2026.06.27 Mkutano Mkuu Maalum wa Makardinali. 2026.06.27 Mkutano Mkuu Maalum wa Makardinali.  (@Vatican Media)

Mkutano wa Makardinali umehitimisha sehemu III:Tafakari kuhusu mgawanyiko leo hii!

Majadiliano ya asubuhi Juni 27 katika Ukumbi wa Paulo VI ya Makardinali yalikuwa kufanya wito wa amani wa Papa uwe na ufanisi zaidi,ukizingatia katika majimbo na tafakari kuhusu ukosefu unaoongezeka wa mahusiano yenye maana na ubinafsi uliozidi katika jamii.Papa Leo XIV alihudhuria kikao cha ufunguzi na akarudi kabla ya mawasilisho ya kikundi,baadaye aliongoza sala ya kufunga.

Vatican News

Kumuunga mkono Papa katika wito wake wa amani, na kuwafanya wawe na ufanisi zaidi kwa kuwashirikisha katika majimbo na maeneo yao. Tafakari  ya migawanyiko mikubwa ya wakati wetu, ambayo huchochea na ukosefu wa maana na mahusiano yenye maana na kukuza ubinafsi uliofadhaika, unaozidishwa zaidi na maendeleo yenye matatizo zaidi katika akili unde. Badala yake, kuhamasisha manufaa ya wote na Injili inayoweza kuponya majeraha ya wakati huu, na kuwafanya Wakristo  wasiwe  watazamaji wa uharibifu wa kijamii, bali wasanifu wenye busara wanaojenga upya mji wa wote.

Hizi ni baadhi ya mada zilizoibuka wakati wa kikao cha tatu cha Mkutano Mkuu Maalum wa Makardinali , kilichofanyika asubuhi ya Jumamosi tarehe 27 Juni 2026, katika Ukumbi wa Paulo VI, baada ya Misa iliyoongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Mkuu wa Baraza la  Makardinali. Papa, aliyekuwepo mwanzoni mwa kikao, alirudi kabla ya mawasilisho ya kikundi na kuhitimisha kazi ya asubuhi kwa kuongoza sala ya Malaika wa Bwana.


Kupotea kwa utambulisho na ubinafsi ulioenea kuchambuliwa

Mratibu wa Kikao hicho alikuwa ni Kardinali Protase Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Tanzania alitoa shukrani zake, kwa niaba ya wote Papa Leo XIV, kwa maneno yake ya kuunga mkono wito wake wa amani na kuwasihi Makardinali kuufanya uwe wenye ufanisi zaidi, wakichukua jukumu kwa ajili yao katika majimbo na maeneo yao, "ili wito wa pamoja uweze kutolewa ambao unaipatia nguvu zaidi ahadi hii ya pamoja,"alisema Kardinali kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican.

Na kufuatia uwasilishaji wa Kardinali Stephen Brislin, Askofu Mkuu wa Jiji la Johannesburg, nchini Afrika Kusini  vikundi kumi na moja viliripoti kwenye Ukumbi, vikizingatia tafakari zao kuhusu mgawanyiko unaoenea katika ulimwengu mamboleo. Iliakisiwa  miongoni mwa mambo mengine, jinsi ya kupoteza utambulisho kunavyoweza kukuza mtazamo wa kikabila. Makardinali pia walikubaliana kwamba ubinafsi ulioenea huchochea udanganyifu kwamba wengine wapo kwa ajili ya mafanikio yetu na kuhoji jinsi akili unde  inaweza kuelekezwa kwa manufaa ya ubinadamu, bila kupunguza mtu binafsi katika idadi na takwimu."


Thamani ya Manufaa ya Wote

Makundi mengi pia yalisisitiza thamani ya manufaa ya wote, ambayo siasa mara nyingi hushindwa kuyatafuta, yakisisitiza jinsi yanavyotokana na imani na kupelekea ubinadamu kushinda kila mipaka, ya kwanza inayotupeleka mbali zaidi ya sisi wenyewe, kuishi kwa mshikamano na maskini, kama jibu la ubinafsi, kuishi kikamilifu Ukatoliki." Makardinali kisha walirudia katika jukumu la siasa katika kutumia mafundisho ya kijamii ya Kanisa kama dawa dhidi ya migawanyiko. Makundi kadhaa pia yalisisitiza thamani ya Sinodi kama njia ya kusikiliza, mazungumzo, na uwajibikaji wa kanisa. Baada ya mawasilisho, nafasi ilitolewa kuingilia kati na makardinali kadhaa, ambao walizungumzia mada zilizojitokeza wakati wa kikao kwa njia ya kibinafsi zaidi. Wengine walimshukuru Papa Leo XIV kwa ziara zake za hivi karibuni za kitume na kujitolea kwake mara kwa mara kwa ajili ya  amani.

Mada na mratibu Kard Rugambwa

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

27 Juni 2026, 16:25