Balozi wa Vatican wa Lebanon asambaza misaada kwa vijiji vya kusini na anomba msaada
Na Salvatore Cernuzio – Vatican.
"Sasa hivi, nimesikia mlipuko kutoka kwa Bialozi wa Vatican… Inamaanisha muziki unaanza tena Beirut," Askofu Mkuu Borgia aliiambia Vatican News, Ijumaa jioni tarehe 13 Machi 2026 kutoka Kilima cha Harissa ambapo sanamu ya Bikira Maria Mama Yetu wa Lebanon inatazama jiji kwa huzuni. Hapo awali, alihudhuria mazishi ya Padre Pierre El-Rahi, wa Kimaroniti aliyeuawa alipokuwa akimsaidia mwamini wa Parokia aliyejeruhiwa huko Qlayaa, kabla ya kusafiri hadi vijiji kadhaa vya kusini na lori lililobeba misaada ya kibinadamu.
Kusaidia mahali pale penye dharura
Picha na video za Askofu Mkuu akipakua vifurushi akiwa amevalia kanzu, sashi, na kikofia cha kiaskofu (zucchetto) zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ya Lebanon. "Tulishirikiana ili kupakua vifaa vyote ili tuweze kuanza," alisema. "Tulitembelea vijiji sita na kukutana na jamii mbalimbali: Wamaronite, Wakristo mchanganyiko, Waothodoksi, Wagiriki-Melkite, Kilatini, na hata vikundi vyenye wakazi wa Druze na Sunni." Balozi wa Vatican alielezea uzoefu huo kama "wakati mzuri wa udugu" na kushiriki wakati mgumu lakini wa kuchekesha, tukipiga magoti kwenye madhabahu ya kanisa dogo la kijiji, makombora matatu yalirushwa. "Mtu mmoja aliniambia, 'Askofu mkuu, wanakukaribisha.' Tulicheka kuhusu hilo..."
Mtumaini Papa
Askofu Mkuu Borgia alibainisha imani dhabiti ya wenyeji kwa Vatican na Papa. "Watu walihitaji msaada na, zaidi ya yote, neno kutoka kwa Papa. Wanaiamini Vatican na hasa Papa, ambaye walimwona hapa Beirut na ambaye mara moja walihisi uhusiano maalum naye," alisema, akikumbuka ziara ya Papa Leo XIV mnamo Desemba 2025.
Barabara zilizolipuliwa na vijiji vilivyofungwa
Askofu Mkuu alionyesha wasiwasi kuhusu miundombinu iliyoharibika. "Tulisikitika sana kwamba, baada ya kuondoka katika eneo hilo," alibainisha, "baadhi ya barabara zililipuliwa kwa mabomu. Qlayaa, baada ya kutukaribisha, sasa imefungwa kabisa, kama vijiji vingine vilivyo karibu. Wameanza hata kukata njia za mawasiliano kuelekea Kusini. Tunatumai kwamba vita vitaisha hivi karibuni na amani kurejea," alisema.
Hofu na matumaini
Balozi huyo alikumbuka jinsi mashambulizi ya Hezbollah na mabomu yaliyolengwa na Israeli yalivyolazimisha watu wengi kuhama. "Hezbollah," alielezea, "hufyatua makombora na roketi kuelekea Israeli, wakati mwingine mara kwa mara. Israeli hupiga mabomu kwa hiari huko Dahieh, ikilenga magari, mahoteli, makaazi ya watu au nyumba. Vitongoji vyote vya Washia huko Beirut karibu viko tupu kwa sababu ya harakati za watu wengi." Takriban watu 800,000 wamejiandikisha kwa usaidizi kwenye tovuti ya Wizara ya Masuala ya Jamii, huku takriban watu 120,000 wakisaidiwa katika vituo vya ndani. "Watu katika vituo," Askofu Mkuu Borgia alisema, "wanaogopa," akibainisha kwamba, "Ni hali ya kipekee." "Tutumaini mema," alisema.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.