Tafuta

Askofu Mkuu Balestrero,Mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa huko Geneva. Askofu Mkuu Balestrero,Mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa huko Geneva. 

Vatican:Kuelekea utamaduni wa majadiliano ili kujenga amani

Askofu Mkuu Balestrero,Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa na Mashirika Mengine ya Kimataifa huko Geneva,akizungumza katika Kikao cha 62 cha Baraza la Haki za Binadamu alisema:"Leo,ongezeko la migogoro linapunguza ufadhili wa maendeleo.Gharama halisi ya haya yote inawaangukia maskini na wahitaji."Onyo dhidi ya taarifa potofu:Utafutaji wa ukweli ni muhimu kwa demokrasia."

Vatican News

Ili kujenga amani, ni muhimu kuhama kutoka 'utamaduni wa madaraka' hadi 'utamaduni halisi wa mazungumzo' unaotegemea mshikamano na kutambua kwamba jirani yetu si adui hasa, bali ni mwanadamu mwenzake. Hiki ndicho kiini cha kauli ya Askofu Mkuu Ettore Balestrero, Mwakilushi wa Kudumu wa Vatican katika  Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa huko Geneva, Uswiss katika hotuba yake wakati wa Kikao cha Kawaida cha 62 cha Baraza la Haki za Binadamu.

Udugu na urafiki wa kijamii, kiini cha kila uhusiano wa haki

Mjumbe wa Vatican alitoa msukumo wa tafakari yake kutokana na Ripoti ya Wataalamu Huru wa Amani na Mshikamano wa Kimataifa, ambayo ilisisitiza "umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa utatuzi wa amani wa mizozo kuhusu ujeshi na mgawanyiko," kama ilivyoainishwa pia katika Hati ya Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo, Askofu Mkuu Balestrero alisisitiza kwamna inasisitiza ukweli kuwa "leo, ongezeko la migogoro linaambatana na kupunguzwa kwa wakati mmoja kwa ufadhili wa maendeleo, pamoja na kupunguzwa kwa bajeti kwa ajili ya afya, elimu, na sekta zingine za kijamii." Na "kwa bahati mbaya, gharama halisi ya haya yote inawaangukia maskini zaidi na wenye uhitaji zaidi," Askofu Mkuu alisema. Kisha alisema kuwa inavutia umakini wa pamoja kwenye mada za "udugu" na "urafiki wa kijamii:" kanuni, ambazo lazima ziwe katikati ya uhusiano wowote wa haki kati ya watu,"alisema.

Taarifa potofu zinaendeleza utengwaji

Askofu Mkuu Balestrero kisha alizingatia  "tabia ya taarifa potofu kwenye mitandao ya kijamii na katika mazungumzo ya kisiasa" ambayo "huendeleza utengwaji wa watu wa dini au makabila tofauti, na kuongeza hatari ya kuchochea ubaguzi na/au vurugu." "Amani na mshikamano" pia ziko hatarini. Katika suala hilo, Askofu Mkuu alinukuu waraka wa hivi karibuni wa Papa Leo XIV wa Magnifica Humanitas, ambapo Papa alisisitiza kwamba: "Taarifa potofu hazikutokana na AI, lakini leo zinapata kipaza sauti chenye nguvu katika AI. Uwezo wa kudhibiti maudhui, picha, na video huwaweka watu katika mitazamo potofu au inayopotosha." "Utafutaji wa ukweli," mjumbe huyo alihitimisha, "ni kipengele muhimu cha demokrasia, ambacho chenyewe ni njia ya kuchangia kwa manufaa ya wote."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

18 Juni 2026, 14:38