Tafuta

Kardinali Koovakad alizungumzia kuhusu wanawake. Kardinali Koovakad alizungumzia kuhusu wanawake.  

Kard.Koovakad: Uongozi wa wanawake unahitajika wakati wa migogoro

Akizungumza katika mkutano uliofanyika Roma,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini alizungumzia kuhusu nafasi ya mwanamke,mazungumzo na utamaduni wa ushirikiano katika ulimwengu ulitawaliwa na migogoro na migawanyo.

Na Pd. Mark Robin Destura RCJ  

Uongozi wa wanawake na mazungumzo ni muhimu katika kujenga daraja kati ya tamaduni na jamii, alisema Kardinal  George Jacob Koovakad  wakati wa mkutano ulifanyika tarehe 6 Marchi, 2026 , kwenye nyumba ya watawa wa Mtakatifu Maria, Roma.

“Majivu ya Dunia inayowaka”

Katika hotuba yake, Kardinal Koovakad alizungumzia juu ya maana ya historia ya wakati huu, akikumbishia kuwa kipindi cha Kwaresma kwa mwaka 2026, kilianza sambamba na mfungo wa Ramadhani kwa Waislamu.  Katika Misa ya Jumatano ya Majivu, Papa Leo XIV  alieleza “uzito wa dunia inayowaka moto,” akielekeza macho yake katika vita zinazoendelea ulimwenguni, madhara ya kudhoofisha sheria ya kimataifa,uharibifu wa mazingira, na mmomonyoko wa  hekima na namna ya kufikiri. Akinukuu maandiko matakatifu kutoka kitabu cha nabii Joel “Mungu wao yuko wapi? Aliongeza kuwa, mazungumzo ni ishara ya matumaini, kwani inamaanisha “tusiishie kwenye majivu tu, bali tunyanyuke na kuanza kujenga tena.”

Kujenga Daraja kwa njia ya mazungumzo

Kardinali alisisitiza kuwa kuanza kujenga upya, inahitaji mwelekeo mpya katika uongozi wa dunia nzima. Wakati migogoro ya sasa inategemea sana teknologia, akili unde, na matumizi ya silaha, kwake amani inahitaji kile anachokiita “maamuzi ya moyo, akili na maisha.” Ina hamasisha uongozi ulioandaliwa vizuri kitaaluma, mazungumzo ya kiutamaduni, na ushiriki wa jamii kwa ujumla. “Kwa sababu hii,” Kardinal Koovakad alihimiza kuwa uongozi na mazungumzo yanakuzwa na mkutano huu lazima yahusishe maarifa, utamaduni na ushiriki wa jamiii nzima.

Wanawake kutoa Kipaumbele cha Amani

Kardinali Koovakad, alikazia mchango wa wanawake katika historia katika kuchangia upatikanaji wa amani. Alitoa mfano wa Mtakatifu Katarina wa Siena, ambaye alikuwa mpatanishi kati ya viongozi wenye nguvu, pamoja na Eleanor Roosevelt, ambaye alichukua jukumu muhimu katika kuandaa Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu. Kardinali alimnukuu pia Nobel Peace Prze Laureate Wangari Maathai, aliyewahi kusema,“Imefika wakati ambapo ubinadamu unaitwa kuvuka kwenda kwenye kiwango kingine cha ufahamu… wakati ambapo tunapaswa kumwaga hofu zetu na kushirikishana matumaini yetu. Wakati huo ni sasa. Wakati huo ni sasa alisisitiza Kardinal, akiangazia idadi ya wanawake ulimwenguni wanaoshughulikia mipango ya kujenga amani duniani kote. Miongoni mwao ni maelfu ya wanawake wa Israeli na Palestina wanaojihusisha na vyama kama Women Wage Peace (Wanawake na Wimbi la Amani) na Women of the Sun (Wanawake wa jua) wanaojihusisha na masuala ya kidiplomasia ya kutafuta upatanishi kwenye mzozo wa Israeli na Palestina.

Sifa za Kiongozi wa Kike

Kwa mujibu wa Kardinal Koovakad, uongozi wa wanawake mara nyingi huleta mabadiliko ya pekee katika nyakati za mafarakano. Hii ni pamoja na ujasiri wa akina mama wa “kujenga madaraja,” kuguswa kwa namna ya pekee na mateso ya wengine, na uwezo wa kukabiliana na changamoto ngumu za kijamii na uthabiti na uamuzi mahiri. Kwake yeye wanawake wameonyesha uwezo mkubwa wa kushinda chuki kwa kushirikisha pande zote, na kushirikisha wapinzani katika mazungumzo, kuhamasisha haki, utunzaji wa mazingira, na maslahi ya wote. Aliongoza kuwa, ustahimili wa wanawake unawasaidia kukabidhiana na mgawanyiko wa kijamii, umaskini, na mahangaiko ya jamii, huku yakikuza matumaini na hekima.

Wajibu wa Pamoja kwa mustakabali wa baadaye

Akiangazia juu ya mgogoro wa kisiasa wa hivi sasa,Kardinali Koovakad alibainisha kuwa huenda njia za kale za usuluhishi hazitafaa kwa sasa. Alisema kuwa, ubinadamu unapaswa kugundua tena utambulisho wake kama familia moja ya wanadamu inayoshiriki sayari moja ya pamoja.Hivyo, kukuza na kuthamini upekee wa uongozi wa wanawake si suala tu la haki, bali pia ni “dhamana kwa ajili ya mustakabali huu.” Kardinali alihitimisha kwa kusisitiza umuhimu wa ushirikiano miongoni wa watu wote, ili kuleta amani.“Kujenga mustakali wa amani, udugu, na mshikamano, kunahitaji kujitoa na kushikana mikono na mioyo yetu kunia mamoja, alisema. “Ni kwa kushirikiana tu tunashinda ubaguzi,kupanda mbegu ya matumaini, na kuchangia ulimwengu wenye utu na udugu zaidi.

11 Machi 2026, 12:23