Tafuta

2026.05.11a Askofu Sommertag;Kardinali Gomes Furtado;Askofu Mkuu Galagher,Askofu Mendes Tavares,Askofu dos Santos Lopes Fortes 2026.05.11a Askofu Sommertag;Kardinali Gomes Furtado;Askofu Mkuu Galagher,Askofu Mendes Tavares,Askofu dos Santos Lopes Fortes 

Ask.Mkuu Gallagher,Cape Verde:"Amani ya kweli hutoka katika udugu"

Katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Cape Verde,Askofu Mkuu,Gallagher,Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa,aliadhimisha Misa Mei 10,katika Parokia ya Mama Yetu wa Neema,huko Praia.Askofu Mkuu alisisitiza kuwa usalama hautokani na kujilinda,bali unatokana na kumwamini Mungu na upendo wake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa  Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, katika Misa iliyoadhimishwa Dominika tarehe 10  Mei 2026, katika Kanisa la Mama Yetu wa Neema(Nossa Senhora da Graça,) huko Praia, nchini Cape Verde, kwa kutazama hali ya Ulimwengu uliojaa vurugu alisema “Ili kufikia amani ya kweli ambayo ulimwengu unahitaji sana, ni lazima tukumbuke kwamba sisi ni watoto wa Baba mmoja na ndugu katika ubinadamu: Wazo kwamba tutakuwa salama zaidi kadri tunavyozidi kuwa na silaha ni la uongo, kwa sababu ni kwa uwezo wa Mungu pekee tunaweza kuwa salama kweli.

Miaka 50 ya Uhusiano wa kidiplomaisa kati ya Vatican Na Capo Verde

Askofu Mkuu anatembelea Jamhuri ya kisiwa cha Afrika hadi Mei 14, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Nchi hizo mbili. Akifuatilia historia ya mahusiano kati ya Cape Verde na Vatican, katika mahubiri yake, Askofu Mkuu alikumbuka makubaliano ya pande mbili yaliyosainiwa mwaka 2013, yakifunga ushirikiano wa muda mrefu kati Vatican na Kanisa mahalia hasa leo katika nyanja za elimu na ustawi wa jamii. Ingawa mazungumzo yanayoendelea kwa ajili ya utekelezaji wake kamili, hakika yatachangia kuimarisha zaidi hadhi na uwepo wa Kanisa katika jamii ya Cape Verde," alisema.

Vifungo vunavyoainishwa na nchi mbili

Askofu Mkuu Gallagher alisisitiza haki na wajibu wa Kanisa wa kutoa hukumu ya kimaadili wakati haki za msingi na utu wa binadamu ziko hatarini," hasa kwa kuzingatia mchango mkubwa ambao limetoa kwa maendeleo ya taifa,  si tu katika miongo ya hivi karibuni, bali kwa karne nyingi, "kwani Jimbo la Santiago ya  Cape Verde itasherehekea miaka 500 yake hivi karibuni." Kisha  Askofu Mkuu alitaja matendo mengi ya upendo ambayo kupitia kwayo Kanisa huwajali walio dhaifu zaidi kwa mujibu wa utume wa Kristo na habari njema ya utu wa kila mtu, hasa maskini. Dhamira inayoweza kufikiwa ndani ya "uhuru unaohakikishwa na Serikali," aliongeza, huku akitoa "shukrani za dhati" kwa mamlaka ya nchi kwa "ushirikiano wao mzuri" kwa manufaa yaJumumuiya mahalia kwa ujumla. Pia aliakisi "vifungo vya kudumu" kati ya nchi zote mbili vilivyoainishwa na "heshima ya pande zote" na kuhakikisha "ushirikiano mzuri": lengo kuu linabaki kuwa "huduma ya mwanadamu, ili waweze kutekeleza haki zao kikamilifu na kutimiza majukumu yao ipasavyo."

Kanisa linaitikia Upendo katika huduma mbali mbali za kijamii

Akitoa maoni yake kuhusu usomaji wa siku hiyo kutoka Injili ya Yohane (14:15-2) kuhusu hotuba ya Yesu kwa wanafunzi wake wakati wa Karamu ya Mwisho, Askofu Mkuu Gallagher alisisitiza jinsi upendo huzaa upendo na kufuata amri ni jibu la upendo wa bure wa Mungu, ambao humiminwa "juu yetu bila kujali udhaifu wetu, mapungufu, na dhambi zetu. Vile vile, aliendelea, "Upendo wa Mungu hutuunganisha katika kifungo cha uaminifu, urafiki na ushirika," na akifafanua Mwalimu wa  Kanisa Mtakatifu John Henry Newman, Askofu Mkuu Gallagher alihitimisha kwamba "Mungu ni upendo na ametuumba kwa mfano na sura yake; kwa hivyo, kupenda ni sehemu muhimu ya asili yetu." Kanisa linaitikia upendo huu "kupitia utume wake, kwanza kabisa kwa kutangaza ukweli wa Injili na kisha kupitia matendo yake," hasa "katika nyanja za elimu, huduma za afya, na huduma za kijamii na si kwa faida ya muda, bali  kwa manufaa ya wanadamu wote."

Bwana alisema hatatuacha peke yetu au yatima

Kwa kujali Maendeleo Fungamani ya  binadamu," Kanisa linafundisha kanuni ya "mwisho wa ulimwengu wote" wa mali na linathibitisha haki ya kila mtu ya kupata "mali muhimu kwa maendeleo yao: si "makubaliano bali haki ya asili, yenye mizizi katika utu wa binadamu, ambayo hutangulia mfumo wowote wa kisheria, ambao utekelezaji wake unahitaji utaratibu wa haki, uliojengwa juu ya kanuni za pamoja katika ngazi za kitaifa na kimataifa." Ikiwa katika uumbaji na mwili Mungu alifunua upendo wake, katika kifo na ufufuko wa Kristo alitoa uthibitisho mkuu wake: aliitwa kuishi katika upendo, hii inaoneshwa kikamilifu katika utii. Na ingawa Bwana hakuwahi kuzungumzia maisha bila changamoto na magumu, pia alituhakikishia kwamba hatatuacha peke yetu au yatima, na akaahidi zawadi ya amani, ambayo sio tu kutokuwepo kwa migogoro au matatizo, lakini, ukamilifu wa maisha na wema,"Askofu Mkuu Gallagher alihitimisha.

GALLAGHER CAPE VERDE

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

11 Mei 2026, 15:59