Tafuta

Utoaji mimba siyo chaguzi la kweli. Utoaji mimba siyo chaguzi la kweli.  Tahariri

Utoaji mimba kamwe si chaguo la kweli!

Karibu kila nchi duniani ambapo sheria zimepitishwa zinazoruhusu mauaji ya mtoto tumboni mwa mwanamke zina vifungu vinavyolenga kuzuia mauaji haya:kwa usaidizi, utunzaji,ukaribu,lakini sheria hizi zinabaki bila kutumika kwa karibu visa vyote.Tunazungumzia kuhusu chaguzi za wanawake,kuhusu matibabu,lakini hatutoi fursa halisi ya kuchagua kwa sababu tunapendekeza njia inayoonekana kuwa rahisi zaidi,lakini si rahisi.Ni tahariri inayoakisi Ulinzi wa Mwanadamu tangu kutungwa kwake hadi kifo.

Massimiliano Menichetti

Kuna picha na historia zinazosambaa sana, zinazoakisi ukweli, uzuri, na ushirika, zinazotoa matumaini, kama mfululizo uliorekodiwa nchini Colombia, ukimuonesha mama akiwa chini ya kifusi, akimlinda mwanawe mchanga kwa mwili wake baada ya jengo la ghorofa tano kuanguka katika kitongoji cha mji wa Cali, kwa kusababishwa  na tetemeko la ardhi la ukubwa wa kipimo cha 7.4. Picha hizo, ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na habari za televisheni, zinaonesha hofu ya uharibifu huo, waokoaji wakitafuta na kukimbia dhidi ya wakati na vifusi, na mwanamke huyo na mtoto walitolewa wakiwa hai na sasa wako nje ya hatari. Taswira hiyo, katika ubora wake wa mwonekano, inakamata jamii nzima, yenye udugu na usaidizi, yenye nia ya kuokoa, kujali, na kuchukua jukumu kwa wengine, na kujiokoa yenyewe. Haijalishi ni rasilimali ngapi zinahitajika: lengo ni kuhifadhi hata maisha ya mtu mmoja tu.

Takriban kilomita 4,300 kutoka Massachusetts, Marekani tukio hilo ni  tofauti kabisa: ni ile ya hati inayotakiwa kusainiwa. Na maisha ya mtoto, katika kesi hii akiwa tumboni mwa mama, hayaonekani tena; kitu kingine kinapewa kipaumbele. Hapa, ilisainiwa  "Sheria ya Kuweka Kipaumbele cha Upatikanaji wa Huduma kwa Mgonjwa" (“Prioritizing Patient Access to Care Act”), sheria inayoondoa kikomo cha Juma ishirini na nne cha utoaji mimba kwa hiari na kutoa uamuzi mpana kwa uamuzi wa kitaalamu wa daktari. Ndani ya Sheria hii ina neno "tiba," lakini hapa ina maana sawa na kifo. Sasa  kuna majimbo kumi nchini Marekani ambayo hayana vikwazo vya jumla kuhusu utoaji mimba. Katika hali hii, maisha hayajashinda. Ulimwenguni yanaenea, hatua kwa hatua, katika ukimya wa usahihi wa kisiasa au katikati ya kishindo cha upinzani wa kiitikadi unaogongana, upepo wa kifo dhidi ya binadamu. Kwa mfano, mwaka huu tu, Luxembourg ilijumuisha uhuru wa kutoa mimba katika Katiba yake, nchi ya pili baada ya Ufaransa kuwa na marejeo dhahiri katika Katiba yake na Uingereza iliiondoa hatia ikiwa itafanywa nje ya mfumo wa kisheria.

Karibu kila nchi duniani ambapo sheria zimepitishwa zinazoruhusu mauaji ya mtoto tumboni mwa mwanamke zina vifungu vinavyolenga kuzuia mauaji haya: kwa usaidizi, utunzaji, ukaribu, lakini sheria hizi zinabaki kama vitendo bila kutumika kwa karibu visa vyote. Kwa sababu ni ghali sana. Tunazungumzia kuhusu chaguzi za wanawake, kuhusu matibabu, lakini hatutoi fursa halisi ya kuchagua kwa sababu tunapendekeza njia inayoonekana kuwa rahisi zaidi, lakini ambayo si rahisi. Tunapendekeza uingiliaji kati wa haraka, kuondoa tatizo, kufumbia macho, kukataa ushahidi wote wa kisayansi unaoonesha jinsi ambavyo  tangu wakati wa kutungwa mimba, mchakato usiozuilika huanza ambao humtengeneza mtu. Kupendekeza kuua bila kusema hivyo. Kumruhusu mwanamke chaguo halisi kungemaanisha kutoa msaada wa kisaikolojia, kifedha, na kiroho, lakini hii inakuja kwa gharama kubwa zaidi katika suala la fedha na rasilimali, kwa hivyo ni bora kukaa kimya.

Serikali moja huonesha mtazamo wake kamili na upeo wake inapowajali raia wake, inapohakikisha amani, usawa, haki ya uhuru wa kujieleza, na kulinda maisha; wananchi wanapojenga jamii yenye uwezo wa kuwatambua wengine, kuwasaidia, kuwaunga mkono, kuwasindikiza, na kuwapenda, na kujenga  kwa wakati uliopo mizizi ya mstakabali. Utoaji mimba kisha unakuwa uthibitisho au upotoshaji wa yaliyo mema na mabaya, yaliyo ya kuunga mkono uhai na yaliyo kinyume na uhai. Upotoshaji huo upo katika kutaka kuficha mateso, ugumu, na maumivu, badala ya kutaka kuwakumbatia wale wanaojikuta katika hali mbaya na wasiopata njia ya kutokea. Hapa ndipo tunapopima ubinadamu ambao hauui, bali unapenda na kujali, ambao uko tayari kupitia vifusi ili kuokoa maisha na kufurahi kikamilifu wakati hili linapotokea.

ULINZI WA MAISHA TANGU KUTUNGWA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

13 Agosti 2026, 16:07