Tafuta

Watu wa Asili. Watu wa Asili.  (Renan Dantas)

Vatican,Jukwaa la 25 la watu Asili:Watu wa Asili wana haki,bila ubaguzi,kuboresha hali ya kiuchumi na kijamii

Kukuza afya si suala la kiufundi au la kimwili tu;ni sharti kubwa la kimaadili linalotokana na hadhi isiyoweza kupuuzwa ya kila mwanadamu,aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu.Watu wa Asili wana haki,bila ubaguzi,ya kuboresha hali ya kiuchumi na kijamii na kupata huduma za kijamii na za afya.Haya yalisemwa na Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa huko New York,Aprili 20 katika Jukwaa la 25 kuhusu Watu wa Asili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwakilishi wa kudumu wa Vatican alishirikisha hotuba yake katika Ufunguzi wa Kikao cha 25 cha "Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa" kuhusu Masuala ya Watu wa Asili kwa mada: “Kuhakikisha afya ya watu wa kiasili, ikiwa ni katika muktadha wa migogoro, ”Jumatatu tarehe 20 Aprili 2026 huko New York, Marekani. Mwakilishi wa Vatican akianza hotuba yake alisema kuwa,  “Vatican inakaribisha umakini wa wakati unaofaa wa Kikao hiki cha 25 cha Jukwaa kuhusu afya ya Watu wa Asili, hasa kwa katika muktdha wa athari mbaya za migogoro.”

Watu wa Asili wana haki,bila ubaguzi wa kuboresha hali ya kiuchumi na kijamii 

“Kukuza afya si suala la kiufundi au la kimwili tu, alisisitiza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican bali,  "ni sharti kubwa la kimaadili linalotokana na hadhi isiyoweza kupuuzwa ya kila mwanadamu, aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu.” Kwa hivyo, “haki ya afya lazima ieleweke kwa maana yake kamili - kimwili, kiakili, kiutamaduni, na kiroho.” Watu wa Asili “wana haki, bila ubaguzi, ya kuboresha hali ya kiuchumi na kijamii, ikiwa ni pamoja na afya na usafi wa mazingira, kushiriki katika kuandaa na kubaini programu za afya zinazowahusu, kudumisha dawa zao za jadi na kupata huduma za kijamii na huduma za afya.”

Huduma za afya zinazozingatia utamaduni

Katika suala hilo, Vatican, inasisitiza hitaji la hatua madhubuti za kuboresha hali ya kiuchumi na kijamii ya Watu wa Asili, hasa wazee, wanawake, watoto na vijana, na watu wenye ulemavu. Serikali zinapaswa pia kuondoa vikwazo vya kiutamaduni, kiuchumi, lugha na taarifa ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya. Wakati huo huo kuna haja maalum ya huduma za afya zinazozingatia utamaduni. Utekelezaji wa mifumo ya afya inayopuuza utu na haki za Watu Asilia, una hatari ya kuwa aina mpya ya ukoloni.

Majeraha,magonjwa ya kuambukiza, utapiamlo na hukatisha uhusiano 

Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican, aidha alibainisha kwamba “Katika hali za migogoro ya silaha, Watu wa Asili mara nyingi huwa miongoni mwa walio hatarini zaidi na walioathiriwa kwa kiasi kikubwa. Kwa masikitiko, vurugu kama hizo zinaweza kusababisha uharibifu wa miundombinu ya afya, kuhamisha familia, kuweka jamii katika hatari ya kupata majeraha, magonjwa ya kuambukiza, na utapiamlo, na kukatisha uhusiano muhimu kati ya watu na ardhi unaomwilisha mwili na roho.

"Katika mkutano wa mataifa, watu wa asili lazima watoe utajiri wao"

Sheria ya kimataifa ya kibinadamu lazima izingatiwe kwa makini; mashambulizi ya makusudi dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na Jumuiya za Watu Asili na kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu kamwe haviwezi kuhalalishwa. Watu wa Asili,  lazima watoe utajiri wao wa kibinadamu,kiutamaduni na Kikristo,kwa ujasiri na uhuru," Papa Leo XIV anathibitisha kuwa: "Katika Mkutano wa Mataifa, Watu wa Asili,  lazima watoe utajiri wao wa kibinadamu, kiutamaduni na Kikristo, kwa ujasiri na kwa uhuru." Jukwaa hili na lichangie katika vitendo halisi vinavyoheshimu utu uliotolewa na Mungu wa kila mtu na kukuza manufaa ya wote."

MWAKILISHI WA VATICAN, NEW YORK

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

22 Aprili 2026, 10:45