Siku ya kuwekwa wakfu wa maaskofu Wafebvrerian huko Uswiss. Siku ya kuwekwa wakfu wa maaskofu Wafebvrerian huko Uswiss.  (AFP or licensors)

Kuwekwa Wakfu kwa Maaskofu wa Walefebvrian:Amri ya Kutengwa imetolewa

Hati iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa inafafanua wazi juu ya ibada inayoadhimishwa Julai 1 kama "kitendo cha asili ya mgawanyiko."Maelezo yanabainisha kwa undani kuhusu adhabu kubwa ya kisheria.

Vatican News

Maaskofu wa Jumuiya ya Mapadre wa Mtakatifu Pio X, Alfonso de Galarreta na Bernard Fellay (wote wawili waliowekwa wakfu kwanza) na Maaskofu wapya waliowekwa wakfu: Pascal Schreiber, Michael Goldade, Michel Poinsinet de Sivry, na Marc Hanappier, wamejikuta katika "ipso facto"et "latae sententiae" yaani tendo moja sawa kwa hukumu inayotolewa na Kiti cha Kitume kutokana na kufanya "tendo la asili ya mgawanyiko," hasa "kuwekwa wakfu wa kiaskofu mapadre wanne, bila idhini ya kipapa na kinyume cha utashi wa Baba Mtakatifu." Haya yameelezwa katika amri(Decreto) iliyosainiwa na Kardinali Víctor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kusainiwa na makatibu wawili wa Baraza hilo hilo. Kwa bahati mbaya, hili ndilo hitimisho, ambalo limetangazwa, na ambalo linakuja saa ishirini na nne(24)baada ya sherehe kuu iliyoadhimishwa huko Écône, Uswiss asubuhi ya tarehe 1 Julai 2026.


Amri ya Ofisi Takatifu ya awali inathibitisha kwamba katika tendo la kutekeleza kuwekwa wakfu, wawekaji wakfu na waliowekwa wakfu wanajikuta wakitengwa na Kanisa kwa njia inayotarajiwa. Ni uchungu mwingi, matokeo ya maamuzi yaliyochukuliwa na Walefebvrian dhidi ya utashi ambao mara nyingi ulielezwa na Papa Leo XIV.  Kutengwa kwa Kanisa kunawakataa Maaskofu na mapadre wote, ambao ni wa Jumuiya ya Mtakatifu Pio X, kwa kujitenga na Kanisa la Roma. Kuhusiana na waamini walei, vile vile watafikiriwa kutengwa ikiwa  wataudhuria kwa kawaida Udugu huo. Sehemu kubwa ya maelezo zaidi iko katika “Nota esplicativa”, hati ya maelezo hayo iliyochapishwa na Baraza la Kipapa pamoja na hati ya kutengwa, ambayo tunaiwekwa kamilifu.

Amri kutoka Baraza la kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa
Amri kutoka Baraza la kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa

Andiko la  Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa 

Katika nyakati za Mtakatifu Paulo VI hadi mazungumzo ya mwisho, yaliyofanywa hivi karibuni katika Baraza la Kipapa, majaribio mengi ya kuweza kuirudisha harakati hiyo iliyoanzishwa na Askofu Marcel Lefebvre, katika muungano kamili na Kanisa Katoliki zionekana bure. Hali hizo ziliongeza kuwa mbaya sana, kwa sababu ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu uliofanyika bila idhini ya Papa, dhidi ya utashi wa Baba Mtakatifu, kwa ukiukaji wa wazi wa Haki za sheria. Kwa hivyo, Baraza hili la Kipapa, katika utekelezaji wa kazi zilizokabidhiwa kwake kwa uaminifu, linaona ni muhimu kutambua kwamba kitendo hiki kilikuwa uhalifu wa mgawanyiko, na matokeo yake yalikuwa ya kisheria kwa wahudumu wa matakatifu na kwa waamini walei waliohusika. Kwa hakika, kama ilivyokuwa imetangazwa tayari kunako mwaka 1988, “kutotii huko, ambako kunapelekea kukataa zoezi la Ukuu wa Roma kunafanya kitendo cha mgawanyiko (Yohane  Paulo II,  Ecclesia Dei, 3).


https://www.vatican.va/content/john-paul-ii/it/motu_proprio/documents/hf_jp-ii_motu-proprio_02071988_ecclesia-dei.html

Kwa mtazamo huo na kuendelea:

1. Wahudumu wa Jumuiya ya Udugu wa Mapadre wa Mtakatifu Pio X, wako katika mgawanyiko na kwa hivyo lazima wachukuliwe kama mgawanyiko(taz. Ecclesia Dei, 5 c; Baraza la Kipapa la Maandiko ya Kutunga Sheria, Maelezo ya Kutengwa kwa ajili ya mgawanyiko unaosababishwa na wale wanaofuata harakati za Askofu Marcel Lefebvre, 24.08.1996, 5-6), na wanakabiliwa na kuondolewa kwa ushirika kama ilivyoainishwa na sheria (can. 1364 § 1 CIC).

2. Kuhusu waamini walei, wale wanaofuata rasmi Jumuiya ya Udugu wa Kipadre wa Mtakatifu Pio X wanapaswa kuchukuliwa kuwa ni watenganifu na kutengwa chini ya masharti yaliyowekwa katika Maelezo ya Baraza la Kipapa la Maandiko ya Kutunga Sheria ya 1996 (taz. ibidem, 7), ambayo bado ina nguvu na ambayo Baraza hili linaikubali kama yake.

https://www.vatican.va/roman_curia/pontifical_councils/intrptxt/documents/rc_pc_intrptxt_doc_19960824_vescovo-lefebvre_it.html

3. Hatimaye, Watu watakatifu wa Mungu wanaonywa kwamba wahudumu wa Jumuiya ya Udugu wa Mapadre wa Mtakatifu Pio wa X hutoa sakramenti kinyume cha sheria, na kwamba sakramenti ya toba inayotolewa nao na ndoa zinazosaidiwa nao ni batili. Kanisa, kama mama anayejali, litawakaribisha kwa upendo wa dhati na kwa shauku kubwa wale wote wanaotaka kurudi kwenye ushirika kamili.

Balozi wa Kitume atapanga taratibu ambazo Maaskofu wanaweza kutumia katika kesi mbalimbali. Na mwishoni waamini wote wanahimizwa kubaki imara katika ushirika na Baba Mtakatifu wa Roma, pamoja na Maaskofu katika ushirika naye, na pamoja na Kanisa lote (taz. Lumen Gentium, 22; can. 751 CIC), na kujiepusha kushiriki katika sherehe na shughuli zinazoendelezwa na Jumuiya ya Udugu wa Mapadre wa Mtakatifu Pio X uliotajwa hapo juu.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

02 Julai 2026, 09:00