Tafuta

Tarehe 6 Mei 2026 Kikundi kipya cha Walinzi 28 wa kipapa kutoka Uswiss watakula kiapo! Tarehe 6 Mei 2026 Kikundi kipya cha Walinzi 28 wa kipapa kutoka Uswiss watakula kiapo!  (Vatican Media)

Mei 6 ni siku ya kuapishwa kwa Kikundi kipya 28 cha Walinzi wa Kipapa wa Uswiss

Sherehe hiyo muhimu ni katika mkutadha wa siku ya kukumbuka mjini Roma mnamo 1547,ambapo Walinzi 147 wa Uswisi walipoteza maisha yao wakimtetea Papa Clement VII huku 42 wakifanikiwa kumuokoa huko 'Castel Sant'Angelo."Hafla hiyo itafanyika mbele ya Papa Leo XIV saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Mtakatifu Damaso wa Jumba la Kitume ndani ya mji wa Vatican.

Vatican News.

Wahudumu wapya wa Kikosi cha Ulinzi wa Papa kutoka Uswisi wataapa kiapo "cha kumtumikia Papa kwa uaminifu, utii, na kwa heshima" mnamo tarehe 6 Mei 2026.  Ni katika fursa ya  maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari 189 kutoka Uswiss waliofariki dunia kunako mwaka 1527 wakati wa kumlinda Khalifa wa Mtakatifu Petro, wakati huo akiwa ni Papa Clement VII dhidi ya Mfalme Charles V. Tangu wakati huo, hawa wamekuwa ni walinzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Kwa njia hiyo walinzi wapya 28 watakula kiapo hicho katika Sherehe hiyo itakayofanyika saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Mtakatifu Damaso  katika Jumba la Kitume mjini Vatican; Ikiwa hali ya hewa itakuwa siyo nzuri, hafla hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Paulo VI.

Kila mlinzi ataapa, juu ya bendera ya Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswisi na mbele ya Papa Leo XIV, kumlinda na kumtetea Papa wa sasa na wahudumu wake wote halali, hata kwa kuhatarisha maisha yao wenyewe, kama walinzi wengine wengi walivyofanya hapo awali. Tukio hilo lina sifa ya mazingira ya sherehe maalum. Walinzi wakiwa wamevalia nguo rasima "Gran Gala," yaani sare, ikiwa ni pamoja na silaha, zinazovaliwa kwa ajili ya baraka ya Papa ya "Urbi et Orbi" wakati wa Noeli na Pasaka.

Programu

Sherehe kuu ya kuapishwa itatanguliwa na Masifu ya Jioni mnamo Mei 5 saa 11:00 jioni katika Kanisa la Mtakatifu Maria wa Huruma  Katika Makaburi ya Vatican !(Campo Santo Teutonico.) Hii itafuatiwa na kuwekwa kwa shada la maua kwa heshima ya wale waliokufa mnamo tarehe 6 Mei 1527, na kukabidhiwa heshima. Siku ya sherehe ya kuapishwa, tarehe 6 Mei  saa 1:30 asubuhi, Katibu Mkuu wa Vatican  Kardinali Pietro Parolin ataongoza Ibada ya Misa katika Basilika ya Mtakatifu Petro. Sherehe ya kuapishwa inaweza kuonyeshwa moja kwa moja kwenye tovuti rasmi ya Kikosi cha Walinzi wa Kipapa wa Uswiss: www.guardiasvizzera.ch.

Wajumbe kutoka Uswiss

Ujumbe kutoka Shirikisho la Uswiss utakuwepo, ukiongozwa na Rais Guy Parmelin, Rais wa Baraza la Kitaifa Pierre-André Page, na Rais wa Baraza la Mataifa Stefan Engler. Jeshi la Uswiss pia litawakilishwa na Mkuu wa Jeshi, Luteni Kamanda Benedikt Roos, huku Baraza la Maaskofu wa Uswiss litawakilishwa na Rais wake, Askofu Charles Morerod, Askofu wa Lausanne, Geneva, na Fribourg. Ujumbe wa Cantone mgeni rasmi wa mwaka huu 2026, Thurgau, utaongozwa na Baraza la Serikali na kuongozwa na Rais wa Baraza hilo Dominik Diezi.

Jeshi la Kongwe Zaidi Duniani

Walinzi wa Kipapa wa Uswisi ndio jeshi kongwe zaidi duniani. Lilianzishwa mnamo tarehe 22 Januari 1506, na Papa Julius II, ambalo linawajibika kwa ulinzi wa Papa na makazi yake. Likiongozwa na Kanali Christoph Graf, linawajibika kudhibiti ufikiaji wa Vatican na Jumba la Kitume; kuhakikisha utaratibu na kutekeleza majukumu ya uwakilishi wakati wa sherehe za upapa na mapokezi ya serikali, na pia kulinda Baraza la Makardinali wakati wa nafasi wazi ya kiti cha Kipapa. Kikosi kinajumuisha walinzi kutoka maeneo yote ya lugha ya Uswiss. Wajumbe wengi wa Kikosi hicho wanatoka katika Jimbo la Valais (18), wengine wanatoka katika Jimbo la Ticino (13) na Lucerne (11).

KIAPO CHA KIKOSI CHA USWISS

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

29 Aprili 2026, 10:15