Tafuta

2026.07.20 Kongamano la Vijan Wamisionari nchini Mexico. 2026.07.20 Kongamano la Vijan Wamisionari nchini Mexico. 

Mexico:Ask.Mkuu Nwachukwu atoa Wito wa kimisionari kwa vijana ili kutumikia kwa ujasiri

Zaidi ya vijana 6000 Wakatoliki wa Mexico walikusanyika huko Mtakatifu Luis Potosí kwa ajili ya Kongamano la XV la Vijana Wamisionari Kitaifa(CONAJUM)kwa siku nne,ambapo Askofu Mkuu Fortunatus Nwachukwu aliwatia moyo kukubali wito wao wa kimisionari kwa ujasiri.Askofu Mkuu aliwakumbusha kwamba wameitwa kusafiri baharini,wasifungiwe kwenye bwawa na kwamba kila Mkristo aliyebatizwa ametumwa kumtangaza Kristo zaidi ya mipaka yote inayojulikana na yenye starehe.

Na Sr. Christine Masivo, CPS, Vatican.

Jimbo Kuu la Mtakatifu Luis Potosì lilikuwa kitovu cha uhamasishaji wakati wa Kongamano la XV  la Kitaifa la vijana Wamisionari (CONAJUM), lililofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 26 Julai 2026, lililotayarishwa na Mashirika ya Kipapa ya Utume wa Kimisionari(PMS) ya Mexico kwa ushirikiano na Jimbo Kuu la Mtakatifu Luis Potosí. Katika hafla hiyo, iliwakusanya zaidi ya vijana 6,000 kutoka majimbo nchini kote kwa kuongozwa na mada:"Pamoja na Mama Yetu wa Matarajio, Vijana Wenye Matumaini Kupitia Utume!" Kongamano hilo la siku nne liliwaimarisha vijana kupitia sala, mafunzo, uzoefu wa kimisionari, na kujitolea upya kwa uinjilishaji, ikiwa ni pamoja na utume unaokua katika ulimwengu wa kidijitali.

Nendeni Ulimwenguni kote

Askofu Mkuu Fortunatus Nwanchuku,Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji (Kitengo cha Kwanza cha Uinjilishaji na Makanisa Mapya maalumu), aliwapatia changamoto vijana kuitikia kwa moyo wote agizo la kimisionari la Kristo. Aliwapatia msukumo huu kutoka katika amri ya Injili, "Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Injili kwa kila kiumbe," akiwakumbusha kwamba Wakristo wote wameitwa kutangaza mema. Habari kwa wote ana kwa ana na hata katika nafasi ya kidijitali.

Wito wa kutupa nyavu ndani ya kina kirefu

Askofu Mkuu aliwahimiza vijana kusonga mbele zaidi ya mazingira wanayojua kama wanafunzi wa Yesu kwenye Bahari ya Galilaya. “Hamtumwi kwenye aquarium yaani bwawa, mahali penye nafasi ndogo, salama, inayotabirika, na inayodhibitiwa, bali katika bahari iliyo wazi, ambayo ni kubwa, yenye kina kirefu, na wakati mwingine, yenye dhoruba,” alisema, huku akisisitiza kwamba kila moyo wa mwanadamu umeumbwa kwa ajili ya upeo mpana wa utume wa Mungu. Aliwakumbusha kwamba, wito wao wa kimisionari ulianza wakati wa Ubatizo na kwamba walikuwa tayari wametumwa na wamekabidhiwa utume: “kumjua Kristo, kumpenda, na kumfuata." Ujumbe wake uliwaita kumwamini Mungu na kutangaza Injili kwa ujasiri popote walipo.

Moyo wa kimisionari

Askofu Mkuu aliwatia moyo kukumbatia sifa tatu muhimu za mmisionari ambazo wanapaswa kukuza: Ya kwanza ni kujitenga. Nia ya kuacha chochote kinachozuia kujitolea kwa undani kwa Kristo. Ya pili ni kukutana yaani, kutambua kwamba Uinjilishaji wa kweli huanza na mahusiano ya kweli badala ya kuwasilisha mawazo tu. Hatimaye, Askofu Mkuu alizungumzia kuhusu kukubali Msalaba, na kukubali kwamba, kazi ya kimisionari mara nyingi inahitaji kujitolea, uvumilivu, na uaminifu hata wakati matokeo ya haraka hayaonekani. Aliwasihi vijana pia  changamoto za utume. "Bahari ya ubinadamu ni kubwa." Ulimwengu unawahitaji wamisionari. Kanisa linawahitaji. Na Kristo anawaita." Alihitimisha kwa changamoto ya kibinafsi, na swali, "Je, uko tayari kutoa kitu cha maisha yako ili kuleta uso wa Kristo kwa wengine?"

Kuwa mwanafunzi wa kimisionari kwa leo

Kongamano liliadhimisha mwendelezo wa kazi ya kimisionari ya Kanisa huku likitazama mstakabali kwa  ujasiri. Katika fursa ya Kongamano hilo sambamba na maadhimisho ya miaka mia moja ya utume Duniani na maadhimisho ya miaka 75 ya umoja wa  Wamisionari wa Vijana wa Mexico, Kongamano hilo la Vijana Kitaifa lilithibitisha tena kujitolea kwa Kanisa kuunda wanafunzi wachanga wa kimisionari.

Antonio de Jesus Mascorro Tristán, MG, Mkurugenzi wa Kitaifa wa Vyama vya Kitume vya Kipapa PMS vya Mexico, alibainisha kuwa makongamano yamekuwa yakiunda mafunzo ya kimisionari tangu 1982 kupitia programu tajiri ya makongamano, ushuhuda, Ibada za Misa, sala, na ushirika. Jambo muhimu la Kongamano la mwaka huu lilikuwa ni mkazo wake katika uinjilishaji wa kidijitali, ambapo waundaji wa maudhui ya Kikatoliki walishirikisha jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kuwa nafasi ya kutangaza Injili. Tukio hilo lilihitimishwa  kwa maandamano ya kimisionari na Misa  ya kufunga iliyoongozwa na Askofu Mkuu Joseph Spiteri, ambaye aliwasilisha baraka za Papa Leo XIV. Washiriki waliondoka sio  kwa kuhudhuria mkutano mkuu  tu bali  pia wakiwa na ahadi mpya ya kurudi katika jumuiya zao kama wanafunzi wa kimisionari, wakishiriki wa tumaini na furaha ya Injili.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

01 Agosti 2026, 13:49