"Kuwa huru chini ya Neema,"ni kitabu cha kuelewa Prevost katika mazungumzo na Ulimwengu
Tiziana Campisi na Salvatore Cernuzio –Vatican.
Kurasa za Kitabu "uhuru chini ya Neema”kilichochapishwa na Nyumba ya Vitabu LEVna kuwasilishwa alasiri Mei 6, Jijini Roma katika Ukumbi Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Mababa wa Kanisa ya Augustinianum, kinafichua mawazo na hali ya kiroho ya Robert Francis Prevost. Mkusanyiko huo wa mahubiri, hotuba, barua, na jumbe kutoka miaka ambayo Papa wa sasa alikuwa Mkuu wa Awali wa Shirika la Mtakatifu Agostinian, ulihaririwa na Mababa wa Kiagostinian Rocco Ronzani, Miguel Ángel Martín Juárez, na Michael Di Gregorio ulioneshwa yaliyomo. Baada ya salamu kutoka kwa Kardinali Joseph Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha, na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, kulikuwa na maoni kutoka kwa Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin na mwandishi Maria Grazia Calandrone, yaliyoongozwa na Andrea Tornielli, Mkurugenzi wa Uhariri wa Vyombo vya Habari vya Vatican.
Farrell:Kurasa za Kutia Moyo
Kardinali Farrell alisimulia kwamba mwaka mmoja uliopita, Kardinali Prevost alishiriki chakula cha mchana cha mwisho kabla ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi(Conclave) na ndugu zake katika Curia akaelezea kwamba Kitabu “Uhuru chini ya Neema” "ni matunda ya ushirikiano wa kweli kati ya watu wengi waliofanya kazi pamoja," watawa wa Kiagostinian na watu wa kawaida, na timu ya Nyumba ya Uchapishaji vitabu ya Vatican, Kardinali huyo pia alieleza kwamba kichwa cha kitabu hicho kimechukuliwa kutoka sura ya mwisho ya Utawala wa Mtakatifu Agostino, ambapo Askofu wa Hippo anawahimiza watawa wake "kuzingatia kanuni hizi kwa upendo, kama wapenzi wa uzuri wa kiroho na kutoa" kutoka "uhai mtakatifu harufu nzuri ya Kristo, si kama watumwa chini ya sheria, bali kama watu huru chini ya neema." Pia alielezea matumaini yake kwamba kila mtu anaweza "kupata msukumo" kutoka kwa maandishi ya Prevost.
Ruffini: Maandishi "Yanayokisi"
Kwa upande wake, Dk. Ruffini alishukuru Shirika la Mtakatifu Agostino kwa kukabidhi LEV, sehemu ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano, uchapishaji wa Kitabu hicho, ambacho kinatoa fursa ya kuelewa vyema Papa Leo XIV, asili yake, na mawazo yake kabla ya kujua kwamba angekuwa Papa. Maandishi haya "yanayoakisi ambayo yanasimulia Kanisa na pia yanaweza kuzingatiwa kwa mada, "iliyoelezwa kama muhimu na vyombo vya habari vya Italia," yanaakisi dhana ya "mamlaka" ya Mkuu wa Zamani wa wakati huo. Haya yote, katika ulimwengu "uliojaa udikteta na nguvu, hutusaidia kuelewa jinsi Papa anavyoongoza na atakavyoongoza Kanisa": kwa "sauti isiyopigwa kelele, kwa uthabiti na upole," kujenga umoja na ushirika.
Maelezo ya Kardinali Parolin
Kuhusu miaka kumi na miwili ya Prevost kama Mkuu wa Awali, kuanzia 2001 hadi 2013, Kardinali Parolin alikumbuka, miongoni mwa matukio yaliyowatofautisha, shambulio la Minara Pacha, kujiuzulu kwa Papa Benedikto XVI, na kuchaguliwa kwa Papa Francisko. Na katika kitabu hicho, aliakisi sifa za Prevost za Kiagostinian, kwamba kumtafuta Mungu na hamu ya moyo wa mwanadamu ambayo ilimfanya Papa Leo XIV wa baadaye aanze kila wakati "na ukuu wa Mungu, na uhusiano wa awali" kati ya mwanadamu na Mungu. Kwa hivyo, kwa mfano, katika hotuba huko Australia mnamo 2002, Kardinali alibainisha, Prevost aliwaalika Wakristo "kuwa 'wataalamu' katika kutafuta maana ya mwanadamu" na kutoa "ushuhuda wa wokovu na utimilifu unaotoka kwa Mungu." Lakini alibainisha kwamba waamini si "watu 'wanaomiliki' ukweli," bali "washirika katika safari, kaka na dada wanaoendelea pamoja katika matukio ya maisha." Mada, ile ya "umiliki wa ukweli," ambayo "pia ilikuwa ya thamani sana kwa Papa Francisko," Kardinali alisisitiza, akiongeza kwamba "utaftaji wa ukweli, kwa Mungu ambaye ndiye ukweli, Sio milki ya kipekee wala njia ya kipekee,” bali “safari” inayotufanya “kaka na dada katika Mmoja.”
Kugundua Imani Upya
Kitabu hiki pia kinaakisi wasiwasi wa Prevost wa “kutafuta njia zenye maana za kuwaalika watu, katika jamii iliyojaa udini, ‘kugundua upya’ uzoefu wa imani, kugusa mwelekeo wa kiroho wa maisha yao.” Na tena, katika hotuba ya 2012 huko Peru, tofauti kati ya “usekula” na kiulimwengu” iko wazi: kwanza si “mchakato hasi” wenyewe, huku ya pili, badala yake, ni kitu ambacho “hujaribu kuwatenga au kuondoa maadili ya kidini au ya kiroho yenye maana.” Kwa Katibu Mkuu wa Vatican, kuna "upatanisho wa mawazo na Joseph Ratzinger- Benedikto XVI," na kiukweli Prevost ameelezea maneno ya heshima kubwa kwake kama Mtaalimungu na msaada kamili kama Papa. Na kisha, katika kurasa za Kitabu, kuna "maneno sahihi sana, wazi sana na yenye ufasaha kuhusu jinsi Kanisa" linapaswa "kuwa duniani", na kuna "mwangwi unaorudiwa wa Mtaguso wa Pili wa Vatican na hati zake, "ambapo Papa Leo XIV anaendesha mfululizo wa Katekesi kila Jumatano."
Uzoefu wa Utume
Kardinali Parolin pia alibainisha katika mahubiri na hotuba za Prevost kuhusu "nafasi ya jumuiya ya Kanisa katika ulimwengu mamboleo." "Ni muhimu kuendelea, kujirekebisha, na kugundua upya wito wetu binafsi wa utakatifu na kuishi mwitikio wetu kwa njia inayoeleweka kwa ulimwengu wa leo huu" alisema Mkuu wa Shirika wa wakati huo mnamo 2002, katika Mkutano Mkuu wa Shirika hilo. Alisisitiza kwamba "haitoshi kurudia suluhisho za zamani." Badala yake, lazima "tuweze kuwasilisha ujumbe wa Injili kwa lugha inayoeleweka kwa utamaduni wa sasa" Kisha akawaomba wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, hasa, "wasikilize mioyo isiyotulia, wasikilize katika maombi," wawe "waangalifu kwa Neno la Mungu, na kuwasikiliza" wengine. Kwa Katibu Mkuu wa Vatican, mambo haya yanafichua "uzoefu wa umisionari" wa Prevost na "uchaguzi wake wa kushawishi, wa msimamo, ambao unatazama 'Kanisa linalotoka nje' badala ya ugomvi wa wale wanaotafuta zaidi ya yote kuhifadhi kile ambacho tayari kipo."
Umaskini wa Kiinjili
Cha kufurahisha zaidi, kwa Kardinali Parolin, ni uhusiano kati ya uinjilisti na "jinsi Wakristo," na "hasawatu wa kidini," "wanavyohusiana na kiwango cha kiuchumi." Prevost amechunguza hili mara kadhaa, kama vile mwaka wa 2006 huko Pavia, ambapo alisisitiza kwamba "umaskini usio wa haki wa ulimwengu wa leo, pamoja na kashfa ya mkusanyiko unaoongezeka wa mali na ukosefu wa mshikamano miongoni mwa Wakristo, huzuia uinjilishaji mpya." Kwa hivyo, "ni muhimu kugundua tena maana ya umaskini wa kiinjili na kutafuta njia za kisasa za kuishi kihalisi" "kiapo cha umaskini." Kuhusu uhusiano wa karibu kati ya "uchaguzi wa umaskini kama mtindo wa maisha" na "uaminifu wa ujumbe wa Kikristo," ambao Prevost ameakisi unafanana na wazo la Papa Francisko la Kanisa "maskini na kwa ajili ya maskini."
"Sio bahati mbaya kwamba hati rasmi ya kwanza ya Papa Leo XIV, ya Dilexi te, iliwekwa wakfu kwa ajili ya upendo kwa maskini," alisema Kardinali, ambaye pia alibainisha kufanana kati ya Hati ya Kiikolojia na "Kuwa huru chini ya Neema," ambacho "pia kinaturuhusu kukataa tafsiri hizo zilizofikiriwa awali na zenye kupotosha za hati ya kwanza ya Papa Leo XIV, kana kwamba Dilexi te ilikuwa maandishi yaliyotokana na urithi wa Papa Francisko pekee."
Umakini kwa walio na upendeleo mdogo
"Maneno 'maskini,' yanaonekana mara 195" katika kitabu hicho, Kardinali Parolin alibainisha, na kuongeza kwamba hii "inashuhudia bila shaka umuhimu wa umakini kwa walio na upendeleo mdogo," ikiwa ni pamoja na wahamiaji. Kuhusu wao, mnamo 2010, Prevost wa zamani aliuliza: "Je, tuko wazi, je, tunawakaribisha, je, tunatambua kwamba wao ni wana na binti za Mungu? Au tunataka tu kufunga mipaka, kufunga milango, na kuepuka mawasiliano yote?" Maneno haya ni "muhimu sana leo barani Ulaya," ambapo kuna mazungumzo ya "uhamiaji," neno "ambalo halina mengi kuhusu Mkristo kuhusu hilo," Kardinali alisema. Kwa hivyo matumaini kwamba "Ziara ijayo ya kichungaji ya Papa Leo XIV kwenda Lampedusa mnamo Julai 4" inaweza kuwa "hatua ya kukabiliana na 'utandawazi wa kutojali' ambayo ameilaani mara kwa mara.
Diplomasia, ushirikiano wa pande nyingi, mazungumzo
Hatimaye, haki, amani, "kilio cha maskini," na "taabu ya mamilioni ya wanadamu" yalikuwa mada zingine ambazo Prevost alizizungumzia katika hotuba yake huko Australia mwaka wa 2002, na katika maandishi yaliyotolewa Roma mwaka huo huo. ambapo alithibitisha kwamba "haki ni sehemu ya msingi ya ujumbe wa Injili" na kwamba "juhudi nzito, zenye ufanisi, na zilizopangwa zinahitajika ili kukuza haki na kufikia amani." Kardinali Parolin, kwa Papa maneno haya "yana changamoto kwa kila mtu, hasa wale wanaohusika katika siasa na jamii wenye nafasi za uwajibikaji," kwa sababu "amani haihitaji tu mawazo ya uchamungu tu, bali kujitolea kwa uzito, kwa ufanisi, na kupangwa', ambako kiukweli inamaanisha 'diplomasia, ushirikiano wa pande nyingi na mazungumzo.'"
Calandrone:Maneno Sahihi Wakati wa Mgogoro
Maria Grazia Calandrone, mshairi, mwandishi wa habari, na mwandishi wa tamthilia, alitoa hotuba ya shauku na mada. Alilenga, kuanzia na tafakari za Prevost katika kitabu juu ya matatizo ya umaskini, lugha, mawasiliano, au, kwa usahihi zaidi, ukosefu wa mawasiliano, katika enzi kama ya leo ambapo msemo unaojirudia zaidi ni "Sina muda." Maneno ya Papa wa wakati ujao yanashughulikia masuala haya na, kulingana na Calandrone, ni "maneno yanayofaa kwa wakati wa shida, yakituhimiza kuwa na nguvu, yaani, kutoa unabii, ambayo ina maana ya maono ya sasa na ya baadaye, kutoka katika mtazamo wa roho ya umisionari."
Upweke wa vijana
Mshairi pia alilinganisha imani na ushairi, "lugha" ambayo inaweza kuwa na "kazi ya kijamii." Sio "kimbilio la kificho," "ambapo unaweza kukimbilia kutoka katika ubaya wa ulimwengu," bali ni msaada wa "mambo ya ndani" ambayo, kama Padre Prevost wa wakati huo alivyosema, "hutajirisha"mbele ya mambo ya juujuu ambayo "husababisha umaskini." Neno la imani, kama ushairi, "lazima liletwe katika historia halisi ya mwanadamu," Calandrone aliendelea. Hasa kwa vijana ambao, kwa ujio wa mitandao ya kijamii kama TikTok, "wanaishi katika wakati wa sasa wa milele" na katika "kuridhika kwa haraka na bila wakati ujao." "Hakuna tena uvumilivu, kusubiri, au uwezo wa kujaza uchovu kwa kitendo cha ubunifu cha mtu binafsi. Kimsingi, hakuna wakati wa kuchunguza matamanio ya mtu, kuwa peke yake na nafsi yake. Vijana wako peke yao kila wakati, lakini hawako peke yao kamwe," mzungumzaji aliendelea. Kwa maana hiyo, aliongeza, akinukuu tafakari ya Prevost, "lazima iwe ni onesho la njia tofauti ya kuwa duniani." Suluhisho moja ni ushuhuda, kisha maisha ya kijumuiya: "Mfano halisi wa uwezekano mwingine wa maisha duniani, ni ule ambao si upweke na mapambano kwa ajili ya manufaa ya mtu binafsi." "Katika ulimwengu uliojaa upweke," mwandishi alihitimisha, "maisha ya kupatikana kwa wengine yanaweza kuwa mfano wa kuvutia."
Imetafsiriwa na Angella Rwezaula.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.