Tafuta

2026.04.20 Teilhard-De-Chardin 2026.04.20 Teilhard-De-Chardin 

Teilhard de Chardin na kina cha fumbo katika maada

Kuanzia utotoni akiwa na uzoefu wa udhaifu hadi wito wake wa pande mbili kama mwanasayansi na Padre,safari ya Pierre Teilhard de Chardin inasimuliwa katika makala iliyowasilishwa Jumatatu,Aprili 20,katika Maktaba ya Filamu ya Vatican.Kupitia utafiti,imani,na mawazo ya kinabii kama vile ulimwengu mpya,sura hiyo inajitokeza ya mtu aliyemtafuta Mungu katika moyo wa mageuko.

Na Silvia Guidi

Mtoto mdogo wa kiume na mama yake wako nyumbani, wameketi mbele ya mahali pa moto; mama anakata nywele za mtoto na bila kujali anatupa nywele zake zilizosokotwa kwenye moto. Baada ya muda mfupi, kila kitu kinatoweka, kikiteketezwa na miali ya moto. Mtoto anatazama moto, anajaribu kuelewa kilichotokea, na anaanza kulia kwa kukata tamaa, hawezi kujizuia. "Lazima nilikuwa na umri wa miaka mitano au sita; labda yalikuwa machozi machungu zaidi maishani mwangu," anaandika Pierre Teilhard de Chardin, Mjesuit maarufu na mwanahistoria wa paleontolojia Sayansi ya maisha ya kihistoria kupitia visukuku,kuchambua mabaki ya wanyama na mimea ili kujenga upya mageuzi ya kibiolojia) ambaye alitoa mchango mkubwa katika ugunduzi wa Sinanthropus,(Fuvu) akisimulia kukutana kwake kwa mara ya kwanza akiwa mtoto na vifo na kutodumu kwa vitu.

Pierre mdogo ghafla anatambua kwamba mwili wake ni kitu kilichokusudiwa kuangamia, kwamba kila kitu anachokiona kinaweza kuharibiwa. Hata mandhari nzuri ya Auvergne, mahali alipozaliwa. Chuma hugeuka haraka kuwa kutu, nyuso za wale tunaowapenda zimekusudiwa kubadilika; kwa Pierre mdogo mawazo haya ni mbegu ya wito maradufu, ule wa kuhani na mwanasayansi, kama Frank na Mary Frost wanavyoelezea wanapozungumzia kuhusu makala waliyoitoa mwaka 2023, “Teilhard visionary scientist,” yaani “Mwanasayansi wa maono Teilhard “ ambayo iliwasilishwa jijini Roma alasiri tarehe 20  Aprili 2026 katika Maktaba ya Filamu ya Vatican.

"Dhana yake ya noosphere," alitarajia kwa miongo kadhaa ulimwengu uliounganishwa tunaoishi leo," walisisitiza waandaaji hao. Wakati wa ujana wake, upendo wake kwa maumbile uliongezeka, na ufahamu wake wa wito wake wa maisha ya kitawa uliongezeka. Mnamo 1899, aliingia katika Unovisi wa Kijesuit huko Provinsi ya Aix-en kwa mafunzo ambayo, kama ya wanashirika wote wa Jumuiya ya Yesu, yangedumu kwa miaka 13. Akiwa mhusika wa somo la fizikia na kemia katika chuo cha Kijesuit huko Cairo, alianza utafiti wake wa kwanza katika uwanja. "Na ilikuwa Mashariki iliyoonekana na kunywa kwa bidii mwanga wake, maumbo yake, na jangwa lake," aliandika mtu ambaye marafiki zake Waislamu walimwita Sidi Marabout, mtu aliyelindwa na Mungu, "ulimwengu bado unaumbwa, na ndani yake, Kristo anatimizwa." Nilipoelewa na kutambua neno hili, nilitafakari, na nikagundua kana kwamba kwa furaha kwamba kupitia maumbile yote nilikuwa nimezama ndani ya Mungu.

Pierre Teilhard de Chardin katika picha iliyopigwa kati ya Septemba 1908 na Julai 1912.
Pierre Teilhard de Chardin katika picha iliyopigwa kati ya Septemba 1908 na Julai 1912.

Alipowekwa wakfu wa kipadre huko Hastings mnamo 1911, aliandika: "Kwa nguvu zangu zote, kama Padre, ninataka kuwa wa kwanza kutambua jinsi ulimwengu unavyopenda, unavyofuatilia, na kuteseka... Kwa undani zaidi, mwanadamu zaidi, mtukufu zaidi kuliko mtumishi mwingine yeyote wa ulimwengu." Shauku yake ya ‘paleontolojia’ ilimpelekea kusoma  mwanasayansi mashuhuri Marcelin Boule huko Paris; Vita vya Kwanza vya Dunia, akionekana kama mtu anayebeba machela, viliimarisha imani yake na shauku yake ya maarifa, kama inavyooneshwa katika barua alizomtumia binamu yake Marguerite katika kipindi chote cha vita. Hati hiyo ya maandishi inatoa nafasi kubwa kwa wanawake walioheshimu na kuunga mkono kazi ya Padre huyo, ambaye alipenda sana maisha na maarifa.

Huko China, ambapo aliishi kwa miaka ishirini, Teilhard alifanya urafiki na mchongaji Lucile. Ili kuepuka utata na kutoelewana, katika barua nzuri kwa Lucile alielezea mwisho wa ajabu wa wito wake: "Siwezi kuwa wa mtu yeyote kabisa kwa sababu mimi si wa nafsi yangu tena." Miezi michache kabla ya kifo chake, katika barua kwa mtu anayemfahamu, aliandika: "Ikiwa sijakosea, namwomba Bwana aniruhusu nife Dominika ya Pasaka."

Mnamo tarehe 15 Machi 1954, wakati wa chakula cha mchana katika Ubalozi wa Vatican nchini Ufaransa, aliwaambia jamaa zake siri: "Ningependa kufa Dominika ya Pasaka." Mwaka uliofuata, mnamo  tarehe 10 Aprili 1955, alifariki huko New York, Marekani, baada ya kuhudhuria ibada Takatifu ya Pasaka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrick.

Makala hii imeasasishwa na saa 5.57 asubuhi,  Aprili 21, 2026 na Angella Rwezaula.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

21 Aprili 2026, 11:31