Tafuta

2026.04.20 Viaggio Apostolico in Angola - Visita alla Casa di accoglienza per anziani

Pope Leo XIV:Uzee ni ushuhuda wa kwanza na wenye mamlaka zaidi kupitia uzoefu na hekima

Katika barua iliyotumwa kwa Kardinali Kevin Farrell,Mwenyekiti wa Baraza la Walei,Familia na Maisha wakati wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi uliowekwa wakfu kwa Utunzaji wa Kichungaji wa Wazee anathibitisha tena thamani ya wazee na jukumu lao kama walimu wa maisha.Wazee mara nyingi hutoa huduma nyingi kwa jamii.Huu ni wakati wa neema,unaoishi katika sala,huduma na huruma.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV wakati huyo katika Ziara yake ya Kitume nchini Hispania kuazia 6 -12 Juni 2026, ilituma barua kwa niaba yake na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin kwa Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia, na Maisha, wakati wa Siku ya Mafuzo ya Kichungaji ya wazee iliyaoandaliwa na Baraza hilo kwa kuongazwa na mada: "Daraja kuelekea Mbinguni. Majisterio ya Udhaifu katika Wakati nguvu," tarehe 10 Juni 2026, katika ukumbi wa Pio XI wa Jumba la Mtakatifu Calisti, Roma.

Kwa njia hiyo Papa kuhusu Utunzaji wa Kichungaji wa Wazee alibainisha kuwa “Wazee, kwa kukubali kwa utulivu mapungufu yanayowekwa na miaka inayopita bila kuyaficha au kuyaonea aibu wanaweza kuwa walimu wa maisha, na kuweza kuwaonyesha kila mtu na hasa vijanakwamba thamani ya maisha haipimwi kwa ufanisi au kujitosheleza, bali kwa uwezo wa kupenda na kupendwa, kutoa na kupokea.

Thamani ya udhaifu

Katika jamii ya leo, uzee ni kipindi kigumu cha maisha, wenye uwezekano mwingi, na kwa Kanisa, ambalo limewahi kutambua uwepo muhimu kwa wazee, mpango huu hakika ni muhimu sana, alisisitiza. "Leo, katika maeneo mengi ya dunia, wazee, mara nyingi bado wana nguvu nyingi za kujitolea katika huduma kwa jamii." Alisema hili linaonekana katika aina mbalimbali za kujitolea, ambazo ni muhimu katika maeneo mengi ya maisha ya kikanisa. Lakini zaidi ya haya, uzee, Baba Mtakatifu alibainisha, pia unaelekeza umakini kwenye kipengele cha kina na muhimu zaidi cha maisha ya Kikristo, yaani thamani ya udhaifu.

Mtazamo wa Kikristo wa kuishi wakati huu ni upi?

Baba Mtakatiu Leo alipendekeza kwamba ongezeko la wastani wa matarajio ya maisha bila shaka linahusisha kuongezwa kwa kipindi dhaifu cha uzee, ambacho kinatoa changamoto ya kutafakari maana ya hatua hii ya maisha.  Kadhalika Papa alitafakari: "Ni thamani gani inapaswa kuhusishwa na miaka mingi ambayo mwanamume au mwanamke anaweza kuishi katika hali ya udhaifu wa kimwili au kiakili? Mtazamo wa Kikristo wa kuishi wakati huu ni upi? Tunawezaje kutangaza kwamba maisha ya mwanadamu huhifadhi 'heshima yake isiyo na kikomo' kila wakati, katika kila hatua?"

Uzee ni wakati wa neema, wa kuishi katika sala, huduma, huruma

Papa Leo alisema,  tafakari ambazo washiriki wa Mkutano wanafanya zinaweza kusaidia kujibu maswali haya na mengine. Pia alisisitiza kwamba udhaifu una thamani ya kiroho na ya kijamii, akitukumbusha kwamba tunategemeana na tunahitaji Mungu, na akarudia Papa Francisko katika kuuelezea kama "magisterium" ambayo ina mengi ya kufundisha ubinadamu leo hii. Uzee, ni wakati wa neema, wa kuishi katika sala, huduma, huruma, na katika kumbukumbu iliyohifadhiwa na kupitishwa: baraka kwa vizazi vijavyo.

Hata kama jamii tunamoishi inatawaliwa na mantiki ya utendaji na ushindani, ambapo nguvu huchukuliwa kama onyesho la nguvu na huelekea kupungua hadi kutawala, alisema Kanisa linaendelea kupendekeza ujumbe wa Injili wa upole, unyenyekevu, na amani. Wazee wa jamii zetu, kupitia uzoefu wao na hekima yao ya maisha, ndio mashahidi wa kwanza na wenye mamlaka zaidi wa maono haya ya Kikristo ya ubinadamu." Papa Leo XIV alibanisha  matumaini yake kwamba kazi yao inaweza kuchangia kukuza, kwa wazee na wakati wenye baraka wa uzee, mitazamo mipya na kuamsha katika wale waliozeeka, jukumu la kusambaza maadili yenye afya na imara kwa vizazi vijavyo. Hatimaye, Papa Leo XIV aliwaombe kwa  maombezi ya mama ya Bikira Maria na kwa moyo wote akawapa kila mtu Baraka yake ya Kitume.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

10 Juni 2026, 13:27