Hati ya Vatican ya"kuishi ikolojia fungamani katika familia"
Vatican News
"Ikolojia fungamani katika Maisha ya Familia" ni jina la hati iliyoandaliwa kwa pamoja na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu (Dssui) na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha (Dlfv) ili "kusambaza utunzaji wa Uumbaji na maisha ya kibinadamu ndani ya familia." Taarifa inaarifu kwamba Wataalimungu, washauri, na wanandoa walihusika katika kuandaa hati hiyo, iliyoundwa ili kujibu wito wa Papa Francisko na Papa Leo XIV wa kusikiliza kilio cha maskini na Dunia na kutoa jibu halisi, kwa kutumia mafundisho ya Wosia wa Kitume wa baada ya Sinodi, wa "Amoris Laetitia" na hati ya "Laudato si'."
Ardhi yenye rutuba kwa Jamii
"Maadili yanayochukua umbo na kukua ndani ya familia yanaunda ardhi yenye rutuba ambayo maisha ya jamii huchipuka. Kwa hivyo, familia ni msingi wa kuhamasisha na kusambaza thamani ya kutunza nyumba yetu ya pamoja na kwa kila mtu," wanaandika Makardinali Michael Czerny na Kevin Farrell, Wenyeviti wa Mabaraza mawili, katika uwasilishaji wao. "Familia nyingi," Makardinali hao wawili wanaendelea, "tayari wanaishi wito huu kwa moyo wazi na kwa tumaini ambalo ni Kristo Yesu. Katika familia, tunajifunza kujitoa, uvumilivu, na kujitolea, kukaribisha na kulinda maisha, ili yaweze kustawi na kukua kikamilifu; pamoja na kukamilishana na kukubaliana, kubadilishana vizazi na mshikamano na familia zingine, pamoja na uwasilishaji wa maarifa na utamaduni.
Maarifa na Tafakari
Hati hii inatoa maarifa muhimu kwa familia, vikundi vya makanisa, na wasomaji binafsi ili kushughulikia changamoto za mazingira ya sasa na kuhamasisha maendeleo fungamani ya kila mtu. Sehemu ya kwanza inakusanya dhana za msingi kulingana na maandishi muhimu zaidi ya Papa Francisko; Sura ya pili ina sura zenye mada zinazoakisi malengo saba yaliyotolewa kutoka Laudato si': kusikiliza kilio cha dunia, cha maskini na walio katika mazingira magumu, kukuza uchumi wa ikolojia, kupitisha mitindo wa maisha yanayofaa, ikolojia na elimu shirikishi, roho ya ikolojia kutoka katika mtazamo wa familia, na familia zinazoshiriki katika maisha ya jamii.
Hati hiyo inapatikana bila malipo ambapo kila sura inaelezea maelezo, matokeo, maswali, na vitendo halisi
"Ikolojia Fungamani ya Maisha ya Familia" inapatikana bila malipo katika lugha tano kwenye tovuti rasmi za Mabaraza mawili:
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.