Tafuta

Jumuiya Mtakatifu Pio X yawaweka wakfu maaskofu wanne wapya bila idhini ya Vatican. Jumuiya Mtakatifu Pio X yawaweka wakfu maaskofu wanne wapya bila idhini ya Vatican.  (ANSA)

Walefebvrian wawaweka wakfu maaskofu wanne wapya bila agizo la Papa

Katika makao makuu ya Udugu wa Kipadre wa Mtakatifu Pio X nchini Uswiss,Maaskofu Alfonso de Galarreta na Bernard Fellay wameongoza kuwekwa wakfu kwa Maaskofu, na Mkuu wa Shirika hilo alitangaza:“Adhabu au karipio zozote zilizotolewa kwa kitendo hiki hazina thamani yoyote."Adhabu au karipio zozote zilizotolewa kwa kitendo hiki hazina thamani yoyote."

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Vazi la Kristo lisilo na mshono, ambalo Papa Leo XIV alikuwa amesihi katika barua kutoka mwake moyoni mnamo Juni 29 "lisichanike  vipande vipande," sasa, kwa maoni ya Vatican, limechanika! Asubuhi ya Jumatano tarehe 1 Julai 2026 huko Ecône, Uswiss katika makao makuu ya Jumuiya ya Mapadre wa Mtakatifu PioX (FSSPX)—Walefebvrian,  wafuasi wa Askofu Mkuu Marcel Lefebvre, waliwaweka wakfu maaskofu wapya wanne bila agizo la Papa.

Walifanya hivyo ingawa maaskofu wapya walijibu kwa kukubali swali la kiliturujia, "Habetis mandatum apostolicum?" ("Je, una Mamlaka ya Kitume?"). Walihalalisha uwekaji wakfu kama muhimu ili kuhakikisha mwendelezo na uhai wa Jumuiya  yao, licha ya juhudi za Kiti Kitakatifu katika mazungumzo na maonyo ya mara kwa mara dhidi ya kuendeleza kile kilichoonekana kama kitendo cha mgawanyiko. Maonyo hayo yalitoka kwa Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti  wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  na pia kutoka kwa Papa Leo XIV mwenyewe katika barua iliyotolewa siku mbili kabla ya kuwekwa wakfu huko.

Sherehe huko Ecône

Zaidi ya mapadre 1,000, wanaume na wanawake watawa, na watu wapatao 15,000 walihudhuria sherehe hiyo, iliyoanza saa 3:00 asubuhi katika kibanda kikubwa cheupe karibu na seminari ya FSSPX. Tukio hilo lilirushwa moja kwa moja kwa lugha sita kwenye tovuti rasmi ya Jumuiya hiyo  ambapo idhadi ya sherehe hiyo ilikuwa ikiendelea katika siku za hivi karibuni, ikiambatana na mambo ya ukumbusho na matukio mengine yanayohusiana.

Maaskofu wanne waliowekwa wakfu  ​​ni Pascal Schreiber, Padre wa  Uswisi mwenye umri wa miaka 53 aliyewekwa wakfu huko Ecône mnamo 1998; Michael Goldade, asili yake ni Dakota Kaskazini na alikulia Kansas, Marekani; Michel Poinsinet de Sivry, 42; na Marc Happier, 36, wote wakiwa Wafaransa. Mshereheshaji mkuu aliyefanya ibada hiyo ya wakfu alikuwa Askofu Alfonso de Galarreta, huku Askofu Bernard Fellay. Wao ni Maaskofu wawili waliosalia miongoni mwa wanne waliowekwa wakfu awali na Askofu Mkuu Lefebvre mnamo  tarehe 30 Juni 1988. Kulingana na sheria ya Kanisa Katoliki, kutekeleza ibada hizo bila agizo la Papa kunasababisha kutengwa kwa latae sententiae (mara moja).

Hotuba ya Pagliarani, Mkuu wa Shirika

Mwanzoni mwa liturujia, Mkuu  wa Jumuiya ya Mtakatifu Pio X, Ndugu Davide Pagliarani, alitoa hotuba fupi akisema, "Tuko tayari kulipa gharama yoyote ili kuokoa Kanisa." Kulingana na Mkuu huyo hivyo ni "jukumu zito zaidi" "kukabidhi neema ya uaskofu kwa makuhani hawa." Tunaona kwamba adhabu au lawama zozote zilizowekwa kwa kitendo hiki hazina thamani yoyote," aliongeza. Kwa Walefebvrian, mkuu wao alihitimisha, akisema kuwa leo ni "siku ya kihistoria" na "sherehe." Hata hivyo, kwa Kanisa la ulimwengu wote, ni siku ambayo, katika tathmini ya Vatican, jeraha la zamani limefunguliwa tena yaani jeraha la mgawanyiko.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

01 Julai 2026, 14:21