Tafuta

Askofu Mkuu Caccia. Askofu Mkuu Caccia. 

Vatican:Uaminifu na Mshikamano ni muhimu katika muktadha wa sasa wa Kimataifa

Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwa Umoja wa Mataifa huko New York, Askofu Mkuu Gabriele Caccia,alizungumza wakati wa Siku ya Kimataifa ya Mapambano dhidi ya Uislamu,akisisitiza umuhimu wa kupambana na ubaguzi unaoharibu uhusiano wa "kiroho, maadili, na kijamii" kati ya makundi tofauti ya kidini."Ujuzi mpya wa kidijitali" unahitajika ili kuzuia kuenea kwa chuki za kidini mtandaoni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika hotuba yake Askofu Mkuu Gabriele Caccia, Mwakilishi wa  Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa, iliyotolewa tarehe 16 Machi 2026 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani,  wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana dhidi ya Chuki ya Uislamu, iliyoandaliwa na Muungano wa Ustaarabu wa Umoja wa Mataifa na Tume za Kudumu ya Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu kwa Umoja wa Mataifa alibainisha kuwa, "Ubaguzi na vurugu dhidi ya Waislamu sio tu kwamba vinawadhuru watu binafsi, bali pia vinadhoofisha muundo wa kiroho, kimaadili na kijamii wa jamii kwa ujumla, na kudhoofisha vifungo vya uaminifu na mshikamano ambavyo ubinadamu unahitaji hasa katika muktadha wa sasa wa kimataifa."

Kulinda uhuru wa kidini ni kipaumbele

Askofu Mkuu Caccia aliyeteuliwa  hivi karibunu tarehe 7 Machi na Papa Leo XIV kama Balozi mpya wa Vatican nchini Marekani, alibainisha kuwa "uendelevu wa Uislamuu" ni kama ishara ya hitaji la haraka la kulinda uhuru wa kidini. "Kutovumilia, ubaguzi na uadui" dhidi ya Waislamu, Wayahudi, Wakristo na wafuasi wengine wa dini za kiutamaduni ni matokeo ya moja kwa moja ya "kutotambua na  kutotetea uhuru wa dini na imani".

Haki ya mtu ambaye, kama mwanadiplomasia wa Vatican alivyofafanua kwa kunukuu hotuba ya Papa Leo kwa Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji,mwezi Oktoba 2025( discorso di Leone XIV tenuto lo scorso ottobre all’organizzazione Aid to the Church in Need, alisema inaharibiwa na  miunganisho ya kijamii kwa kuanzisha kutoaminiana kati ya makundi ya kidini. "Uhuru huu unapokataliwa, mwanadamu hunyimwa uwezo wa kujibu wito wa ukweli kwa uhuru," alisisitiza Askofu huyo. "Kinachofuata ni kuvunjika polepole kwa miunganisho ya kimaadili na kiroho inayodumisha jamii; uaminifu huacha nafasi ya hofu, tuhuma hubadilisha mazungumzo, na ukandamizaji huzaa vurugu."

Papa:Uhuru wa kidini si jambo la hiari, bali ni msingi wa jamii yenye haki

Katika hotuba yake kwa wajumbe wa Mfuko wa Kipapa wa Kanisa Hitaji( Aid to the Church in Need),Papa  Leo XIV alisisitiza kujitolea kwake kuunga mkono Wakristo walio wachache katika nchi kama vile Jamhuri ya Afrika ya Kati, Burkina Faso, na. ambapo Mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa pia alisisitiza jukumu la mtandao katika kueneza "ubaguzi dhidi ya makundi ya kidini." Alisisitiza kwamba mtandao unaweza kuwa mazingira mazuri kwa kuenea kwa haraka kwa "masimulizi ya uadui" na "kushawishi mtazamo wa umma." Hatari hii lazima ishughulikiwe kupitia "mipango imara ya kielimu" na "ujuzi wa kidijitali" zaidi, ambao husaidia watumiaji wa majukwaa ya mtandaoni kukuza "mawazo muhimu" na uhuru wa roho.

Kubadilisha Tofauti Kuwa Utajiri

Hatimaye Askofu Mkuu Caccia alisisitiza umuhimu wa kukuza "mazungumzo halisi ya kidini," chombo kinachoweza kubadilisha tofauti kuwa "chanzo cha utajiri" na kuhakikisha kwamba "hakuna dini inayotumiwa vibaya au kuendeshwa kwa vyombo." Aliunga mkono hoja hii kwa nukuu kutoka kwa hotuba ya Papa Leo XIV iliyotolewa mnamo tarehe 25 Oktoba 2025 katika maadhimisho ya miaka sitini ya Nostra Aetate: "Mazungumzo,  si mbinu au chombo, bali ni njia ya maisha, njia ya moyo inayobadilisha washiriki wake wote, wale wanaosikiliza na wale wanaozungumza."

17 Machi 2026, 12:36