Papa amemteua Balozi El-Kassis,kuwa Mwakilishi wa Kudumu UN huko New York
Vatican New
Papa Leo XIV tarehe 25 Julai 2026, alimteua Askofu Mkuu Christophe-Zakhia El-Kassis, Askofu Mkuu wa Roselle, kama Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) huko New York, Marekani. Hapo awali alikuwa Balozi wa Vatican katika Falme za Kiarabu na Yemen na mjumbe wa kitume katika Ghuba ya Arabia.
Mnamo Januari 2023, Papa Francisko alimteua kuwa Balozi wa Vatican katika Falme za Kiarabu, na mnamo Julai 2024, pia kwa Yemen na mjumbe wa kitume katika Ghuba ya Arabia. Mnamo Novemba 2018, Papa wa wakati huo alimteua kuwa Balozi wa Vatican enchini Pakistan, akimpandisha cheo cha kiti cha Roselle, na heshima ya Askofu Mkuu.
Alizaliwa Beirut, Lebanon, mnamo tarehe 24 Agosti 1968, Askofu Mkuu El-Kassis alipewa daraja la upadre 21 Mei 1994. Aliingia katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican mnamo tarehe 19 Juni 2000, na alihudumu kama mshauri wa ubalozi katika ubalozi wa kitume nchini Indonesia, Sudan, Uturuki, na katika Kitengo cha Mahusiano na Nchi za Sekretarieti ya Nchi. Anazungumza Kiarabu, Kifaransa, Kiitaliano, Kiingereza, Kiindonesia, Kihispania, na Kijerumani.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.