Tafuta

Tetemeko la ardhi nchini Venezuela. Tetemeko la ardhi nchini Venezuela.  (AFP or licensors)

Papa Leo XIV atuma msaada wa Euro 100elfu kufuatia Tetemeko la Ardhi,Venezuela

Kiasi hicho kimetolewa kwa ajilinya Kanisa la nchi hiyo ya Amerika Kusini kupitia Ofisi ya Misaada ya Papa.Jimbo la pwani la La Guaira ndilo lililoathiriwa zaidi,lililoelezewa na Rais Rodríguez kama "eneo la maafa."Askofu Pablo Modesto González Pérez:"Hatuna umeme na sote tumeathiriwa.Kuta nyingi katika seminari zimeanguka."

Vatican News

Habari hizo zilifika alasiri ya tarehe Juni 25 Juni 2026 kuwa Baba Mtakatifu Leo XIV  kupitia Ofisi ya Baraza la Kipapa la Upendo, walituma msaada wa awali nchini Venezuela, ambayo ilikumbwa na matetemeko makubwa ya ardhi usiku kati ya 24 na 25 Juni. MMsaada wa Papa Leo ni jumla ya euro 100,000, zilizoamuliwa baada ya majadiliano na balozi wa Vatican nchi hiyo, Askofu mkuu Alberto Ortega Martín, wa Midila, na Askofu Mkuu wa Caracas, Raúl Biord Castillo.

Hata hivyo, umakini wa mara kwa mara utasaidia mahitaji ya watu wa Venezuela, ambayo, katika siku zijazo, yatashughulikiwa, kama ilivyoelekezwa na Kanisa hilo mahalia. Ripoti za tetemeko la ardhi zinaonesha kwamba La Guaira ilikuwa eneo lililoathiriwa zaidi nchini. Rais wa mpito Delcy Rodríguez alitoa kauli hii alipotangaza hali ya hatari ya kitaifa kufuatia matetemeko mawili ya nguvu, yenye ukubwa wa 7.2 na 7.5, yaliyopiga kaskazini magharibi mwa nchi. Asubuhi Juni 25 asubuhi, idadi ya vifo imesasishwa: watu 164 wamekufa na 971 wamejeruhiwa, lakini mamlaka imeonya kwamba idadi ya waathiriwa inaweza kuongezeka huku shughuli za uokoaji zikiendelea. Kulingana na idadi mpya iliyotolewa na mamlaka jioni hii, watu 35,848 hawajulikani walipo, huku watu 2,570 wakiokolewa na timu za uokoaji.

Hali huko La Guaira

Hali mbaya zaidi iko katika jimbo la pwani la La Guaira, lililoelezewa na Rodríguez kama "eneo la maafa." Hapa, kulingana na serikali, majengo kadhaa yameanguka, na shughuli kali zinaendelea kutafuta manusura chini ya vifusi. Uharibifu pia umeripotiwa katika mji mkuu, Caracas, ambapo wazima moto na maafisa wa polisi wanafanya kazi katika maeneo yaliyoathiriwa. Mitetemeko hiyo pia ilihisiwa nchini Colombia na kufuatiwa na angalau mitetemeko ishirini ya chini ya nguvu. Kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani, kitovu cha tetemeko la ardhi kilikuwa takriban kilomita 28 kaskazini magharibi mwa Montalbán, kwa kina cha kilomita 13.2.

Katika saa za kwanza baada ya tetemeko la ardhi, mamlaka za mitaa zilithibitisha vifo vinne nje kidogo ya Caracas, kati ya Baruta na Los Salias, kabla ya idadi ya vifo vya kitaifa kusasishwa.Kanisa limekuwa likihama tangu saa za kwanza baada ya tetemeko hilo. "Tunafanya kile ambacho tumekuwa tukifanya wakati wa mgogoro: kufungua milango yetu, kuandamana na wale ambao wamepoteza kila kitu, na kuleta matumaini ambapo hofu imeenea." "Tunashukuru sana," alisema Marco Mencaglia, mkurugenzi wa mipango ya Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji (ACN)la Kimataifa, akiongeza kuwa Mfuko huo utaendelea kusaidia jamii zilizoathiriwa "kwa msaada na maombi yetu."

Caritas Internationalis ilitangaza kutoa euro 100,000

Caritas Internationalis pia ilitangaza mgao wa €100,000 kwa ajili ya huduma ya kwanza, kwa ushirikiano na Caritas Venezuela na mtandao wake wa takriban watu 30,000 wa kujitolea. Akiwa uwanjani, Askofu Mkuu wa Caracas, Raúl Biord Castillo, akirudi kutoka ziara ya shambani, aliripoti kwamba "Parokia nyingi zina uharibifu mkubwa wa kimuundo," pamoja na kanisa kuu na takriban makanisa kumi na mawili yaliyoharibiwa. "Parokia nyingi zimewakaribisha watu kulala katika vituo vyao. Tayari tumeanzisha mtandao wa mshikamano kupitia mashirika ya parokia ya Caritas," alielezea askofu huyo.

Askofu Mkuu wa Caracas pia alisisitiza kwamba idadi ya watu ingekuwa mbaya zaidi, lakini kwamba "namshukuru Mungu ilikuwa likizo. Kama ingekuwa siku ya juma, huku shule, ofisi, na maduka yakiwa wazi, idadi ya vifo ingekuwa kubwa zaidi." Hali bado ni mbaya zaidi katika dayosisi ya La Guaira, ambapo askofu, Monsignor Pablo Modesto González Pérez, alisema: "Hatuna umeme na sote tumeathiriwa. Kuta nyingi katika seminari zimeanguka." Askofu Mkuu Pérez aliongeza kuwa makanisa kadhaa yamepata uharibifu mkubwa.

Akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican, Askofu Mkuu Carlos Cabezas, Askofu wa Dayosisi ya Ciudad Guayana, pia alirudia: "Hali ni mbaya, haswa katika miji ya kati ya nchi - Caracas, La Guaira, Valencia, na Maracai - ambapo majengo na miundo mingi imeanguka na kubomoka, na kusababisha vifo na majeruhi zaidi. Zaidi ya yote, tunaomba maombi mengi kwa ajili ya Venezuela, na mshikamano kutoka nchi zingine pia, wakati huu wa mateso makubwa kwa watu wetu, haswa katika miji hii ambapo tetemeko la ardhi lilihisiwa kwa nguvu zaidi."

Misaada na mshikamano kutoka kote ulimwenguni

Wakati huo huo, matoleo ya misaada yanaongezeka kimataifa. Marekani imetangaza kupeleka mara moja timu za utafutaji na uokoaji, rasilimali za matibabu, na usaidizi wa kibinadamu. Rodríguez alimshukuru Rais Donald Trump, ambaye yuko katika "mawasiliano ya kudumu" na serikali ya Venezuela. Mshikamano pia ulifika kutoka Kolombia, Cuba, ambayo iliwahamasisha madaktari wake waliokuwepo uwanjani, na nchi zingine kadhaa za Amerika, ikiwa ni pamoja na Ekuado na Uruguay, pamoja na India na Italia, ambazo zilionyesha nia yao ya kushirikiana katika shughuli za dharura.

Tuko wapi sasa Venezuela? Wakazi wa eneo hilo wanaendeleaje leo? Miezi mitano baada ya shambulio la Marekani, dhidi ya hali ya mvutano mpya na Cuba, wakati huo huo, leo tu, gazeti la Uingereza la Financial Times lilifichua kwamba Venezuela inajiandaa kuzindua kile kinachoweza kuwa marekebisho makubwa zaidi ya deni la serikali kuwahi kufanywa. Kulingana na gazeti hilo, katika juma zijazo serikali itafichua deni la umma la takriban dola bilioni 240, zaidi ya makadirio ya awali, kwa lengo la kufikia makubaliano na wadai ifikapo mwisho wa mwaka na kuirudisha nchi katika masoko ya kimataifa baada ya karibu muongo mmoja wa kutengwa kifedha. Mzigo wa kifedha ambao, unakabiliwa na janga la asili na hali ngumu ya kisiasa na kijamii, unaweza kuwa wa kukandamiza zaidi.

Sasisho la mwisho ni saa 2.40 usiku tarehe 25 Juni 2026 na Angella Rwezaula.

25 Juni 2026, 14:36