Tafuta

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, aliyekuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii, kuwa Katibu mkuu mpya wa Baraza la Kipapa kwa Ajili ya Huduma ya Upendo Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, aliyekuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii, kuwa Katibu mkuu mpya wa Baraza la Kipapa kwa Ajili ya Huduma ya Upendo   (ANSA)

Monsinyo Lucio Adrian Ruiz Katibu Mkuu Baraza la Huduma ya Upendo

Papa Leo XIV amemteuwa Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, aliyekuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii, kuwa Katibu mkuu mpya wa Baraza la Kipapa kwa Ajili ya Huduma ya Upendo na anaanza utume huu tarehe Mosi, Septemba 2026. Itakumbukwa kwamba, Monsinyo Ruiz, alikuwa ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha “Santa Croce” na Mjumbe wa Kikosi maalum cha Teknolojia ya Akili Unde katika Taasisi ya Kipapa ya Maisha!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baraza la Kipapa kwa Ajili ya Huduma ya Upendo, ambalo pia huitwa, Ofisi ya Misaada ya Kitume, ni kielelezo cha pekee cha huruma na upendo wa Mungu, kwa kutoa upendeleo wa pekee kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii; watu wanaohitaji kuonjeshwa huruma na upendo kutoka kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro ambaye katika hali ya umaskini au mahitaji mengine ambayo Baba Mtakatifu binafsi anaamua juu ya misaada itakavyogawiwa. Baraza hili liko chini ya Mtunzaji mkuu wa Sadaka ya Kipapa anayeshirikiana na Mabaraza mengine, ili kuhakikisha kwamba, misaada inawafikia walengwa, kutoka kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, Mchungaji mkuu wa Kanisa la Kiulimwengu kwa ajili ya maskini, watu wanaosukumiziwa pembezoni mwa jamii au katika matukio ya majanga makubwa yanayoendelea kuwasibu walimwengu.

Mons. Lucio Adrian Ruiz, Katibu mkuu Baraza la Huduma ya Upendo
Mons. Lucio Adrian Ruiz, Katibu mkuu Baraza la Huduma ya Upendo

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, aliyekuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii, kuwa Katibu mkuu mpya wa Baraza la Kipapa kwa Ajili ya Huduma ya Upendo na anaanza utume huu mpya kuanzia tarehe Mosi, Septemba 2026. Itakumbukwa kwamba, Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, alikuwa ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha “Santa Croce” na Mjumbe wa Kikosi maalum cha Teknolojia ya Akili Unde katika Taasisi ya Kipapa ya Maisha na tangu tarehe 27 Juni 2015 aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii.

Maskini ni amana na utajiri wa Kanisa
Maskini ni amana na utajiri wa Kanisa   (AFP or licensors)

Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, alizaliwa tarehe 5 Machi 1965 huko Jimbo kuu la “Santa Fe” nchini Argentina. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 30 Septemba 1990 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la “Santa Fe, Argentina. Baada ya kufanya kazi sehemu mbalimbali kama mtaalamu mbobezi wa teknolojia ya mawasiliano ya jamii, Baba Mtakatifu Francisko tarehe 27 Juni 2015 akamteuliwa kuwa ni Katibu mkuu mpya wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii na ilipo gota tarehe 30 Juni 2026 Baba Mtakatifu Leo XIV akamteuwa kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa Kwa Ajili ya Huduma ya Upendo.

Mons. Lucio Adrian Ruiz, Katibu mkuu Baraza la Kipapa la Huduma
Mons. Lucio Adrian Ruiz, Katibu mkuu Baraza la Kipapa la Huduma

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Dr. Massimo Ralli, Afisa mkuu mtendaji Baraza la Kipapa Kwa Ajili ya Huduma ya Upendo aliyezaliwa tarehe 20 Januari 1982 kuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Huduma ya Upendo. Dkt. Massimo Ralli amekuwa profesa msaidizi katika Idara ya “Sense Organs,” Chuo Kikuu cha Sapienza cha Roma tangu mwaka 2018. Alipata Shahada yake ya Uzamili ya udaktari na upasuaji kutoka Chuo Kikuu cha Sapienza cha Roma. Alimaliza Shahada yake Uzamivu katika “neurophysiology” kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki Cha “Sacro Cuore” kunako mwaka 2014 na ameendelea na shughuli ya kufundisha, kufanya tafiti na kutibu.

Huduma ya Upendo
01 Julai 2026, 15:45