila Wapalestina! Ombi kubwa la kuelezea hasira zao zote, lililotiwa saini na zaidi ya Wakuu wa Kiyahudi 350, wanaharakati na watetezi wengine wa ulimwengu wa utamaduni wa Kiyahudi wa Amerika Kaskazini, ambao wameamua kulaani pendekezo la rais wa Marekani "kuwaondoa Wapalestina nje ya Ukanda" ili kujenga pwani muhimu ya mali isiyohamishika. Mpango huo ambao utahusisha kuhamishwa kwa takriban watu milioni 2 walionusurika katika mzozo kati ya Israel na Hamas hadi nchi za Kiarabu kama vile Misri na Jordan, ulitangazwa na Trump mwishoni mwa mkutano wa Juma lililopita na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Wawakilishi wa mashirika ya kiraia waliotia saini wito huo ni pamoja na mwandishi wa tamthilia Tony Kushner; mwigizaji Ilana Glazer; Mwandishi na mwanaharakati wa Canada Naomi Klein; mwigizaji Joacquin Phoenix.
Mpango wa Trump ni hila
Katika ripoti kwenye gazeti la The Guardian, Cody Edgerly, mkurugenzi wa kampeni ya ‘”In our name” yaani “Katika Jina Letu,” na mmoja wa waaandaaji wakuu wa tangazo hilo, alisema: “Inatia moyo kuona uungaji mkono wa haraka hivyo kutoka katika nyanja mbalimbali za kidini na kisiasa.” Wazo la Trump, ambalo kwa wengi linaibua Nakba ya 1948, lilipingwa na mmoja wa waliotia saini, Tobia Spitzer, Mkuu wa kiyahudi wa Usharika wa Doshei Tzedek huko Newton, Massachusetts, kama "mpango wa hila ambao ni muhimu kuupinga.” Sisi Wayahudi tunajua vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote vurugu ambazo aina hizi za ndoto zinaweza kusababisha," aliongeza huku akiibua mauaji dhidi ya watu wa Kiyahudi yaliyofanywa na Hitler. Na mkuu wa Kiyahudi Yosef Berman wa Mpango wa ‘New Synagogue’ huko Washington, DC, pia katika orodha ya waliotia saini, alisema kuwa "Mafundisho ya Kiyahudi yako wazi: Trump si Mungu na hawezi kuchukua heshima ya asili ya Wapalestina au kuiba ardhi yao kwa ajili ya mkataba wa mali isiyohamishika. Tamaa ya Trump ya kuwasafisha kikabila Wapalestina kutoka Gaza ni ya kuchukiza kimaadili."
Mkuu wa Kiyahudi Rosen: Ni kinyume na Mkataba wa Geneva
Alipoulizwa na vyombo vya habari vya Vatican kutoa maoni yake, Mkuu wa Kiyahudi David Rosen, mkurugenzi wa zamani wa kimataifa wa masuala ya dini mbalimbali wa Kamati ya Kiyahudi ya Marekani na mshauri maalum wa sasa wa masuala ya dini mbalimbali katika Nyumba ya Familia ya Ibrahimu(Abrahamic) huko Abu Dhabi, alisisitiza umuhimu wa mpango huo, ambao ni muhimu kwa "ulimwengu kujua mengi iwezekanavyo" kwamba wazo la Trump, "kama lilivyo na jinsi linavyokubalika, halikubaliki." Hata hivyo, pia alieleza kuwa haamini kwamba “wito huu utafanya tofauti yoyote, hasa kwa sababu unatoka katika sehemu hiyo ya wigo wa kisiasa ambayo inapingwa" na kiongozi wa sasa wa Marekani, na ambayo kwa hiyo hana nia ya kulipa kipaumbele." Kuhamisha "idadi ya watu dhidi ya mapenzi yao ni kinyume na Mkataba wa Geneva," alisema, "lakini muhimu zaidi, ni ukosefu wa maadili. Wakati watu wanachagua kwa hiari, hilo ni jambo lingine." Lakini "uhamisho wowote wa kulazimishwa haukubaliki kutoka katika mtazamo wa maadili."
Upinzani uliotangulia 2024
Wakuu wa Kiyahudi wa Marekani si kwa mara ya kwanza wanachukua misimamo ya juu ya vyombo vya habari dhidi ya sera za Marekani na kuunga mkono suala la Palestina kama hilo. Kwani ni thelathini na sita kati yao, mnamo Januari 2024, walikatiza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa nyimbo na mabango kumtaka Rais wa wakati huo Bwana Joe Biden kuacha kulipinga Baraza la Usalama kuchukua hatua za haraka za kuunga mkono usitishaji vita wa mara moja na wa kudumu huko Gaza.