Kard Ryś: Kanisa lazima liponye majeraha ya wanadamu katika dunia ya migogoro
Daniele Piccini na Angella Rwezaula
Ulimwengu ambao tumeitwa kutangaza Injili si mahali, bali ni mtu. Hakika, wa watu wawili. Mmoja ni Msamaria Mwema, mhusika mkuu wa mfano katika Injili ya Luka. Mwingine ni jirani yake aliyepata majeraha na mgeni aliyesimama kumtunza. Wote wa wili wanatuelezea kwa undani, na kutokana na wote wawili, tuna kitu cha kujifunza: majeraha, upweke, mateso, na sababu zake kwa upande mmoja; na kwa upande mwingine, umakini katika kuinama ili kutunza. Hiki kilikuwa kiini cha tafakari ya kibiblia iliyotolewa asubuhi ya IJumaa tarehe 26 Juni 2026, na Kardinali Grzegorz Ryś, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kraków, mbele ya Papa Leo XIV na Makardinali 180 , wakati wa shughuli za Mkutano Mkuu Maalum katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican wenye kichwa: "Tunaitwa Kutangaza Injili Katika Ulimwengu Gani?"
Mhathiriwa wa Majambazi ni taswira ya Mwanadamu wa Kisasa
Kardinali alipata msukumo kutoka katika hotuba ya kuhitimisha Mtaguso wa II wa Vatican ya Mtakatifu Paulo VI. Akitaka kuelezea "ulimwengu wa kisasa," Papa Montini wa wakati huo alisema kwamba: "historia ya kale ya Msamaria" ilikuwa mfano na dhana. Hivyo, mwelekeo wa kidunia umepunguzwa kwa mtu binafsi: "Tuwafikirie wanaume na wanawake halisi, tukikumbuka kwamba wote wawili ni waumbaji wenza wa ulimwengu na wanawajibika kwa ajili yake, na kwamba hatimaye wao ndio 'njia ya kwanza na ya msingi wa Kanisa." Kadhalika Askofu Mkuu wa Karakow pia alielezea akinukuu waraka wa Mtakatifu Yohane Paulo II wa Redemptor hominis yaani, "Mkombozi wa Mwanadamu"(ambao ulikuwa ni waraka wa kwanza uliochapishwa tarehe 4 Machi 1979, Miezi mitano baada ya kutachuguliwa kwake.)
Uso wa kwanza wa mwanadamu, uliosimuliwa na mwinjili Luka, unashuka kutoka Yerusalemu hadi Yeriko na kuwa "mhathiriwa wa majambazi." Kuwa mwathirika wa vurugu," Kardinali wa Kipoland alisisitiza, "ni maelezo ya karibu sisi sote leo, tunaishi katika ulimwengu mkuu uliokumbwa na vita 32 vinavyoendelea. Uchokozi huu pia unaathiri ulimwengu mdogo wa leo, hii ambapo watoto na vijana wanazidi kuwa waathiriwa wa vurugu shuleni kutoka kwa wenzao. Unyanyasaji huanza kwa lugha ya ukali na kisha huendelea hadi "mauaji" na "kujiua." Mwanadamu pia "huibiwa", "huvuliwa nguo", "hupunguzwa hadi utumwa." Hali ya kupoteza heshima ambayo inaweza kuwa halisi - katika utumwa unaoteseka, kwa mfano, na wahamiaji - au ya mfano na "ya kisasa zaidi", kama ile inayosababishwa na "dawa za kulevya, picha mbaya za mitandaoni, uraibu wa kila aina na hata teknolojia za kisasa, kama inavyofundishwa na Magnifica humanitas”.
Zaidi ya hayo, mtu katika mfano huo, Askofu Mkuu wa Krakow aliendelea kusema anapigwa na kujeruhiwa na anahitaji hospitali kambini." Kujeruhiwa ni uchunguzi wa kawaida zaidi leo hii kwa sababu: baadhi ya majeraha haya yanaonekana ya kimwili, kisaikolojia, au kiroho, mengine "yamefichwa sana na hayaonekani, lakini yanaamua tabia na matendo ya mtu." Mwanamume ambaye ni mwathirika wa majambazi pia ameachwa nyuma, yaani, peke yake, mwathirika, kama wanaume na wanawake wengi leo hii, wa sintofahamu. Kardinali Ryś, akimnukuu Padre Timothy Radcliffe, aliakisi utata wa jamii ambapo njia za mawasiliano za kisasa" zinapatikana, huku mwanadamu leo akiteseka na thoruba ya upweke." Ni nusu mfu au anaishi pembezoni mwa maisha, na hatimaye anatembea katika mwelekeo ulio kinyume na hekalu, yaani, mbali na Yerusalemu: picha ya jamii zetu za Magharibi zilizotawaliwa na dini au ya upotoshaji wa dini, unaolenga kukuza mawazo na matendo ambayo ni mageni kabisa kwake."
Msamaria Mwema, Mfano Mwingine wa usasa
Alama nyingine ya mwanadamu wa kisasa ni "Msamaria Mwema, mgeni, hata adui, anayetendewa kwa mashaka na tahadhari kila wakati." Kardinali Ryś alisema Kristo anatualika "tujifunze kutoka kwake." "Sasa tumeitwa kujenga hospitali ya kisasa kwa ajili ya mtu aliyepigwa, kujua majeraha yake yote, lakini pia kwenda shuleni kwake na kujifunza kutoka kwake kwa unyenyekevu, tukimruhusu awe mwalimu wetu." Kardinali alisisitiza kuwa kutoka kwa mtu huyu, tunaelewa maana ya huruma, hasa huruma na upendo vinaweza kuwa mahali pa kukutania kwa Kanisa na ulimwengu. Pia anatufundisha ukaribu na huruma, ukarimu na kujitolea."
Kifungu cha mwisho cha tafakari ya Kardinali kilikuwa ni uchambuzi wa watu wawili waliowasilishwa katika Injili na kutia moyo kufanya kazi ya uinjilishaji ndani ya vipimo hivi viwili vya ubinadamu: "Nyuso mbili za mwanamume na mwanamke wa kisasa, za ulimwengu wa leo: mtu aliyekufa nusu na mgeni anayetufundisha maisha ya kweli yapo wapi! Sura zote mbili ni muhimu. Zote mbili ni za kweli sawa. Zote mbili zinadai. Katika zote mbili," Mungu anatuita kutangaza Injili duniani."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
