Tafuta

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Askofu Msaidizi Mariusz Kasperski, O.M.I wa Jimbo Kuu Katoliki la Toamasina, Madagascar tarehe 19 Agosti 2026. Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Askofu Msaidizi Mariusz Kasperski, O.M.I wa Jimbo Kuu Katoliki la Toamasina, Madagascar tarehe 19 Agosti 2026.  (@VATICAN MEDIA)

Askofu Msaidizi Mariusz Kasperski, O.M.I wa Jimbo Kuu Katoliki la Toamasina

Baba Mtakatifu Leo XIV, tarehe 19 Agosti 2026 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Mariusz Kasperski, O.M.I., Mmisionari wa Shirika la Oblati wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Toamasina nchini Madagascar. Askofu mteule alizaliwa tarehe 15 Agosti 1963 huko nchini Poland. Akaweka nadhiri zake za daima tarehe 8 Septemba 1991 na hatimaye, kupewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 21 Juni 1993.

Na Padre Richard A. Mjigwa C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, tarehe 19 Agosti 2026 amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Mariusz Kasperski, O.M.I., Mmisionari wa Shirika la Oblati wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Toamasina nchini Madagascar. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Msaidizi mteule Mariusz Kasperski, O.M.I., alikuwa ni Mkuu wa Jumuiya ya Oblati wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili Jimbo Katoliki la Toamasina. Itakumbukwa kwamba, Askofu Msaidizi Mariusz Kasperski, O.M.I., alizaliwa tarehe 15 Agosto 1963 huko mjini Wolsztyn, Jimbo kuu la Poznań, nchini Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kitawa na Kipadre, tarehe 8 Septemba 1991 akaweka Nadhiri zake za daima na hatimaye, kupewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 21 Juni 1993 huko Obra.

Papa Leo XIV akiwa na Maaskofu wa Madagascar
Papa Leo XIV akiwa na Maaskofu wa Madagascar   (@VATICAN MEDIA)

Baadaye kama Padre na Mmisionari alifanya utume wake nchini Poland na Madagascar na baadaye akateuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya “Saint Jean Baptiste” huko Analakininina, Jimbo kuu la Toamasina kati ya Mwaka 1997 hadi mwaka 1999. Na kati ya Mwaka 1999 hadi mwaka 2006 aliteuliwa kuwa ni Mlezi wa wale waliokuwa wanajiandaa kujiunga na Unovisi. Kati ya Mwaka 2003 hadi Mwaka 2025 alikuwa ni Mwakilishi wa Shirika la Oblati wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili nchini Madagascar; Paroko na Mkuu wa Jumuiya ya Antananarivo huko Soavimbahoaka  kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2012; Paroko wa Parokia ya “Saint Jean Paul II” huko Tsimahavaobe, Jimbo Katoliki la Morondava kati ya Mwaka 2012 hadi mwaka 2015; Mkuu wa Shirika la O.M.I. nchini Madagascar kati ya Mwaka 2015 hadi mwaka 2022; Mkuu wa Jumuiya O.M.I., Jimbo kuu la Toamasina na Paroko wa Parokia ya “Saint Eugène de Mazenod” huko Tsarahonenana, Jimbo kuu la Toamasina tangu mwaka 2023 hadi uteuzi wake tarehe 19 Agosti 2026 wa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Toamasina nchini Madagascar.

Uteuzi Madagascar
20 Agosti 2026, 15:40