Tafuta

2026.03.23 Mtumushi wa Sr Stanislawa Samulowska anakaribia utakatifu. 2026.03.23 Mtumushi wa Sr Stanislawa Samulowska anakaribia utakatifu. 

Vatican:Watakatifu sita wapya wameongezeka katika Kanisa!

Utambuzi wa maisha ya Askofu wa Albano,aliyekufa kwa kipindupindu akiwa amesimama kidete pamoja na waamini wake.Fadhila za kishujaa za Edward Joseph Flanagan,mwanzilishi wa Jiji la vijana;Henri Caffarel,mwanzilishi wa Chama cha"Equipes Notre Dame"na Taasisi ya Kidunia ya "Udugu wa Mama Yetu wa Ufufuko;"Stanisława Samulowska,Romero Algarín,wote wakiwa watawa na Giuseppe Castagnetti,Mlei.

Vatican News

Papa Leo XIV akikutana na  Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuwatangaza  Watakatifu, mjini Vatican Jumatatu asubuhi tarehe 23 Machi 2026 aliidhinisha  Baraza la Kipapa kutangaza amri kadhaa zinazohusisha  watu sita kuelekea utakatifu.

Papa alitambua kujitolea kwa Mtumishi wa Mungu Ludovico Altieri, Askofu wa Albano, Kardinali wa Kanisa Takatifu la Roma, aliyezaliwa tarehe 17 Julai 1805  Roma, Italia, ambaye alifariki tarehe 11 Agosti 1867 katika mji wa vilima wa Albano Laziale nchini Italia.

Ludovico Altieri
Ludovico Altieri

Baba Mtakatifu pia alitambua sifa zifuatazo za kishujaa za watu wanne watawa na mlei wa Kiitaliano ambaye alikuwa baba wa familia:

- Mtumishi wa Mungu Edward Joseph Flanagan, Padre wa Jimbo, Mwanzilishi wa Kijiji cha Watoto aliyezaliwa huko Berlin, Ujerumani;

Edward Joseph Flanagan
Edward Joseph Flanagan

- Mtumishi wa Mungu Henri Caffarel, Padre wa Jimbo na  Mwanzilishi wa Chama cha "Timu za Mama Yetu"(Équipes Notre-Dame) na wa Taasisi ya Kidunia "Udugu wa Mama Yetu wa Ufufuko", aliyezaliwa tarehe 30 Julai 1903 huko Lyon, Ufaransa, na kifo chake tarehe 18 Septemba 1996 huko Beauvais;

Henri Caffarel
Henri Caffarel

- Mtumishi wa Mungu Stanisława Samulowska (jina la ubatizo  Barbara), mtawa wa shirika la Mabinti wa Upendo  Mtakatifu  wa Vincent wa Paulo,  alizaliwa tarehe 30 Januari 1865 huko Woryty nchini Poland,  na kifo chaketarehe 6 Desemba 1950 katika Jiji la Guatemala.

Stanisława Samulowska
Stanisława Samulowska

- Mtumishi wa Mungu María wa Bethlehemu wa Moyo wa Yesu Romero Algarín (kwa ubatizo María Dolores), mtawa wa Shirika,  Wajakazi wa Moyo wa Kimungu, aliyezaliwa tarehe 7 Oktoba 1916 huko Seville, Hispania, ambaye alifariki tarehe 12 Novemba 1977 huko Sanlúcar la Meya;

Maria wa Betlehem wa Moyo wa Yesu- Romero Algarín
Maria wa Betlehem wa Moyo wa Yesu- Romero Algarín

- Mtumishi wa Mungu Giuseppe Castagnetti, mwamini mlei na baba wa familia, aliyezaliwa tarehe 15 Machi 1909 huko Montebaranzone, Italia, na kufariki tarehe 22 Juni 1965.

Giuseppe Castagnetti
Giuseppe Castagnetti

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

23 Machi 2026, 16:19