Mkutano kuhusu Papa Pio XII mnamo Mei 4 mjini Roma
Vatican News.
"Eugenio Pacelli jina la Papa Pio XII: Kati ya Jiji la Mungu na Jiji la Mwanadamu" ndiyo mada ya mkutano utakaofanyika mini Roma Jumatatu,tarehe 4 Mei 2026, katika Ukumbi wa Mapapa wa Konveti ya Mtakatifu Maria juu ya Minerva mjini Roma, saa 11:00 jioni. Mkutano huo umeandaliwa kama sehemu ya kuadhimisha miaka 150 ya kuzaliwa kwake.
Watoa mada
Chini ya urais wa Kardinali Dominique Mamberti, Mkuu wa Mahakama Kuu ya Saini ya Kitume, wazungumzaji watakuwa ni pamoja na Johan Icks, Mkurugenzi wa Kumbukumbu za Kihistoria za Kitengo cha Mahusiano na nchi cha Sekretarieti ya Vatican, ambaye atazungumzia "Eugenio Pacelli na Makubaliano"; Andrea Tornielli, Mhariri Mkuu wa Uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambaye ataakisi juu ya sura ya Kardinali Eugenio Pacelli, Katibu Mkuu wa Vatican; Stefan Heid, Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Akiolojia ya Kikristo, ambaye atawasilisha mada kuhusu: "Pio XII na uchimbaji chini yaMadhabahu ya kukiri kwa Mtakatifu Petro na Padre Fabrizio Cambi Mdominika na Mkuu wa Conveti ya Mtakatifu Maria Juu ya Minerva, ambaye atatoa muhtasari wa "Italia na Wasimamizi wake, Mtakatifu Catherine na Mtakatifu Francis, katika Majisterio ya Pio XII."
Tukio limeandaliwa na Kamati ya Papa Pacelli-Chama cha Papa Pio XII, kwa maelezo zaidi unaeweza kuwasiliana:comitatopapapacelli@gmail.com.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.