Tafuta

2026.03.19 Ndoto ya Mtakatifu Yosefu,Giacinto Brandi(anayehusishwa),yapata mwaka 1648,Chuo cha Kipapa cha Mkusanyo wa picha kupitia wenye ujuzi katika Pantheon. 2026.03.19 Ndoto ya Mtakatifu Yosefu,Giacinto Brandi(anayehusishwa),yapata mwaka 1648,Chuo cha Kipapa cha Mkusanyo wa picha kupitia wenye ujuzi katika Pantheon.  (© Paolo Sparac)

Pantheon:Katika sherehe ya Mtakatifu Yosefu,misa katika Kanisa la Mtakatifu Maria wa Mashahidi

Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Mashahidi,Roma Machi 19, kutakuwa na maadhimisho ya misa saa 11.00 jioni ya sherehe ya Mtakatifu Msimamizi wa Chuo cha Kipapa cha wenye ujuzi wa kisanaa na muziki cha Pantheon.Kardinali José Tolentino de Mendonça ataongoza.Katika ukumbi wa chuo hicho kutakuwa na maonyesho yaliyotolewa kwa ajili ya Mtakatifu Yosefu.Muziki na Kwaya ya Jimbo la Roma kwa kuongozwa na Monsinyo Marko Frisina.

Vatican News

Katika Sherehe ya Mtakatifu Yosefu, katika Pantheon, Roma kwa mara nyingine inakuwa mahali pa kukutania imani, sanaa, na tamaduni. Siku ya Alhamisi, tarehe 19 Machi 2026, saa 11.00 jioni, Misa kuu itaadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Mashahidi kwa heshima ya Mtakatifu mlinzi wa Chuo cha Kipapa cha ‘Virtuosi al Pantheon, yaani (wenye ujuzi wa kisanaa na Muziki). Liturujia itaongozwa na Kardinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.

Maonyesho

Sambamba na sherehe hiyo, Chuo hiki kinawasilisha maonyesho katika ukumbi yenye kichwa: "Yosefu, Mtu wa Ndoto," yakionesha kazi kutoka mkusanyo wa picha zinazoongozwa na sura ya Mtakatifu huyu. Maonyesho hayo yanaakisi sifa muhimu za Mtakatifu Yosefu kama baba, mlezi, na kiongozi wa familia, kupitia michoro sita ambayo pia inakumbusha vipindi vya Injili vinavyohusiana na ndoto na maamuzi yanayotokana nayo. Kwa kuanzishwa katika karne ya 16, Chuo hiki cha Kipapa cha 'Virtuosi' katika Pantheon kinawaleta pamoja wasanii, wasanifu majengo, na wasomi waliobobea katika mazungumzo kati ya sanaa na mambo ya kiroho. Kuchaguliwa kwa Mtakatifu Yosefu kama Mtakatifu wake mlinzi kunaibua mtazamo thabiti na wa kimya wa imani, unaooneshwa katika kazi, uwajibikaji, na utunzaji kwa wengine.

Sherehe hiyo itaambatana na Kwaya ya Jimbo la Roma, ikiongozwa na Monsinyo Marco Frisina, ikiwa na mkusanyo wa nyimbo za kiliturujia unaosisitiza asili ya sherehe hiyo. Kulingana na matangazo ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Mashahidi,  Chuo cha Kipapa cha Virtuosi al Pantheon, ufikiaji wa maonyesho utafuata miongozo ya parokia ya Pantheon, huku mipango ya ziara ikiunganishwa na sherehe ya kiliturujia. Ziara zimegawanywa katika vipindi viwili na inahitaji kujiandikisha.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

19 Machi 2026, 12:05