Tafuta

Kard.Van Thuan,Mchungaji aliyefundisha kutumaini

Katika mkutano kwenye Jumba la Lateran ilisimuliwa historia ya kumbukumbu ya sura na kazi ya Kardinali wa Vietnam,aliyefungwa kwa miaka 13 nchini mwake na Mwenyeheri tangu 2017.Ujumbe wa ufunguzi ulikuwa kutoka kwa Papa Leo XIV.Kard.Czerny:"Alikuza upatanisho,haki na amani duniani kote.Katika majaribu,ukuu wa imani yake."Kard.Tagle:"Nilimwita ‘mjomba,’alikuwa zawadi kwa Kanisa."Dada yake Élisabeth Nguyễn na mwakilishi wa mchato wake alikuwepo.

Na Salvatore Cernuzio -Vatican.

Unabii, shujaa, mwenye kuona mbali, mkarimu, na mwenye shauku katika ushuhuda wake wa imani, hata wakati wa miaka ya mateso ya wanadamu ambayo ilikuwa kifungo chake, ambapo aliadhimisha Misa kwa siri akiwa na matone matatu ya divai na moja ya maji mkononi mwake, pamoja na kujitolea kwake kwa Mungu na waliodhaifu wa ulimwengu. Maneno huwa machache sana kuelezea urithi unaong'aa ulioachwa duniani na maisha na kazi ya Askofu Mkuu François Xavier Nguyễn Văn Thuận, Kardinali wa Vietnam aliyetangazwa kuwa Mwenyeheri  mwaka 2017, mfungwa katika magereza ya kikomunisti ya nchi yake.

"Shahidi wa matumaini," kila mtu anamwita. Shahidi wa Matumaini ndiyo ilikuwa mada ya mkutano uliofanyika alasiri tarehe 25  Machi 2026, katika Jumba la Lateran, Roma.  Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza Watakatifu pamoja na Baraza la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Makleri, Jimbo Kuu la Roma na Nyumba ya Uchapishaji ya Città Nuova.

Historia ya kumbukumbu

Ulikuwa ni wakati wa ukumbusho, kushiriki, pia unaoakisi muziki na historia kuhusu vipengele vinavyojulikana zaidi vya Kardinali, mbele ya Makardinali: Michael Czerny, Lazzaro You Heung-Sik, Luis Antonio Tagle, Baldo Reina, dada yake Élisabeth Nguyễn Thị Thu Hồng, na mhamasishaji wa Mchakato wa kutangazwa Mtakatifu, Waldery Hilgeman. Pia ilikuwa fursa ya kusherehekea kumbukumbu ya miaka 50 ya kuandikwa kwa kitabu: "Njia ya Matumaini," mawazo hayo 1001 ambayo Kardinali aliandika akiwa  gerezani, ambapo alitumia miaka 13 (kuanzia mwaka 1975 hadi 1988), na ambayo aliyatoa kwa waamini wake.

Ujumbe wa Papa Leo XIV

Katika Ukumbi wa Mikataba yenye hisia yaani Ukumbi wa Mikataba ya Lateran, lakini pia ulikuwa Ukumbi uleule ambapo, mwaka  2013, hitimisho la awamu ya kijimbo ya mchakato wa kumtangaza Van Thuan kuwa mtakatifu lilisainiwa, kulikuwa na makofi mengi wakati mratibu, wa hafla hiyo, Mwandishi wa habari wa vyombo vya habari vya Vatican Alessandro De Carolis, alipotangaza usomaji wa ujumbe kutoka kwa Leo XIV amnaye  alitaka kuchangia katika tukio hilo, katika ujumbe uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin akisema kuwa: linatusaidia kugundua upya ushuhuda wa Kikristo wenye bidii wa mchungaji huyu mkarimu, ambaye mfano wake umejaa umuhimu leo.” Van Thuan anakumbusha kwamba “tumaini la Kikristo huzaliwa kutokana na kukutana na Kristo na huchukua umbo katika maisha yaliyotolewa kwa Mungu na jirani,” Papa alithibitisha.

KARD VAN THUAN

L'intervento del cardinale Czerny

Hotuba ya Kardinali Czerny

Kardinali Czerny:Bado anatuonesha njia leo hii

Maneno haya yalihibitishwa na hotuba ya Kardinali Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu, ambalo lilijumuisha Baraza la Kipapa la "Haki na Amani," ambalo Kardinali Van Thuan aliwahi kuwa rais wake. Papa Yohane Paulo II alimpatia  wadhifa huu mnamo 1998, kwa kutambua fadhila, mtu anaweza kuziita "shujaa" leo za kardinali, ambaye kila mara alieneza kanuni za haki na amani ndani na nje ya Kanisa. Hakukuza maadili haya tu, bali pia aliyadhihirisha "kwa neno na tendo," kupitia maisha "ya kinabii na yasiyo na ubinafsi," alisema Kardinali Czerny.

Kisha akaungana tena na historia ya "mtangulizi wake mashuhuri": huduma yake ya hiari huko Hue katika hospitali, magereza, na makoloni ya wenye ukoma; ujenzi wa vituo vya ukoma ambapo alichangia akiba yake yote, licha ya kuishi kwa gharama ndogo; Uaskofu wake huko Nha Trang, ambapo alizindua mipango mingi ya kielimu na kijamii na kufanya kazi ya upatanisho katika nchi iliyogawanyika, na, bila shaka, kifungo chake, kilimfanya kudumisha mtazamo wa amani na huruma, hata kwa walinzi wake. "Kilichompa nguvu katika majaribu yake magumu zaidi ilikuwa Injili ya Yesu Kristo," Kardinali Czerny alisisitiza.

Mkuu wa Baraza la Kipapa  la Kuhamasisha Huduma ya maendeleo Fungamani ya Binadamu pia alikumbuka kazi ya Kardinali Van Thuan jijin Roma; tangu 1991, hakuweza kurudi katika nchi yake na akabaki "bila jukumu maalum" kwa miaka kadhaa. Katika kipindi hicho, alifanya "kazi ya kupongezwa" kwa kuwasaidia wakimbizi wa Vietnam na kuanzisha mtandao wa misaada ya kimataifa. Tunawezaje kusahau Muhtasari wa Mafundisho ya Kijamii ya Kanisa wa 2004, ulioandaliwa kwa kuhimizwa na Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo 1999, ambaye alimwomba atoe "muhtasari unaoeleweka kwa wote." "Kwa msaada wa wataalamu kadhaa, Kardinali Van Thuan mara moja alizindua mfululizo wa semina katika sehemu mbalimbali za dunia, mchakato wa mazungumzo na maeneo tofauti ya kijiografia, badala ya kuandika hati iliyofungwa," Kardinali alielezea. Na katika kujibu kilio cha maeneo mengi ya dunia yaliyo maskini kwa unyonyaji na kutengwa, Muhtasari ulikuja, ambao, hata leo hii, Kardinali huyu anaendelea kutuonesha njia ya : "Imani thabiti, tumaini la kuambukiza, upendo unaosamehe kwa dhati."

Makamu wa Papa,Kardinali Reina:pamoja naye tunakusanya urithi wa Jubilei

Mojawapo ya maandishi ya Kardinali Van Thuan pia yaliishia mikononi mwa Padre kijana wa wakati ule Baldo Reina, ambaye sasa ni Makamu wa Papa Jimbo Kuu la Roma. Yeye mwenyewe alikumbuka hilo katika hotuba fupi ya ufunguzi: "Ilikuwa mwaka 1995, na mwanafunzi mwenzangu alinipatia kitabu kidogo ambacho nilisoma kwa hamu, na tangu wakati huo nilishangazwa na mtu huyu wa ajabu." Mtu ambaye Kardinali Reina alitaka kuunganisha na Jubilei ya Matumaini, ambayo ilituachia "ahadi" badala ya "kauli mbiu": kuwa Mahujaji wa Matumaini, kwa hivyo mashuhuda wa matumaini. Kardinali Van Thuan ni hivyo tu, na "kwa nguvu zake, azimio, na utulivu, anatusaidia kukusanya urithi wa Jubilei na kuifanya kuwa yetu wenyewe.

Kardinali You:Mfano wa Maisha ya Kikristo

François-Xavier Nguyễn Văn Thuận ni "mfano wa kweli wa maisha ya Kikristo na kikuhani," alirudia Kardinali You, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makleri, ambaye alitoa ushuhuda wa moja kwa moja wa mfungwa mwenzake wa Kibuddha: Nguyen Thanh Giau, ambaye sasa ni mkuu wa shirika la Hoa Hao. Kisha kumbukumbu za safari ya mashua, zote zikiwa zimefungwa minyororo, hadi kambi mpya kaskazini, huku walinzi wakiwanyang'anya wafungwa mali zao binafsi. "Kila mtu alikuwa akilia kwa hasira na kukata tamaa, lakini Askofu Thuận alituambia: 'Tutanyang'anywa karibu kila kitu, lakini kuna kitu kimoja ambacho hakuna mtu anayeweza kutunyang'anya, nacho ni imani yetu kwa Mungu.'" Au dawa, zilizotumwa na familia yake, ambazo Padre huyo alishiriki na wenzake wa gerezani ambao waliteseka kutokana na kichefuchefu cha baharini, au kazi ya kulazimishwa kambini, katika baridi chini ya nyuzi joto 2 , ambapo alilazimishwa kusomba choo kinachobebeka. Hatukutaka afanye kazi hii chafu, lakini yeye alisisitiza: "Ni heshima kwangu kushiriki katika maisha yetu yote." "Nilikuwa naye kwa miezi michache tu, lakini ninaweza kushuhudia kwamba alikuwa kile ambacho sisi Wabudha tunakiita Bo tac, yaani, mtu Mtakatifu sana. Natumaini kuona siku ambayo Askofu Thuận atatangazwa kuwa Mtakatifu, ili watu wa dini zote waweze kumheshimu," Giau alisema. Maneno ambayo Kardinali You aliongeza: "Maisha yake yaligubikwa na majaribu magumu sana, lakini ilikuwa hasa katika majaribu hayo ndipo ukuu wa imani yake ulifunuliwa."

La relazione del cardinale You

Hotuba ya Kardinali You

Kardinali Tagle:Mtumishi wa Mungu na Kanisa

Kuanzia machozi hadi tabasamu au hata kicheko cha moja kwa moja kwa mfululizo wa historia zilizoshirikishwa na Kardinali Tagle, ambaye Văn Thuận alimjua vizuri sana. Uhusiano ulioibuka ghafla na polepole ukawa na nguvu zaidi, kiasi kwamba Kardinali alimwambia Padre kijana wa Ufilipino amwite "mjomba." Ulikuwa mwaka 1995, tukio la kikao cha jumla cha Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Asia (FABC). Kardinali Tagle alipewa jukumu la kutoa tafakari ya utangulizi: "Nilipojikuta mbele ya Maaskofu wa Asia, nilijuta kukubali mwaliko huo. Nikiwa na wasiwasi mwingi, nilisoma maandishi yangu haraka na, mara tu nilipomaliza, nilitoka haraka nje ya ukumbi, nikaenda kwenye chumba cha chakula nikajitengenezea kikombe kikubwa cha kahawa, na nilitumaini hakuna mtu angeniona. Wakati nilipokuwa nikinywa kahawa yangu, Askofu mmoja alinikaribia: 'Ulionekana kuwa na wasiwasi wakati wa mkutano, lakini ulishughulikia vyema sana. Ulikuwa mzuri sana,'" alisema.

 Alikuwa Kardinali Văn Thuận, ameketi mbele ya Padre huyo mwenye hisia, ambaye alimwambia historia yake. "Nilishangazwa na ukweli kwamba, ingawa alikumbuka matukio yenye uchungu na hata ya kufedhehesha, sauti yake ilibaki tulivu na uso wake ulikuwa mtulivu. Hakukuwa na chembe ya uchungu au chuki ndani yake," Kardinali Tagle alisimulia. "Kabla hatujatengana, aliniambia: 'Kuanzia sasa, niite mjomba. Ukienda Roma, hakikisha unakuja kuniona.'" Kardinali Tagle alitimiza ahadi yake na, kila alipokuwa Roma, alimpigia simu Kardinali Van Thuan, rais wa Baraza la Kipapa la Haki na Amani ("Mjomba wangu sasa alikuwa rais!").

Chakula cha jioni pamoja, mazungumzo, zawadi za vitabu, Kardinali Tagle alikuwepo wakati wa kuundwa kwa Kardinali na Van Thuan hakuwepo kwenye Kuwekwa wakfu  wa kiaskofu kutokana na matatizo ya kiafya. "Aliahidi kuniombea. Tulitaniana kwamba Kardinali sasa ana mpwa ambaye ni Askofu." Mnamo 2002,  Roma, Mwenyekiti wa  sasa wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji aliitwa makazi ya Kardinali wa Vietnam: "Niliambiwa kwamba mjomba wangu Kardinali alikuwa mgonjwa sana. Alikuwa na saratani ya tumbo. Sasa naelewa ni kwa nini alikula kidogo sana. Lazima alikuwa na maumivu aliponipeleka kwenye migahawa. Lakini mateso yake hayakumzuia kuwafurahisha wengine." Mnamo Septemba 16, alifariki. Kardinali Tagle alihudhuria Misa ya mazishi mnamo tarehe 20 Septemba 2002, katika Kanisa la Mtakatifu Petro. "Huzuni ilikuwa wazi hewani, lakini pia shukrani kwa zawadi ya mtumishi huyu wa Mungu na Kanisa. Nilipokaribia mlango, nilisimama na kugusa jeneza lake, nikinong'ona: 'Mjomba, niko hapa. Ulifanya kazi nzuri. Ulikuwa bora sana.'"

Il ricordo del cardinale Tagle

Kumbukumbu ya Kardinali Tagle kuhusu Kardinali Van Thuan

"Asante"ya Dada Élisabeth

Hotuba ya Élisabeth, Dada yake Mwenye heri ilikuwa sauti ya familia nzima ya Văn Thuận iliyoenea katika mabara matano, pia ilikuwa ya kugusa moyo. Neno moja, "Asante," lilikuwa la kudumu midomoni mwake. Asante kwa kueneza ushuhuda wa kaka yake na kwa uzoefu huu mgumu wa kidunia ambao Mungu aliumba pamoja naye, ambao, kama uzi wa kawaida, uliunganisha historia ya mateso ya mababu zao, kulazimishwa kuona alama kwenye nyuso zao, vijiji viliharibiwa, mali zilizochukuliwa, familia za Kikristo zilitenganishwa kwa nguvu. Licha ya kila kitu, "waliweza kudumisha uwepo wa Yesu hai, na hii iliwaweka umoja katika imani." Ndugu yake François alifanya vivyo hivyo alipoandika na kutuma kwa siri Tafakari 1001: "safari ya uinjilishaji" iliyogusa seli na kambi, kuvuka bahari, na kusafiri na watu wa boti. "Leo, pamoja nanyi, kwa roho ya shukrani, tunashuhudia nguvu ya uwepo wa Mungu kupitia historia ya mchungaji aliyetengwa na kundi lake, lakini tukibaki tumeungana nao kwa karibu kupitia Neno la Mungu."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

26 Machi 2026, 10:25