Kardinali ajiuzulu shughuli ya upatriaki wa Baghdad ya Wakadayo
Vatican News
Tarehe 10 Machi 2026, Papa Leo XIV alikubali kujiuzulu kutoka wadhifa wa Upatriaki wa Baghdad wa Wakaldayo, uliowasilishwa na Kardinali Louis Raphaël Sako, kwa mujibu wa kanuni 126 §2 ya Kanuni za Makanisa ya Mashariki (CCEO).
Barua ya Kardinali Sako
Katika barua iliyotolewa na Kardinali Sako anaelezea kwamba alikuwa amefikiria kujiuzulu miaka miwili iliyopita, alipokuwa akitimiza miaka 75, na kwamba alikuwa amezungumza kuhusu hilo wakati huo na Papa Francisko na kwamba alikuwa amehimizwa kubaki. Uamuzi wa kuwasilisha kujiuzulu kwake kwa Papa Leo XIV, ili "kujitolea kwa kimya kimya kwa maombi, maandishi, na huduma rahisi,"na kuelezea hilo katika barua "ili kuepuka kutoelewana kokote," akithibitisha kwamba hakulazimishwa na mtu yeyote kufanya hivyo na kwamba aliomba ajiuzulu kwa hiari. "Niliongoza Kanisa la Wakaldayo katika hali ngumu sana na katikati ya changamoto kubwa," Kardinali Sako aliandika. "Nilihifadhi umoja wa taasisi zake na kujitahidi kuutetea.” Kardinali pia anasema kwamba amefanya vivyo hivyo kwa ajili ya "haki za Wairaq na Wakristo, akichukua msimamo na kudumisha uwepo ndani na nje ya nchi."
Patriaki mpya anayeamini katika ufufuko
Kardinali anasimulia kwamba miaka yake 13 ya huduma huko Baghdad "ilikuwa miaka ya utunzaji wa kichungaji wenye upendo, usindikizaji, na ukuaji." Anamshukuru Mungu "kwa neema ya upendo" aliyopewa yeye, familia yake, wale walioishi naye wakati wa miaka aliyohudumu kama kuhani huko Mosul, Askofu huko Kirkuk, na patriaki huko Baghdad, na wasaidizi wake. "Katika nyakati hizi ngumu, ninatumaini kwamba uongozi wa Kanisa Katoliki la Wakaldayo utakabidhiwa kwa Patriaki mwenye utamaduni imara wa kitaalimungu, ujasiri, na hekima," anatumaini Patriaki Sako, ambaye anaamini kwamba Wakaldayo huko Baghdad wanahitaji "mtu anayeamini katika upya, uwazi, na mazungumzo, na ambaye pia ana ucheshi."
Wosia
Hatimaye, katika barua hiyo, Kardinali anafichua kwamba aliandika wosia wake akiwa bado ni Padre na kuusasisha mara kadhaa, na kwamba ana "takriban dinari milioni arobaini za Iraqi, dola elfu tano za Marekani, na euro elfu tano" zilizokusanywa kutoka "mishahara kwa zaidi ya miaka 52 ya utumishi wa upadre, pamoja na mapato kutokana na mauzo ya nyumba ya familia huko Mosul." Sako hatimaye anasema kwamba hana nyumba au gari, na kwamba "utajiri wake wa kweli" ni "utumishi wake wa kujitolea na vitabu 45 na makala nyingi" ambazo amechapisha.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.