Tafuta

Kardinali Parolin akiwa mbele ya Masalia ya Mtakatifu Francis wa Assisi. Kardinali Parolin akiwa mbele ya Masalia ya Mtakatifu Francis wa Assisi. 

Kard.Parolin:Mt.Francis alikuwa Ndugu wa Wote!

Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican aliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Basilika ya Juu ya Assisi wakati wa maonesho maalum ya mabaki ya Mtakatifu huyo,yakiashiria kumbukumbu ya miaka 800 ya kifo chake.Katika mahubiri yake kwa kutazama hali halisi ya vita,Kardinali alisema:“Kwa ulimwengu wa wasiwasi na vita,Mtakatifu Francis anatoa furaha na udugu.Furaha ya vitu vidogo ni jibu la wasiwasi na huzuni ya kizazi chetu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Dominika tarehe 15 Machi 2026asubuhi saa tano kamili, Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, katika Basilika ya Juu ya Assisi, aliongoza ibada ya misa katika fursa ya maonyesho maalum ya  mabaki ya Mtakatifu Francis, kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 800 ya kifo chake.  Kardinali alielezea msisimko ambao Mtakatifu Mlinzi wa Italia anauonesha ulimwenguni, hata karne nyingi baada ya kifo chake. Kwa njia hiyo “wasiwasi na huzuni kutokana na kazi hatarishi, migogoro ya kiuchumi, mabadiliko ya tabianchi na vita vya wote dhidi ya wote na kila kitu” ilikuwa kiini cha mahubiri yake.

Mtakatifu Francis alikuwa mwenye tabia ya upole na mtulivu

Katika mahubiri yake, Kardinali Parolin, kwa msukumo wa simulizi ya kitabu maarufu cha "Maua Madogo, " ambacho siku moja, Ndugu  Mdogo Masseo wa Marignano, mmoja wa Ndugu zake wa kwanza wa  Mtakatifu Francis, aliuliza kwa nini ulimwengu wote ulimfuata, ukimsikiliza na kumtii, licha ya ukweli kwamba hakuwa mtu mzuri, hakuwa na maarifa mengi, na hakuwa mtukufu. Francis alijibu kwamba,  macho matakatifu zaidi ya Mungu hayajawahi kumtegemea mtu mchafu, asiyetosha, na mwenye dhambi zaidi kuliko yeye. Na bado, Kardinali Parolin alibainisha, Francis aliweza kuvutia pongezi za wataalamu wawili wasiopingika wa Enzi za Kati, mchoraji na mbunifu Giotto na mshairi Dante. Sababu ya mvuto huo mwanadiplomasia wa Vatican alisema, iko katika "wasifu wake wa kibinadamu na wa kiroho," kama ilivyoelezwa na mwandishi wake wa kwanza wa wasifu, Thomas wa Celano. Kwanza kabisa, Mtakatifu Francis alikuwa mwenye tabia ya upole, mtulivu, mkarimu katika usemi, mwangalifu katika kuonya, mwaminifu katika kutimiza majukumu aliyokabidhiwa, mwerevu katika shauri, mwenye ufanisi katika vitendo, mwenye kupendeza katika kila kitu.

Mtakatifu Francis wa Assisi alivumilia

Akiwa na akili tulivu, mtamu katika roho, mwenye kiasi katika roho, aliyezama katika kutafakari, mwenye kudumu katika maombi, na mwenye shauku katika kila kitu," anaandika mwandishi wa Mtakatifu Francis. Lakini vipengele vingine vya utu wake vinaendelea kuvutia "umakini wetu" baada ya karne nane, Kardinali Parolin aliongeza: “Furaha yake kamilifu, umaskini wake mkuu, udugu wake wa ulimwengu wote. Mtakatifu wa Assisi alijua jinsi ya kukubali magumu ya maisha kwa unyenyekevu, uvumilivu, na furaha. Umaskini wake haukuwa njia ya kujinyima furaha  ya kujitahidi kufikia ukamilifu tu, bali njia ya kuwa sawa iwezekanavyo na Kristo. Hatimaye, alijiona kama ndugu kwa kila kitu na kila mtu: kwa wanadamu, kwa uumbaji, kwa ulimwengu, hata kifo dada.

Kumuomba Mungu ambaye hatuachi

Kardinali Parolin mwisho mwa mahubiri yake alikumbuka kuwa Francis, aliandika "Wimbo wa Sifa ya Viumbe" katika wakati wa mgogoro, wa giza, ndani na nje." Wakati, ule  si tofauti na wetu wenyewe, ambapo giza la vita linaonekana kuficha nuru ya matumaini. Hasa katika kipindi hiki cha kihistoria na cha kuwepo, akiitakia amani na wema ulimwengu mzima, na kwa njia hiyo Kardinali Parolin aliwaalika kila mtu kusali, akitumia maneno ya Mtakatifu Francis wa Assisi: akimwomba Mungu ambaye hatuachi, aangaze giza la moyo, atupe imani sahihi, tumaini hakika, upendo kamili, na unyenyekevu mkubwa."

Kardinali Parolin

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

15 Machi 2026, 15:36