Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni kote watangaza Kanuni zake kuu
Vatican News
Mnamo tarehe 19 Machi, 2026, katika Sherehe ya Mtakatifu Yosefu, mlinzi wa Shirika la Yesu, Kanuni mpya za Jumla za Mtandao wa Nia za Maombi ya Papa Ulimwenguni Pote (PMPN) zilichapishwa. Uchaguzi wa tarehe si wa bahati mbaya, kwani : Baba Mtakatifu aliikabidhi Jumuiya usimamizi wa kitume wa Kazi hii ya Kipapa, ambayo huduma yake inaelezwa kupitia Mfuko wa Vatican , Roma na mtandao wenye wanachama milioni 22 waliopo katika zaidi ya nchi 90. Waraka huu unatoa maono kamili na yaliyosasishwa ya utambulisho, utume, na muundo wa chombo hiki cha kikanisa ambacho, tangu kuundwa upya kwake, hakijitokezi tena kama harakati rahisi ndani ya Kanisa, bali kama mtandao wa ulimwengu wote katika huduma ya moja kwa moja ya Baba Mtakatifu na wote walioungana naye kupitia vifungo vya sala na huduma
Utume wa Huruma inayotokana na Moyo wa Yesu
Kanuni zinafafanua Mtandao wa Nia za Maombi wa Baba Mtakatifu( RMPP) kama Huduma ya Kitume ya Kipapa na Mfuko wa Kipapa "katika huduma ya kikanisa ya Kiti Kitakatifu." Kusudi lake ni wazi: kuwahamasisha Wakristo (mmoja mmoja au katika vikundi) kujibu, kupitia sala, malezi ya kiroho, na huduma, changamoto za ubinadamu na utume wa Kanisa, kama Papa anavyozitambua na kuzielezea kila mwezi katika nia zake za maombi. Padre Cristóbal Fones SJ, Mkurugenzi wa Kimataifa wa Mtandao wa maombi Ulimwenguni(RMPP,) alisema kwamba kuchapishwa kwa Kanuni Kuu ni "ukumbusho wa mara kwa mara wa utume ambao Baba Mtakatifu ametukabidhi na ambao tunatafuta kuutumikia kwa uaminifu ulimwenguni kote."
Utume huu umejikita katika hali ya kiroho ya Moyo wa Yesu na hupata marejeo yake ya msingi ya ufundishaji katika programu ya malezi ya Njia ya Moyo. Ni pendekezo linalochanganya urafiki wa karibu na Kristo na kujitolea halisi, likitualika kupata uzoefu wa maombi si kama kitendo cha pekee, bali kama uwazi wa huruma kwa majeraha ya ulimwengu. Mrithi wa Utume wa Maombi wa kihistoria, Mtandao wa maombi kimataifa wa Papa (RMPP) unaoanisha tamaduni yake na changamoto za kisasa katika Sheria zake Ndogo mpya. Kwa hivyo maandishi yanatoa "miongozo iliyo wazi ili kutusaidia kutembea pamoja," sambamba na Sheria zilizoidhinishwa mwaka 2024, na huanzisha mfumo wa udhibiti wenye uhalali wa awali wa miaka miwili, hadi marekebisho yaliyopangwa kufanyika mwaka 2028.
Muundo katika huduma ya utume
Sheria Ndogo zimegawanywa katika sehemu nne. Ya kwanza inafafanua utambulisho na asili ya Kazi kama Mfuko wa Vatican. Ya pili inaelezea muundo wake wa kimataifa, kitaifa, kijimbo, na kijumuiya, ikibainisha vyombo vyake vya uongozi, kamati za ushauri, na miongozo ya utawala. Ya tatu inaelezea njia za ushiriki. Hatimaye, mfumo wa pamoja wa ulinzi na ulinzi wa watoto na watu wazima walio katika mazingira magumu umeanzishwa, kupitia vigezo vya lazima vya mbinu, mafunzo, na utaratibu kwa Mtandao mzima, kuhakikisha uthabiti, uwazi, na uwajibikaji.
Mfuko wa Vatican, pamoja na Ofisi yake ya Kimataifa jijini Roma, huhuisha na kuratibu utume wa kimataifa, kila mara katika mazungumzo na miundo ya kanisa ya ndani, kijimbo, na Mtandao wa Maombi. Ufafanuzi huu unaruhusu Mtandao wa Nia za Maombi ya Papa Ulimwenguni (RMPP )kudumisha tabia yake ya ulimwengu wote, huku ikijumuisha hali halisi mbalimbali za kitaifa kikanisa.”
Ni mtandao, si harakati
Mojawapo ya mambo yanayosisitizwa wazi ni asili ya Mandao wa nia za mambi ya Papa Ulimwenguni(RMPP.) Sio muungano uliofungwa wala harakati yenye utambulisho huru, bali ni mtandao mpana na tofauti wa Wakristo ambao, kuanzia uanachama wao wa kikanisa, kama vile parokia, Majimbo, mashirika, harakati, Jumuiya, wahamasishaji na dhamira ya pamoja ya kuomba na kutenda kwa hisia za Kristo na kulingana na dira ya nia ya Papa, ambayo hupanua mtazamo wetu wa ulimwengu.
Kanuni zinatofautisha njia mbili za kushiriki. Ya kwanza iko wazi: mtu yeyote anaweza kujiunga, hasa kupitia Siku ya Kila Mwezi ya Maombi kwa nia za Papa, Ijumaa ya kwanza ya mwezi. Ya pili ni aina ya uanachama iliyo wazi zaidi, ambayo inahusisha kupitisha mdundo wa sala ya kila siku na, inapobidi, kujiweka wakfu kwa Moyo wa Yesu, kibinafsi na kama jumuiya. Harakati ya Vijana wa Ekaristi (EYM), mpango wa ufundishaji wa vijana wa Mtandao, inafaa katika mfumo huu. Inachukua historia ya wanafunzi wa Emau (Luka 24) kama safari yake ya uundaji. Harakati ya Vijana wa Ekaristi(EYM) si ukweli unaofanana, lakini ni sehemu ya utume huu wa kipekee wa huruma, unaoendana na umri na mazingira ya vijana.
Imeongozwa na mwaliko wa Papa Leo XIV
Katika mkutano wake wa hivi karibuni na wanachama wa Ofisi ya Kimataifa, wafadhili, na marafiki wa Mtandao wa Nia za Maombi (Januari 30, 2026), Papa Leo XIV alisisitiza kwamba utume wa maombi ya Mtandao wa Maombi ni "sehemu muhimu ya kazi ya kiinjili ya Mwili wa Kristo." Alisisitiza kwamba kusali kwa nia yake ni jibu la "huruma na upendo" iliyozaliwa kutokana na urafiki na Moyo wa Yesu na hutafsiriwa katika upatikanaji wa kitume. Baba Mtakatifu alithibitisha waziwazi Njia ya Moyo kama mwongozo wa malezi kwa waliobatizwa kuchukua utambulisho wao kama "marafiki na mitume wa Kristo" katikati ya changamoto za sasa. Pia alitoa mwaliko wazi wa kutazama wakati ujao: "waalike vijana kushiriki," akiashiria Harakati ya Vijana ya Ekaristi kama njia yenye matunda hasa ya kuunda "kizazi kijacho cha waombezi."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.